Rais Samia tusaidie, Polisi wanatumaliza, Polisi ilindeni CCM itawale milele ila roho zetu tuachieni

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Najua Polisi wa Tanzania wamejipa jukumu la kuhakikisha rais unatawala Milele. Waambie wakutetee lakini roho zetu watuachie. Watanzania wote ni ndugu uwe Polisi Mgambo au Mpiga debe

Soma Ujumbe kaandikiwq baba Askofu

=====

POLISI WAFANYA MAUAJI YA KUTISHA KIJIJI CHA IKWAMBI, KATA YA MOFU, MLIMBA KATIKA WILAYA YA KILOMBERO, MOROGORO!

Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!

Huku kwetu katika Kijiji cha Ikwambi, Kata ya Mofu, katika Halmashauri ya Mlimba (Jimbo la Uchaguzi la Mlimba) Wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro kumetokea mauaji ya kutisha ya raia wawili yaliyofanywa na Jeshi la Polisi kutoka Ifakara Mkoani Morogoro.

Chanzo cha mauji hayo ni migogoro ya muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji. Wakulima wamekuwa wakilalamika kwa uongozi wa Kijiji na Kata kuhusu kuharibiwa mazao yao pamoja na kupigwa na wafugaji kila mara wanakienda mashambani kulima. Tatizo hilo halijawahi kupatiwa ufumbuzi. Kuna hisia kuwa wafugaji huwahonga viongozi. Baada ya kuchoshwa na matukio hayo, wakulima waliamua kundamana leo asubuhi tarehe 23 Oktoba 2022 kwenda katika Ofisi za Kijiji. Wakawakamata Wenyeviti wa Vitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji, Diwani pamoja na Polisi Kata, wakawaweka chini ya ulinzi na kuwafungia ndani ya Ofisi

Baada ya hapo, Polisi kutoka Mlimba walifika eneo la tukio na baadaye wakaongezewa nguvu na Polisi kutoka Ifakara. Baada ya majadiliano kati ya Polisi na wananchi kuwa magumu, Polisi walianza kupiga mabomu ya machozi na baada ya mabomu kuwaishia wakaanza kutumia silaha za moto na kuua watu wawili kwa kuwapiga risasa za kifuani na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Baada ya mauaji hayo, Polisi wakaondoka na kukimbia na viongozi wa viongozi, Kijijini, Polisi Kata na Diwani na kuondoka nao na kuacha miili ya marehemu mahali pale ikiwa inazagaa!

Tunaomba Baba Askofu tusaidie ujumbe huu ufike hata Kwa wakubwa maana huku kwetu mawasiliano ni hafifu na mambo kama haya ni rahisi kunyamaziwa.

Ni Mimi ...
Mwanachi wa Kijiji cha Ikwambi,
Kata ya Mofu, Mlimba,
Wilaya ya Kilombero, Morogoro
23 Oktoba 2022.
 
Neno moja tu kwenu tiini Sheria bila shuruti.. baasi..tatizo lenu mnataka kupambana na police mkiumizwa mnakimbilia kutafuta huruma ya wananchi..nani atawasikiliza..mnadhani police anaamka tu na kuua watu
 
Ujumbe "kaandikiwa baba Askofu", ishara kwamba matumaini kwa wengine hayapo!

Hii taarifa kama ina ukweli wowote ndani yake, hii ni ishara kwamba Tanzania ina hali mbovu sana kwa sasa hivi kuliko tulivyowahi kuifikiria.

Vyombo vya usalama havina ushirikiano na haviaminiwi na wananchi?

Na haya mambo maovu yanatokea kama mzaha mzaha vile. Serikali haioni hatari inayotokana na hali kama hii?
 
Wananchi waliteka serikali ya Kata/kijiji kwa ufupi na kuwafungia ndani!....hii ni hatari zaidi.

Siafiki mauaji ya aina yeyote ya mtu. Lakini katika hili kuna sehemu wananchi hawakufanya sahihi.
 
Neno moja tu kwenu tiini Sheria bila shuruti.. baasi..tatizo lenu mnataka kupambana na police mkiumizwa mnakimbilia kutafuta huruma ya wananchi..nani atawasikiliza..mnadhani police anaamka tu na kuua watu
Inaelekea uwezo wako wa kusoma na kuelewa kilichoandikwa ni mdogo sana. Lakini inawezekana pia ikawa wewe ni mmoja wa waliojitoa akili wasiweze kamwe kutafakari na kuona tatizo liko wapi.

Watu kama nyinyi ni mzigo katika jamii, lakini hakuna njia za kuwaondoa msieneze upumbavu katika jamii mnayoishi.

Njia pekee iliyopo ni kuwavumilia tu na kuwapuuza.
 
Wananchi waliteka serikali ya Kata/kijiji kwa ufupi na kuwafungia ndani!....hii ni hatari zaidi.

Siafiki mauaji ya aina yeyote ya mtu. Lakini katika hili kuna sehemu wananchi hawakufanya sahihi.
Hao waliofungiwa ni sehemu muhimu ya tatizo, na wananchi hawana njia nyingine yoyote ya kuwaajibisha. Hawa ni watu wanaowekwa tu madarakani bila ridhaa ya wananchi, sasa wanapowakandamiza wananchi wanaokandamizwa wafanye nini?
 
Yaani unamweka polisi chini ya ulinzi, wanakuja kwa ajili ya mazungumzo unakiri kuwa mazungumzo yanakuwa magumu. Wanatumia mabomu ya machozi bado unakomaa tu kupambana nao tena unasema kuwa mpaka kieleweke. Unadhani ungekuwa wewe polisi ungelifanya nini? Yaani polisi wenzenu wamewekwa kizuizini mnaenda kwa mazungumzo waliomshikilia wanaweka masharti yasiyotekelezeka. Ulitaka wakubaliane nanyi?
 
Polisi walipambana na Waasi,).

Nini ilikuwa lengo lao kuwateka viongozi wote wa kata pamoja na Polisi jamii?

Je!
Kama mlikuwa na nia nzuri nao,kwa nini hamkuwakabidhi kwenye mamlaka za kisheria baada ya kuwafikia hapo kijijini?

Na nini mdio ilikuwa lengo na dhamira yenu kubwa hasa,baada ya kuwateka?

Na kama hamkuwa na nia ya kuwadhuru,ni kwa nini mliendelea kuwashikilia hata pale Jeshi husika lilipokuja hapo?

Kama Polisi,waliishiwa Mabomu ya Machozi, huku Raia wakiendelea kuwashambulia.
Walitarajia Polusi haocwatumie Mawe kujihami,huku Wakiwa na Bunduki?

Jaribuni kuwa mnatumia njia stahiki kutafuta suluhu za migogoro kama hiyo.
Badala ya kuamzisha "Uasi" dhidi yaamlaka za Dola.

Tabia hiyo ikiachwa bila kukomeshwa itaweza kuinekana na kusambaa zaidi kwenye jamii na hatimae kuwa mbaya zaidi.

*Sasa # Huyu askofu mliemuamdikia ni kwa nini hamkumuandikia kabla hamjazalisha Uasi huo?

Sasa hivi hawezi kuwasaidia maana nyinyi tayari mnahesabika kama wahaini wa serikali na msidhani kwamba,kuondoka kwa hao Polisi ndio yameisha.
Bali ndio kwanza hali ya HATARI imeanza.

Na itawagharimu sana siku zijazo,kuanzia hiyo juzi.

Alamsikhi!
 
Hao waliofungiwa ni sehemu muhimu ya tatizo, na wananchi hawana njia nyingine yoyote ya kuwaajibisha. Hawa ni watu wanaowekwa tu madarakani bila ridhaa ya wananchi, sasa wanapowakandamiza wananchi wanaokandamizwa wafanye nini?
Wafanye chochote ila sio kumteka askari kata, mwenyekiti, mtendaji au yoyote yule. Na nadhani umeona madhara yaliyotokea
 
Napajua kule hawa jamaa wa kanda ya ziwa huwa wanafungulia mang'ombe yao usiku kwenye mashamba ya wakulima.
 
Hao waliofungiwa ni sehemu muhimu ya tatizo, na wananchi hawana njia nyingine yoyote ya kuwaajibisha. Hawa ni watu wanaowekwa tu madarakani bila ridhaa ya wananchi, sasa wanapowakandamiza wananchi wanaokandamizwa wafanye nini?
Wawafungie ofisini ili hasira zao wananchi zikipanda wawawashe moto!...hili ndio jambo jema?...kwamba hawana njia nyingine ya kuitisha mkutano mkuu wa kujiji na kuwapiga chini wote?
 
Wafanye chochote ila sio kumteka askari kata, mwenyekiti, mtendaji au yoyote yule. Na nadhani umeona madhara yaliyotokea
Ndiyo, nimeona madhara yaliyotokea, lakini wewe hudhani kwamba kuna siku madhara makubwa zaidi upande wa pili yanaweza tokea? Kama huoni hilo, utakuwa umeficha kichwa chako ukidhani huonekani kwa watu wanaokutazama.
 
Wawafungie ofisini ili hasira zao wananchi zikipanda wawawashe moto!...hili ndio jambo jema?...kwamba hawana njia nyingine ya kuitisha mkutano mkuu wa kujiji na kuwapiga chini wote?
Mimi sijasema "ndio jambo jema", lakini inaonyesha wewe unaona ni jambo jema kwa wananchi kutendewa isivyohaki na hao unaowatetea wewe.
Hayo ni matokeo ya matendo ovu wanayofanya hao waliofungiwa ndani.
Sijui kama hao wananchi walikuwa na "njia nyingine ya kuitisha mkutano mkuu wa kijiji...", kwani kama umesoma kilichoandikwa hapo ni kwamba hili halikuwa linawezekana.

Mambo kama haya ni mwanzo tu. Fundisho si kutia woga watu, bali hao wanaowaumiza wenzao watambue kwamba hata wao wanaweza kukutwa na hali hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom