Rais Samia: Ukiwa Sekta binafsi ajira ni nguzo yako ya maisha sio by the way

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kubadilika kwa kutambua kwamba Ajira ndiyo nguzo ya Maisha hasa ukiwa sekta binafsi hata Serikalini huku akiongoza "sekta binafsi ukizubaa nafasi yako inachukuliwa".

Amefafanua "Nilishawahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, wakati ule kesi nyingi nilizokuwa nikipokea ni uzembe, kutokuwa na nidhamu sehemu za kazi, umefiwa na shangazi wa shangazi yako unakwenda kuzika bila kutoa taarifa".

Ameyasema hayo akiwa kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Nguo cha Basra Textile Mills Limited Visiwani #Zanzibar. Kiwanda hicho kinachotarajiwa kuzalisha Nguo siku za usoni, kwa sasa kinazalisha vitambaa tu.
 
HIYO SI NI KAZI YA WAZIR AU RAIS MWINYI,, HIVI HIZO GHARAMA ZA KUTOKA DODOMA KURUDI ZANJ,, HIVI INAMAKE SENSE
 
Mara tujiajili mara ajira ni nguzo , sasa kama ni nguzo mbona huajili vijana ? .
 
Mara tujiajili mara ajira ni nguzo , sasa kama ni nguzo mbona huajili vijana ? .
Hivi una hata data za ajira zilizotolewa na serikali kwa kipindi chake akiwa ikulu mpaka sasa au unajiropokea tu?
 
yaani huyu mama hajielewi elewi, yaani yeye bora kuche na kuchwee basiii…………..
 
Mhe.Rais Ajira za Sekta binafsi hawalipi vizuri,nyingi zinawafaidisha wafanyakazi wa Nje Kuliko Wazawa,Wazawa Wengi pia Ajira zao ni Mguu ndani mguu nje Hawathaminiwi na Hao Waajiri wa Sekta binafsi ndio Maana unasikia by the way.
Mawaziri na Katibu wa Wizara inayohusika na hayo mambo ya kazi wengi wao wamelala hawajali Kwa lolote.Ila Sekta binafsi nyingi Zina uozo mwingi Sana mhe.Rais
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom