Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 90
- 261
DAR: Rais Samia Suluhu Hassan amesema kila anapozunguka Mikoani changamoto ya kwanza anayokutana nayo ni upungufu wa Watumishi wa Afya na Elimu lakini hali hiyo inasababishwa na Sekta hizo kuhudumia Watu wengi na zina mambo mengi.
Akizungumza katika Kilele cha Kumbukizi ya 3 ya Urithi wa Mkapa, Rais ameongeza "Lakini pia, Watu wanaongezeka kwa haraka mno, tunazaliana wengi mno, mahitaji ni makubwa mno na ndiomana kila tunavyoajiri Watumishi hawatoshi".
Aidha, amesema "Kwa bahati mbaya ajira hizi zinaendana na ukuaji wa Uchumi, na ndio maana Uchumi ukikua kidogo tunasema ajira ziende Sekta ya Afya na Elimu, hatuangalii sekta nyingine na tunafanya haraka isijetokea kitu kikashusha Uchumi tukashindwa kuajiri"