Rais Samia umeandika historia kubwa

Hana lolote , alikua wapi siku zote. Mbona hakufurukuta kwa jiwe. Kwahiyo mama kuwapa uhuru wa kuongea imekua makosa.

Wanajaribu kumtikisa na kumchokoza mama ili wakishushiwa kitu kizito wapate lingine la kupigia debe .
Mama asikubali kutolewa kwenye reli, aendelee ku focus kwenye mipango na maendeleo ya nchi.

Halafu mwingira huwa hawapendi kabisa waislamu sijui kwanini ? Namjua vizuri Sana. Haya yote kusema ikulu Kuna shetani ni kwasababu rais ni muislamu. Hata kipindi cha kikwete alikua anamponda Sana madhabahuni. Na kuupondea uislamu. Kwahiyo kwa hili hata sijashangaa.
Askofu kapiga utosini
 
Mwaka 2021 ni mwaka wa kipekee sana katika historia ya JMT, nchi yetu ilipita katika mtihani mgumu ambao utakumbukwa vizazi na vizazi vijavyo. Kuondokewa na Rais aliyepo madarakani lilikuwa pigo kubwa.

Watanzania tunazo sababu nyingi za kumshukuru Mungu kwa kutuvusha salama na zaidi kwa kujaaliwa kiongozi mwingine mwenye uzalendo, uwezo, na karama isiyo na kifani katika uongozi wa kisiasa ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya mambo yaliyofanywa katika kipindi kifupi sana na Rais Samia;

1. Kuimarisha Uchumi- Ukuaji wa pato la taifa katika robo ya pili mwaka 2021, uchumi uliongezeka kufikia 4.3%, ukilinganisha na 4% mwaka jana. Mfumuko wa bei umeweza kudhibitiwa huku akiba ya fedha za kigeni ikiongezeka zaidi.

2. Kuchochea Biashara- Maboresho ya sheria na miongozo mbalimbali yamefanyika na hivyo kuvutia wawekezaji kutoka katika kila pembe ya Dunia huku uuzaji wa bidhaa (Export) ukiongezeka mara dufu.

3. Kukuza Utalii na kuitangaza nchi yetu - Katika hili Mhe. Rais ameweka rekodi ya aina yake hususani katika program maalum ya "ROYAL TOUR " ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa utalii Duniani kote.

4. Kuendeleza miradi ya kimkakati- Mhe. Rais katika hili ameonyesha umahiri na uwezo mkubwa ambapo mpaka sasa miradi yote inaendelea kama ilivyopangwa huku miradi kama SGR ya Mwanza - Isaka ikitengewa zaidi ya Trilioni 1 kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

5. Kuimarisha Sekta ya Kilimo na Ufugaji- Rais Samia ametatua changamoto nyingi za wakulima na kufungua masoko ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha wakulima wanafaidika na shughuli zao. Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, zilipatiwa zaidi ya Bilioni 129 kununua mazao ya wakulima.

6. Kukuza Diplomasia- Rais Samia ameirudisha nafasi ya Tanzania katika mawanda ya diplomasia za kikanda na kimataifa ikiwemo kushirikiana na mataifa mengine kukabiliana na janga la Corona kwa njia za pamoja, uamuzi huu umekuwa wenye manufaa makubwa.

7. Kuboresha huduma za jamii- Rais Samia amefanya makubwa kuhakikisha huduma za Afya, maji, elimu, umeme na miundombinu zinaboreshwa kila uchao. Hivi sasa tunatarajia hapo mwakani kila mwanafunzi aliye faulu darasa la saba aanze shule moja kwa moja.

8. Kuboresha sekta ya madini- Katika sekta hii Mh.Rais amewezesha utoaji wa leseni takribani 7968, huku viwanda vya uchakataji madini vikiendelea kujengwa na sekta hii ikichangia pato la Taifa kwa takribani 7.7%. Juhudi hizi ni kubwa.

9. Kuhakikisha Amani na Usalama- Kama Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia ameweza kusimamia vema amani na usalama wa nchi yetu licha ya hali tete kwa baadhi ya nchi jirani, umakini na uongozi wake thabiti ndio sababu ya mafanikio haya.

10. *Ajira na fursa kwa watumishi- Rais Samia ametoa vibali vingi vya ajira serikalini, ametoa fedha za malimbikizo ya madeni kwa watumishi, vibali vya kupandisha madaraja kwa wenye sifa na zaidi ameondoa tozo (VRF) 6%kwa watumishi ambao ni wanufaika wa fedha za Bodi ya mikopo (HESLB).

Tukiwa mwishoni mwa mwaka, nitoe rai yangu kwa viongozi wote wa dini na watanzania wote kwa ujumla kumuombea heri Rais wetu, kujiombea heri sisi wenyewe na nchi yetu kwa ujumla ili tuendelee kufurahia ustawi wa nchi yetu.
Kazi nzuri mama, huyu Ndugai amefanya jipi bora zaidi ya kuwa dikteta uchwara. Rais Samia usiogope, litimue hilo Ndugai.
 
Back
Top Bottom