Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na TAKUKURU kwa mwaka 2021/2022 leo Machi 29, 2023 Ikulu ya Magogoni, Dar es salaam.



CP. Salum R. Hamduni, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) amesema taasisi hiyo imefanya ufuatiliaji wa miradi 1548 yenye thamani ya Trilioni 5.64 ikiwemo ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere pamoja na Reli ya SGR kwenye kipindi cha mwaka 2021/22.

Katika miradi ya UVIKO-19, amesema wamebaini baadhi ya miradi kutokuzingatia michakato ya ujenzi, uzabuni pamoja na ununuzi wa vifaa vya ujenzi vyenye thamani kubwa kuliko hali halisi ya soko.

picpolisi.jpg

CP. Salum R. Hamduni, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Pia, walichunguza mifumo 739 ya taasisi za umma ikiwemo Hospitali ili kudhibiti mianya ya rushwa. Uchunguzi huu umebaini baadhi ya bidhaa za afya huathiriwa na kutokufuata utaratibu sahihi wa ununuzi, udhaifu katika udhibiti wa vifaa vya afya katika vituo pamoja na kutokutumika kwa mifumo ya kielektroniki vituoni.

Katika uchunguzi uliofanyika kwenye bandari ya Dar es salaam, eneo la forodha, ukusanyaji wa mapato, ukaguzi wa TBS, kilimo, mifugo na TANROAD una mifumo iliyo na mianya (dhaifu) inayoweza kusababisha upotevu wa mapato.

Katika oparesheni mbalimbali za madai na kesi, TAKUKURU imeokoa Bil. 14.2 pamoja na Dola za Kimarekani 14,571, imechunguza majalada 1188 ya kesi mbalimbali huku 16 kati yake yakihusisha rushwa kubwa. Katika kesi zote zilizokuwa mahakamani, jumla ya watuhumiwa 186, sawa na 39.74% waliachiwa huru kwa kutokupatikana na hatia.

Aidha, kwa mujibu wa ripoti ya REPOA, 77% ya watu waliohojiwa walisema kiwango cha Rushwa nchini kimepungua ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesa ofisi hiyo ilifanyiwa tathimini na Taasisi kubwa za Kimataifa na kupewa 92% ya utendaji kazi. Hii inamaanisha wanafanya kazi nzuri.

Kwenye ukaguzi wa miradi ya UVIKO-19, miradi ilitekelezwa kama ilivyopangwa pamoja na uwepo wa changamoto kadhaa.

20sept-pub-kichere-afr-article1.jpeg

Charles Kichele, CAG
Mwenendo wa utoaji wa hati, ofisi hiyo imetoa hati 1045 kwenye taasisi na mamlaka mbalimbali. Kwenye vyama vya siasa, alitoa hati 19 huku 12 kati yake zikiwa zinaridhisha, hati 5 zina mashaka, hati mbaya 1 na hakutoa maoni kwenye hati 1.

Taasisi ya MOI na Magazeti ya Serikali zimeendelea kutajwa kuwa na hati mbaya pia baadhi ya Taasisi za Serikali zimegunduliwa kuwa zinapokea malipo nje ya mfumo wa GePG.

Amegundua kuwa wakusanyaji kodi katika mamlaka 98 hawakuwasilisha bilioni 11.07 kwenye akaunti kuu ya Serikali. Kutoka ukaguzi wa mwaka uliopita hadi ukaguzi wa waka huu, deni la Taifa limeongezeka kwa 10.5% lakini bado ni himilivu.

Bil 25.95 zimelipwa na Serikali pasipo kuomba risiti za kielektroniki. Hii inadhoofisha ukusanyaji wa kodi kwa kuwa wafanyabiashara wanaweza kutumia mwanya huu kutokulipa kodi.

Ukaguzi wa Serikali kuu, katika ukaguzi wa usambazaji wa maji Same, Mwanga na Korogwe wenye thamani ya bilioni 263.67 haujakamilika hadi sasa, na mikataba yake imesitishwa tangu mwaka 2020 na baadhi ya malipo yalikuwa yamefanyika. Serikali iliingia mikataba mingine pasipo kufunga mikabata ya awali ili kubainisha kazi ipi imefanyika na ipi imebaki hivyo kuongeza gharama kwa zaidi ya 61%. Hadi sasa, hakuna kesi yoyote iliyopo Mahakamani kwa wahusika.

