Rais Samia umekosea tena; haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, bali kuongoza Watanzania wa jinsia zote

MWAMBIENI MAMA
____________________

Mwambieni Mama afanye kazi iliyomuweka madarakani kwa mujibu wa Katiba. Yeye ni Rais na si Mwanaharakati wa kupigania haki za Wanawake. Kama anahitaji tumtambue kwa vyeo vyote hivyo viwili basi wacha tumtambue hivyo.

Mwambieni aache kuzungumza maneno ya kejeli na kebehi dhidi ya Wanaume. Kauli zake dhidi ya Wanaume zinazidi kuwa na Ukakasi siku hadi siku. Mwambieni Mama aache dharau, apunguze mipasho na afanye kazi.

Dunia nzima inajua (na hata yeye anajua) kuwa Mwanaume ni Mwanaume na atabaki kuwa Mwanaume tu. Asiendeleze maneno ya kejeli kwa Wanaume kila siku akidhani kwa kufanya hivyo anawasaidia wanawake.

Hakuna aliyewahi kusema kuwa Wanawake hawawezi. Ni hali yake tu ya kutojiamini na kukosa hoja za Msingi. Taifa linamuhitaji ajikite kufanya kazi za maendeleo ya Taifa zima bila kutoa kauli za Uanawake na Uanaume. Afanye kazi aache kutuletea mambo ya U-Feminism kutoka Magharibi.

Kauli zake zinaonesha kama kuna kitu anachokitafuta kwetu. Anahitaji nasi tupande jukwaani na kuanza kurusha vijembe kwa Wanawake kama afanyavyo yeye kwetu.? La hasha, Wanaume ni viongozi, na ndiyo maana tunamuongoza hata yeye arudi kwenye mstari na kufanya yale ya msingi anayohitajika kufanya.

Lakini yapo baadhi ya mambo si ya kuyaacha bila majibu, kwa sababu upotoshwaji unaofanywa kwa makusudi na mtu mzima unaweza kuiathiri sehemu kubwa ya jamii kama hautotolewa ufafanuzi au kujibiwa. Kwa kuzingatia hili ni vyema tuseme kidogo baadhi ya mambo.

Kubeba Mimba na kulea sio hoja kwamba Mwanamke ni zaidi ya Baba. Ni kweli kuwa Mwanaume ndiye mtoa mbegu lakini tusisahau kuwa Mwanaume ndiye mbegu yenyewe iliyowekwa na Mungu duniani ili ienee na kusambaa duniani kote.

Zingatia kuwa Mwanaume ndiye chanzo cha wote, Mama na Watoto wote wanatoka kwenye kiuno cha Mwanaume, hata yeye anayekejeli alitoka kwenye kiuno cha baba yake ambaye ni Mwanaume na wala asidhani umuhimu wa mwanaume ni kuchangia mbegu tu bali hata yeye asemaye hivyo kichimbuko la asili ni 'Mwanaume'.

Wapo baadhi ya wengi wanaokumbwa na propaganda za upotoshwaji wa makusudi katika hili. Wanavikwa pazia kwa sifa ya Mwanamke Kuzaa bila kuangalia Asili haswa ya neno Kuzaa au Uzao ni Nini. Wanadhani labda kuzaa ni sifa ya Mwanamke bila kutambua kuwa sifa hiyo Kimsingi ni ya Mwanaume. (kuelewa hili kutahitaji utulivu haswa)

Kitabu Kitakatifu cha Biblia kinaeleza kwa kina hili katika kitabu cha Mwanzo: 5:3-4. "Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi. Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake."

Hapo ndipo naporejea kwenye msingi wa hoja ili kumaanisha kuwa Kiasili anayezaa na kutoa Uzao ni Mwanaume, na hiyo ndio heshima kuu ambayo Mungu alimpatia Mwanaume katika hii dunia, heshima ambayo pengine kwa makusudi ikageuzwa na dhana kuwa Kuzaa ni sifa ya Mwanamke tu.

Mwambieni Mama hata aseme apinduke hii dunia imewekwa mikononi mwa Mwanaume, na ndiyo maana Mungu alimuumba kwanza na kumpa maagizo na ndipo Mwanaume (baadae sana) akaletewa Mwanamke kutoka kwenye ubavu wake.

Na hata dunia ilipoanguka kosa lilifanywa na Mwanaume, na aliyekuja kuulizwa na Mungu kwa kosa hilo alikuwa Mwanaume pia. Mungu alimuona Hawa lakini aliamua 'kumpotezea' na kuamua kushughulika na Adam kwa kuwa ndiye Kiongozi aliyemchagua kuiongoza hii dunia.

Hata baada ya kutenda kosa hilo, ukiangalia hukumu walizopewa wenza hao (Adam na Hawa) utagundua tu kuwa hata hiki kinachofanywa na baadhi ya Kinamama wenye kauli za 'Ki-Samia Samia' kinakinzana kabisa na kile alichoelekeza mwenye dunia yake.

Hukumu hiyo ilielekeza Mwanaume 'Kula kwa Jasho' na hivyo automatically kuwa na jukumu la kuitunza na kuilea familia, huku Mwanamke akipewa hukumu ya 'Kuzaa kwa Uchungu, Tamaa yake kuwa Juu ya Mumewe na KUTAWALIWA NA MWANAUME.

Mwambie tena Mama, hakuna asiyejua kuwa yeye ni Mwanamke. Kuzungumzia jinsia yake adharani mara kwa mara ni kuonesha udhaifu wake wa hali ya juu unaowakera hata baadhi ya Wanawake wengi wanaojitambua. Kama anahitaji kuwa Kiongozi imara Mwanamke mwenye heshima aache kuwadhihaki Wanaume kila siku na badala yake ajifunze mafanikio ya Madam Angela Merkel wa Ujerumani.

Copied!
 
chewing-kangaroo (1).gif
 
Pamoja na yote kura yangu na mke wangu itategemea kesi ya Mbowe, iwapo haki itatendeka, na hatua kuchukuliwa juu ya shahidi wa tano ambaye hajulikani halipo! Licha ya kushikwa.
 
Yuko sahihi kabisa.

Mh.Rais anavunjavunja MAKUNDI KOKO ya kisiasa ndani ya CHAMA.
...

Huko sio kuvunjavunja Makundi Bali ni kujenga ubaguzi wa kijinsia .
Huko ni kuleta mgawanyiko katika jamii huyu rais kakosea sana
 
Back
Top Bottom