Rais Samia: Tuziangalie Sheria za Uchaguzi zisiwanyime haki wanaokosea kuandika majina yao

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza sheria za uchaguzi kuangaliwa upya ili zisitumike kuwanyima haki wagombea wanaokosea kujaza majina au herufi ya chama chake hali inayosababisha wagombea wengine kupita bila kupingwa.

Ameeleza hayo Jana Jumamosi Agosti 21, 2021 katika hafla ya kupokea taarifa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi amesema sheria zisitumike kuwanyima watu haki kwa masuala ya kiufundi, "hatuna budi kuziangalia sheria zetu ili zisitumike kuwanyima watu haki kwa masuala ya kiufundi, mathalani pale mtu anapokesea kuandika herufi za jina lake au herufi za chama chake nadhani mipango ingewekwa vizuri zaidi."

“Nilijua vyama vya siasa mtashangilia hili kwa sababu tuliwashughulikia kweli uchaguzi ulipita kila mlipokosea tuliwaweka pini na mkatupa fursa ya kupita bila ya kupingwa sasa tutaliangalia vizuri na nyie muwe makini basi vinginevyo…, " amesema Samia.
HAKUNA MAJINA YALIYOKOSEKANA ILA NECCCM ILIFANYA YAKOSEKANE

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Nao wapinzani wana mambo ya kipuuzi , inakuwaje Wana mgombea hawezi kuandika jina lake na la chama chake vizuri kwanini wasimsaidie kumjazia badala ya kumwacha aboronge?
NDUGU,
Kama na wewe kabisa kutoka moyoni mwako unaamini na kufurahia porojo hizo za watoto wa chekechea, basi tuna safari ndefu ya kufika kwenye FIKRA ziletazo maendeleo.
 
Hahahahah

Enzi zile zimeshakuwa tbt

Nakumbuka mgombea Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa sehemu fulani toka vyama korofi alipingwa kwa hoja hajui kuandika, alipotakiwa athibitishe aandike akatakiwa aandike 'Zwangendaba' alipokosea herufi moja akakatwa
Kama alivyoanza Maushungi,
Nanyi mmeanza kushindana kwa 'hekaya za abunuasi', LAKINI kadiri muda unavyoenda na nafsi zinavyozidi kuwasuta, nina hakika, mtakuja TU kutueleza ukweli vizuri kabisa jinsi mlivyoiba kura. Huko ndio kuweweseka.
 
Nao wapinzani wana mambo ya kipuuzi , inakuwaje Wana mgombea hawezi kuandika jina lake na la chama chake vizuri kwanini wasimsaidie kumjazia badala ya kumwacha aboronge?
Hivi inaingia akilini kwamba kukosea jina kunasababisha mtu akose haki ya kupigiwa kura?
Ikulu yenyewe inakosea na kutoa majina katika halmashauri mbili tofauti, nayo utasemaje?
 
Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Tanzania anapoakea ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2020, Ikulu Dar. Katika Uchaguzi huo, Mgombea wa CCM Hayati Rais John Magufuli akiwa na Samia Suluhu kama Mgombea mwenza walishinda

Rais Magufuli alipofariki Machi 2021, aliyekuwa Mgombea mwenza Samia Suluhu akaapishwa kuwa Rais



Rais Samia: Tuziangalie sheria zisiwanyime haki wanaokosea kuandika majina yao

Rais Samia Suluhu amesema sheria za uchaguzi ziangaliwe ili zisiwanyime haki wagombea kwa makosa ya kiufundi

Makosa hayo ni kama kukosea herufi za jina lake au la chama
=====

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema Uchaguzi MKuu wa Mwaka 2020 uligharimu Tsh. 262,493,380,671 ambayo iligharamia ununuzi wa Karatasi za kupigia kura, Mafunzo, Ununuzi wa masanduku na uchapishaji nyaraka
-
Pamoja na gharama hiyo, jumla ya Tsh. 154,313,824,607.88 ilitumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
-
Tume ya Taifa imesema gharama zote ziligharamiwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