Vishikwambi vya sensa 300, 000 vilivyonunuliwa na Wizara ya Elimu vimegunduliwa kununuliwa pasipo kufuata mlolongo sahihi wa tenda na manunuzi.

Tathimini imeonesha kuwa bado kuna hasara kubwa katika mashirika ya kibiashara ya Umma. Shirika la ndege limepata hasara ya bilioni 35.2, Reli 31.2 na Mkulazi bilioni 14.3.

Shirika la Reli lilimkataa Mzabuni aliyetaka kulipwa Tsh. Bilioni 616.4 na kumpa kazi Mzabuni wa Tsh. Trilioni 1.119 sawa na ongezeko la Tsh. Bilioni 503.2 (82%) lisilokuwa na ulazima.

Pia, katika ununuzi wa 'Locomotives' na Makochi ya Abiria, Shirika la Reli (TRC) lilitekeleza Mkataba bila dhamana ya Utendaji na kusababisha hasara ya Tsh. Bilioni 13.7 kutokana na Mkandarasi kushindwa kutimiza Masharti ya Mkataba.

Shirika la Umma la Simu linajiendesha kinyume cha malengo yake, huduma zake zipo chini ikilinganishwa na kampuni zingine pia haikufikia malengo waliyojiwekea kwenye kupata wateja wapya.

Mifuko ya hifadhi ya jamii imegundulika kuwa na changamoto nyingi kwenye makusanyo na uhifadhi na ukusanyaji wa madeni. Mfano, trilioni 1.49 za madeni hazijarejeshwa kati ya mwaka 1-15 tangu zikopwe.

Baadhi ya taasisi za Serikali zimeendelea kusaini mikataba pasipo kuhakikiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Hadi kufikia Januari 2023, ni 2.5% pekee ya kaya zote ndiyo zilikuwa zimehama, ambapo zaidi ya bilioni 24.76, na zoezi zima litagharimu zaidi ya bilioni 900.

Ujenzi wa SGR umekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo ongezeko la gharama zisizo za lazima. Mfano, Mkandarasi mmoja amelipwa bilioni 13.7 pamoja na kuwa mkataba ulikuwa umevunjwa. Pia, baadhi ya vipande vya mradi vimeshindwa kutekelezeka kwa wakati hivyo kuongezeka kwa gharama.

Ujenzi wa Bwawa la Nyerere, Kichere ameshauri TANESCO kuchukua hatua ili kuhakikisha kuwa unakamilika kwa wakati kama ilibvyopangwa.

Mamlaka 180 za Serikali za Mitaa zimegunduliwa kushindwa kukusanya marejesho ya mikopo inayotolewa kwa vikundi mbalimbali vya kijamii. Pia, baadhi zililipa kiasi kikubwa cha pesa kwenye miradi ya ujenzi kinyume cha gharama halisi.

NHIF imebainika kulipa zaidi ya bilioni 14 kwa vituo vya afya visivyo stahili, hadi sasa hakuna hatua zozote zimechukuliwa kwa wahusika waliofanya malipo haya.

Uchunguzi wa Plea Bargaining umebaini mapungufu ya ukusanyaji na uhifadhi wa fedha ikiwemo kutokutoa risiti za malipo, kutokuwepo kwa daftari la utunzaji fedha, uthibitsho wa makabidhiano ya mali, kukiri kwa watuhumiwa kuwa walionewa katika kulazimishwa kukiri makosa pamoja na kutokuwa na timu maalum ya kuendesha keshi hizo. Kichere amependekeza kuundwa tume maalum ya kiuchunguzi ili kuona kama hakuna harufu mianya ya fedha za umma.

Bilioni 4.8 zimepotea, hivyo hazikuwafikia walengwa (Polisi) kwenye mfuko wa kufa na kuzikana. Jeshi la polisi liwatafute waliohusika na ubadhirifu huo wa fedha.

Mfuko wa TANAPA ulifanya malipo hewa ya bilioni 1.95 yasiyo na viambatanisho. ulipaji wa posho za zaidi ya milioni 30 pamoja na kulipana kwa kazi zingine kinyume cha pesa halali za posho. Pia, milioni 114 zililipwa mara 2 kwa shughuli moja ya uandaaji wa hesabu.

