Rais Samia Tunashukuru kwa madarasa. Je, ajira za Walimu lini?

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
478
962
Natumai Mko wazima mabibi na mababu.

Kwanza napenda kuchukua nafas hii kumshukuru Rais samia kwa ujenzi wa madarasa 12,000 ya sekondari na 3000 shule shikizi kupitia pesa ya mkopo ya uviko 19.

Serikali imekuwa ikisifia uongezwaji wa madarasa na kwamba wanafunzi wataanza shule kwa pamoja, wamekuwa wakisifia ongezeko la wanafunzi wa awali, darasa la kwanza, na form 1.

Katika hali hyo imekuwa ikinipa mawazo hawa watoto wataenda fundishwa na kina nani huko madarasani!?? Km kuna shule shikizi mpya za msingi zilizosajiliwa na kujengwa je wanafunz wataenda fundishwa na nani aliyakuwa ajira za walimu hazitolewi! , sekondar kumeongezeka mikondo na ukwel idad ya wanafunz n kubwa je watt watafundshwa na nan ikiwa walimu waliopo mashuleni tu hawatoshi.

Mh rais n kwel umetatua kwa asilimia kubwa changamoto za madarasa lakini bado kuna changamoto kubwa sana ya walimu ktk hzo shule, bila kuongezwa ajira za walimu hao watoto watakuwa wanaenda kushinda kwenye madarasa mapya bila kupata elimu, baada ya shule kufunguliwa tarehe 17 tutegemee kusikia wanafunzi wakisema wameenda hawajasoma chochote, mara hakuna mwalim wa sayansi shuleni, mara mwalimu mmoja mikondo mingi n.k

Ata km tamisemi watataka kufanya msawazo wa walimu kwamba wawapeleke kwny hzo shule ukweli n kwamba walimu wenyewe hawatoshi waliopo kwny system, shule iko mjini tu lkn ina uhaba wa walimu huo msawazo utafanikiwa vipi.

Mh Rais ww ni mpenda maendeleo na upo hapo kuhakikisha ili taifa linapiga hatua, kwa heshima na taadhima tunakuomba toa ajira za walimu ili watoto wetu wakiwa kwenye madarasa mapya huku wanapata maarifa stahiki kutoka kwa walimu wabobezi.

La madarasa na madawati tayari mama je la AJIRA za WALIMU ni LINI mama!?
 
Huwa najiuliza Sana Hawa viongozi wetu wanaishi sayari ipi kwamba hawaoni hii changamoto, baadae najijibu wameamua Bora liende haiwahusu Wala changamoto hiyo haigusi kamwe maisha yao moja kwa moja Bali watoto wamama Tanzania.
 
Ajira ni mpaka uchumi ukue😁😁😁
F1Nr.png
 
Kwa experience yangu hakuna mtoto wa kiongozi anayesomea government hivyo hawana machungu huwezi amini hapa arusha mjini kuna shule inaitwa sinoni secondary wanafunI waliopangwa form one ni zaid ya 900 ila vituko sasa Kwanza wanakaa chini pili hawajui walimu wa secondary wanafanaje
 
Back
Top Bottom