NEC: TULIPOKEA RUFAA 165 NGAZI YA UBUNGE
-
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeripoti kupokea jumla ya rufaa 165 za Ubunge ambapo, rufaa 67 zilizotaka Wagombea kurudishwa kwenye kinyang’anyiro zilikubaliwa, 31 zilikataliwa. Rufaa 4 zilizotaka Wagombea kuondolewa zilikubaliwa
-
Wasimamizi wa Uchaguzi walipokea mapingamizi 1,298 ambapo mapingamizi 451 yalishindwa kuamuliwa na kufika Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambapo Wagombea Udiwani 235 walikubaliwa kurejea katika kinyang’anyiro, mapingamizi 154 yalikataliwa. Rufaa 62 zilizotaka Wagombea kuondolewa zilikataliwa

Rais Samia: Uchaguzi tuligharamia wenyewe, ulimwengu haukuamini kama tungeweza kugharamia wenyewe



Rais Samia, Niwaombe wadau waangalie mapendekezo yaliyotolewa na wayalete serikalini tuangalie namna ya kuyafanyia kazi

Samia ni hatari kwa mstakabali wa ccm. Sheria za uchaguzi zimewekwa kwa madhumuni maalum. Kama mtu hata hawezi kujaza fomu ya kuomba ugombea hafai. Na kama chama hakiwezi kuelekeza wagombea wake namna ya kujaza fomu hakifai. Samia ana hulka kujipendekeza kwa wapinzani ili kuwafurahisha wazungu. Hajui lengo lao ni hatimae kuchukua madaraka toka ccm na huku agenda zao kuikabidhi nchi kwa mabeberu.
 
Kwani ukielezwa ulivyoibiwa inakusaidia nini?
Kama alivyoanza Maushungi,
Nanyi mmeanza kushindana kwa 'hekaya za abunuasi', LAKINI kadiri muda unavyoenda na nafsi zinavyozidi kuwasuta, nina hakika, mtakuja TU kutueleza ukweli vizuri kabisa jinsi mlivyoiba kura. Huko ndio kuweweseka.
 
Anaongelea kitu hakimuhusu yeye alipigiwa kura na nani?! mpaka aongelee uchaguzi? Mimi simuelewi kabisa asubuhi nimeweka 3500 m. Pesa nikanunua luku daaaah pesa wamekata wamenipa unit 3 ?
Ukiweka tick unaweka ya rais na makamu wake
 
Sham democracy.

Kwenye demokrasia geresha ndio kuna mambo ya mapingamizi na kuengua wagombea ili kuondoa ushindani.

Sheria na kanuni zote zinazoipa tume mamlaka ya kupokea mapingamizi na kuengeua wagombea zinapaswa kufutwa kwa sababu zinakiuka msingi mzima wa demokrasia ya vyama vingi na ushindani.

Sheria inapaswa kuwa kwamba wagombea waenguliwe kama sio raia au ni whalifu tena kupitia mahakama na sio tume au kamati.
 
Samia ni hatari kwa mstakabali wa ccm. Sheria za uchaguzi zimewekwa kwa madhumuni maalum. Kama mtu hata hawezi kujaza fomu ya kuomba ugombea hafai. Na kama chama hakiwezi kuelekeza wagombea wake namna ya kujaza fomu hakifai. Samia ana hulka kujipendekeza kwa wapinzani ili kuwafurahisha wazungu. Hajui lengo lao ni hatimae kuchukua madaraka toka ccm na huku agenda zao kuikabidhi nchi kwa mabeberu.
Ukifuatilia kesi ya ugaidi wa Mbowe mahakamani kulingana na Kingai pamoja na maamuzi mengi ya jaji dhidi ya upande wa utetezi utaelewa kuna curable errors (makosa yanayotibika kisheria) kwenye kuandaa na kujaza fomu.
 
Back
Top Bottom