Samia Suhuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepokea ripoti, awali amezishukuru taasisi hizi kwa kuandaa ripoti nzuri zinazotoa dira ya utawala bora na udhibiti wa mapato ya Serikali.

SAMIIIIA URAIS.jpg

Samia Suluhu Hassan, Rais
Ameitaka Taasisi inayohusika na manunuzi ya Serikali GPSA kupunguza urasimu katika manunuzi ili bidhaa na huduma zifike haraka kwa walengwa. Pia ametaka iangaliwe kama bado ina umuhimu kwa kuendelea kuwepo.

Bandari na TRA hawasomani bandarini, Rais amehoji kwanini mifumo yao haisomani. Ametaka taasisi hizi kutatua kero hii haraka, ikiwezekana kukaribisha private sector ili iongeze ufanisi wa kazi.

Ametoa karipio kwa maafisa masuhuli kuacha tabia ya kutokulipa kwa wakati ili wapate riba. Amesema hatua kali zitaanza kuchukuliwa kwa yeyote atakayefanya uzembe wa aina hii, ni lazima pesa zianze kulipwa mapama ili wakandarasi waendelee na kazi zao.

Kuhusu Mashirika ya Umma kupata hasara, Rais metolea mfano NDC kupata hasara kila mwaka tangu kuanzishwa kwake, badala ya kuleta faida kila mwaka hutumia pesa za Serikali kujiendesha na kulipa wafanyakazi.

Kwa kuwa lengo la kuanzishwa kwa mashirika hayo ilikuwa ni kuleta faida Serikalini, tathimini inapaswa kufanywa ili yanayofaa yabaki na yasiyofaa yafutwe.

Manunuzi ya Vishikwambi vya Sensa yaligharimu bilioni 10, pia gharama za awali za ununuzi wa ndege ya mizigo ilikuwa ni dola milioni 37 lakini gharama za mwisho imekuwa dola milioni 86. Amesema huu ni upigaji na wanaofanya hivyo hawafai kuwa kwenye nafasi zao hivyo wapishe.

TTCL imetakiwa kujitazama upya kama inaweza kuendelea kujiendesha, pia watathimini kama biashara wanayofanya wanaweza kuimudu.

Bima ya afya bado imekuwa tatizo kubwa. Kwa mujibu wa Rais Samia, pamoja na kujenga vituo vingi vya afya na kununua vifaa vya kisasa, Serikali inaweza kushindwa kuhudumia watu hivyo atatafuta muda mwingine kulizungumzia.

Bilioni 88 iliyotolewa kwevye vikundi vya kinamama na walemavu haijakusanywa na haikusanyiki. Vikundi vingi ni hewa, na wengine wamepata fedha hizo kwa sababu za kisiasa. Rais ametaka mabadiliko makubwa yafanyike ili pesa hizo zianze kutolewa kupitia benki.
 
Sasa hata tukifuatilia haita ondoa ujinga ujinga unaofanywa serikali coz wanaotakiwa wafuatilie ni serikali na sio sisi, raia tunahitaji kuona serikali ikifanyia kazi mapendekezo ya CAG na sio et tufatilie kupewa nyaraka ambazo hawatazifanyia kazi ok.

Mara ngapi ofisi ya CAG ikitoa mapendekezo yake serikali haifuatili tena na chuki kuundiwa CAG hadi ofisini anatimiliwa kama mbwa, et hao ndo serikali ya wanyonge pumbavu zao.

Hata sasa hii ofisi ya CAG ni upumbavu, tayari hii ofisi ilishakosa sifa kwetu sisi raia, tunahitaji CAG office iliyokamili sio hii iliyochakachuliwa sema tu watanzania hatujitambui make wengi wetu ni mashabiki tu, tena hawajui nchi inatakiwa iendeshwaje.
 
Wakitoka hapo wanaenda kubonyeza mapochopocho na whisky, posho nene nene zinafuatia na vicheko vya ulambaji asali, wanaagana kila mtu kwake. Ya mbele ya kamera ni tofauti na ya nyuma ya kamera!

Wanatuahadaa mengi sana kuliko uhalisia.
 
Back
Top Bottom