Rais Samia tusaidie Watanzania wote tuweze kumiliki ardhi Zanzibar

1. Zanzibar ni nchi kamili huwezi kumiliki ardhi kama hauna sifa.

2. Halafu nafasi za uongozi wanazotamba nazo ni za muungano, maana Zanzibar ni sehemu ya muungano, hakuna nchi Inaitwa Bara duniani kwasasa
Zenji sio Nchi kamili tukiwaachia soon mtaanza kulialia maana Global warming inaongeza kina cha maji na baada ya miaka takribani 50 zenji itabakiwa na nusu ya ardhi mlionayo. sa sijui mtakimbilia wapi
 
Zenji sio Nchi kamili tukiwaachia soon mtaanza kulialia maana Global warming inaongeza kina cha maji na baada ya miaka takribani 50 zenji itabakiwa na nusu ya ardhi mlionayo. sa sijui mtakimbilia wapi
Tatizo mnapenda sana kusemea watu, tuachieni nchi uone kama mtu atalia, Zanzibar ni nchi kamili ndio maana ipo mpaka sasa, Tanganyika ni nchi ya kwenye makaratasi tu
 
Sijui tunakwama wapi sisi Watanganyika!!!
Watanganyika milioni 60 tumeshindwa kumtoa kiongozi miongoni mwetu atutawale, kaja mvaa ushingi toka miongoni mwa watu milioni 1 ndio kawa kiongozi wetu.
Hiyo si ajabu, ajabu ni kwamba sisi watu milioni 60 hatuwezi hata kumweka Mwenyekiti wa mtaa mwembe togwa kule Zanzibar.
Hivi unajuwa kuwa Aboud Jumbe Mwinyi Rais wa pili wa Zanzibar amezaliwa Mji Mwema na baada ya kujiuzulu alirudi kwao mpaka alipokufa ndio watoto wake wakamzika Zanzibar. Jumbe alioa Mzanzibari. Pia, Ali Hassan Mwinyi si kwao T/Bara kwa baba na mama na alikuja Zanzibar kulelewa na pia akawa Rais Zanzibar. Hivi sasa Dkt. Hussein Mwinyi pia ni wa kote Zanzibar na T/Bara na Rais wa Zanzibar na huku hata watu hawalalamiki. Ili uwe mzanzibari na kuweza kupata haki zote ikiwemo kupiga kura kwa Rais wa Zanzibar pamoja na kumiliki ardhi na kupata kitambulisho cha Mzanzibari unahitaji kuishi Zanzibar miaka 10 tu. Acheni longolongo
 
Unaijua Katiba ya Zanzibar wewe kubwa Jinga
Acha kuhamisha magoli .. Mh Samia anaweza kuwa Rais wa Zanzibar na akawa Rais wa Tanzania kama Mtanzania yoyote yule. Mzee Mwinyi alitoka bara akawa rais wa Zanzibar na baadae kuwa rais wa Tanzania, hayo mambo ya katiba ya Zanzibar au ya Tanganyika bakia nayo mwenyewe .
 
Mh Rais, Bwana asifiwe!

Nimatumaini yangu wewe ni mzima wa afya na sisi Watanzania tunaendele kukuombea uendelee kuwa na afya njema. Mh Rais wewe umeonesha wazi ni mpenda haki na ni wazi umeonesha unataka muungano ulio imara kabisa bila kujali chochote umehakikisha Wazanzibari wanapata nafasi mablimbali huku bara na bila kusahau umehakikisha Wazanzibar wananufaika na Muungano wetu.

Mimi naleta ombi moja kwako kuhakikisha unachukua hatua za kutusaidia sisi wa bara kumiliki ardhi kule Zanzibar na pia kushiriki kikamilifu kwenye serikali ya Zanzibar hasa kwenye nafsi za uteuzi kama Wazanzibar wanavyotamba kwenye nafsi za uteuzi huku bara na hii itaimarisha sana Muungano na undugu wetu.

Ni hilo tu Mh Rais.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ardhi ya Zanzibar itamilikiwa tu na mzanzibar. Ushauri wako Ni nzuri Ila upeleke kwa raisi wa Zanzibar ili aufanyie kazi. Raisi wa jamhuri Ni kumtesa tu mama wa watu.
 
Back
Top Bottom