Rais Samia tusaidie Watanzania wote tuweze kumiliki ardhi Zanzibar

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,656
2,000
Mh Rais, Bwana asifiwe!

Nimatumaini yangu wewe ni mzima wa afya na sisi Watanzania tunaendele kukuombea uendelee kuwa na afya njema. Mh Rais wewe umeonesha wazi ni mpenda haki na ni wazi umeonesha unataka muungano ulio imara kabisa bila kujali chochote umehakikisha Wazanzibari wanapata nafasi mablimbali huku bara na bila kusahau umehakikisha Wazanzibar wananufaika na Muungano wetu.

Mimi naleta ombi moja kwako kuhakikisha unachukua hatua za kutusaidia sisi wa bara kumiliki ardhi kule Zanzibar na pia kushiriki kikamilifu kwenye serikali ya Zanzibar hasa kwenye nafsi za uteuzi kama Wazanzibar wanavyotamba kwenye nafsi za uteuzi huku bara na hii itaimarisha sana Muungano na undugu wetu.

Ni hilo tu Mh Rais.
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,156
2,000
Mkuu Leak, aridhi za kumilikishwa au kusaidiwa kumili, hata huku bara, hazipo! Wewe pambania kumiliki au fursa yoyote uitakayo, lakini ukisubiri kutafuniwa, utakufa masikini

Hoja yako ni Sawa na wanao sema tukiruhusu uraia pacha, wageni watachukua aridhi yetu, lakini ukiwachunguza hawana hata kipande cha aridhi!

Kwetu magomvi ya aridhi, wala hatugombani na wageni, ni ndugu wa tumbo moja! Wana makesi mahakamani, wanalogana na hata kuuana kwa ajili ya aridhi!

Point yangu ni kwamba, aridhi inaweza kuwa baraka au laana, na hiyo haitajalisha kama unawania kumiliki na Mzanzibari, Mmarekani au kaka yako
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,156
2,000
Kwa hiyo sheria inaruhusu mtanganyika kumili ardhi zanzibar?
Sijui! Lakini kuna mahitaji hayo? Na kama yakiwepo siyo suala la raisi, ni suala la mchakato wa kuangalia mkataba wa muungano wetu kwa jumla.
Ila kingine mkuu wangu, Leak, Zanzibar ni ndogo sana, hata Chato (Mkoa mtarajiwa) ni kubwa! Sasa hata wangesema Aridhi ni nje nje pale, afu wengi tukachangamkia fursa, tutatoshea pale?!
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,799

Mbona Dar ni ndogo na hakuna kuzuiana kumilikia ardhi

Zanzibar ni wabinafsi ova!
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,656
2,000
Sijui! Lakini kuna mahitaji hayo? Na kama yakiwepo siyo suala la raisi, ni suala la mchakato wa kuangalia mkataba wa muungano wetu kwa jumla.
Ila kingine mkuu wangu, Leak, Zanzibar ni ndogo sana, hata Chato (Mkoa mtarajiwa) ni kubwa! Sasa hata wangesema Aridhi ni nje nje pale, afu wengi tukachangamkia fursa, tutatoshea pale?!
Sasa mbona wanalilia haki sawa kama hoja ni ukubwa?
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,480
2,000
1. Zanzibar ni nchi kamili huwezi kumiliki ardhi kama hauna sifa.

2. Halafu nafasi za uongozi wanazotamba nazo ni za muungano, maana Zanzibar ni sehemu ya muungano, hakuna nchi Inaitwa Bara duniani kwasasa
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,656
2,000
1.Zanzibar ni nchi kamili huwezi kumiliki ardhi kama hauna sifa
2.Halafu nafasi za uongozi wanazotamba nazo ni za muungano, maana Zanzibar ni sehemu ya muungano, hakuna nchi Inaitwa Bara duniani kwasasa
afya ni jambo la muungano?
 
ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,480
2,000
Mbona afya si swala la muungano stil Samia kamteua mzanzibari kuwa naibu waziri 'tena ni yule naibu waziri asiyejua kusoma'
Samia ni Rais wa muungano, na anaongoza serikali ya muungano, anaweza kuchagua yeyote yule kutoka pande yeyote ya muungano, Samia sio Rais wa hiko mnachokiita Bara ,ni wa muungano
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom