Rais Samia, tunaomba ziara ya kikazi mkoa wa Dar es Salaam hasa hasa wilayani Ubungo

Kwaasenga

Member
Jan 28, 2023
73
102
Wana Dar es Salaam tuna changamoto nyingi sana. Lakini ya barabara imekithiri sana. Tunaomba ziara Dar es Salaam tukueleze shida zetu. Dar es Salaam ina barabara zinachongwa kwa mwaka zaidi ya mara tatu kwa gharama kubwa, lakini barabara ikishachongwa inakaa kwa siku tatu hadi tano tu baada ya hapo inakuwa mahandaki.

Kumbuka kila barabara ikichongwa ni pesa nyingi inatumika. Uchongaji wa barabara hizi kila mwaka zaidi ya mara tatu unajenga taswira mbaya na kusababisha sisi raia kujiuliza, kweli hawa wanaotoa tenda wataweza kupendekeza hizi barabara ziwekewe lami? Na zikiwekewa lami mirija ya watu haitakufa?

Tunajiuliza pia kuwa iweje barabara za TANROADS kwa mkoa wa Dar ambao unatengeneza uchumi wa Tanzania ziwe mbovu kiasi hichi?

Tunaomba Mheshimiwa rais hili liangaliwe kwa macho ya ziada ili kuondoa barabara mbovu za TANROADS katika mkoa wa Dar es Salaam kwa maana ni hasara kubwa kwa nchi na inasababisha ugumu wa maisha kwa wakazi wa DSM, watu wanachelewa kufika makazini na matengenezo ya magari yanakuwa juu sana.

Wilaya ya Ubungo especially jimbo la Kibamba ndo lianongoza kwa barabara mbovu katika mkoa wa DSM. Napata shida sana kuona kuwa hili ndo jimbo ambalo liko usoni mwa jiji lakini barabara zake za TANROADS ni mbovu kabisa.
 
kuna mchepuko umejengwa kuanzia kituo kikuu cha Polisi GOGONI kwenda hadi kwa Komba, pongezi kwa hilo, lakini wameacha barabara inayo tumiwa na wananchi wengi sana kwa shughuli za kibiashara, barabara inayo elekea hondogo/shuleni na sehemu za kilimo cha umwagiliaji, pitisheni lami eneo hilo ni muhimu sana.

TARURA wanapaswa wahakikishe kero hiyo wanai tatua kwani Rais alisha toa fedha, waache janja janja!
 
Wana Dar es Salaam tuna changamoto nyingi sana. Lakini ya barabara imekithiri sana. Tunaomba ziara Dar es Salaam tukueleze shida zetu. Dar es Salaam ina barabara zinachongwa kwa mwaka zaidi ya mara tatu kwa gharama kubwa, lakini barabara ikishachongwa inakaa kwa siku tatu hadi tano tu baada ya hapo inakuwa mahandaki.

Kumbuka kila barabara ikichongwa ni pesa nyingi inatumika. Uchongaji wa barabara hizi kila mwaka zaidi ya mara tatu unajenga taswira mbaya na kusababisha sisi raia kujiuliza, kweli hawa wanaotoa tenda wataweza kupendekeza hizi barabara ziwekewe lami? Na zikiwekewa lami mirija ya watu haitakufa?

Tunajiuliza pia kuwa iweje barabara za TANROADS kwa mkoa wa Dar ambao unatengeneza uchumi wa Tanzania ziwe mbovu kiasi hichi?

Tunaomba Mheshimiwa rais hili liangaliwe kwa macho ya ziada ili kuondoa barabara mbovu za TANROADS katika mkoa wa Dar es Salaam kwa maana ni hasara kubwa kwa nchi na inasababisha ugumu wa maisha kwa wakazi wa DSM, watu wanachelewa kufika makazini na matengenezo ya magari yanakuwa juu sana.

Wilaya ya Ubungo especially jimbo la Kibamba ndo lianongoza kwa barabara mbovu katika mkoa wa DSM. Napata shida sana kuona kuwa hili ndo jimbo ambalo liko usoni mwa jiji lakini barabara zake za TANROADS ni mbovu kabisa.
Wasaidiz wamsaidie mama,kama ni ziara atakuja2 akipata muda,hata huku shy & kahama tuna muitaji aje atupe hai na azindue miradi na tumueleze changamoto za mkoa.
 
Ilala,jimbo la ukonga maeneo ya mvuti,aje aone uozo uliopo barabara ya mvuti mpaka gereza la mvuti dondwe.mama'! nchi inapigwa kila kukicha kwa kujifanya kuichonga ili wapige pibha za kujifichia ,mvua ikinyesha hakuna kutoka. Watoto hawaendi shule,wajawazito shauri yao,watumishi watajua wenyewe.huku hakuna mtu wa kupeleka gari ya abiria kwenye barabara ya"makumbusho".
 
Wawakilishi wenu walitakiwa hayo mambo wayawakilishe, wapewe majibu na warudishe majibu kwenu wananchi.

Rais hawezi kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya mambo kama haya.
 
Ndo maana tumeamua kuandika wenyewe kwa maana mama anasoma humu. Wawakilishi wetu wameenda kufanya yao na si kuwawakilisha wananchi.
 
Hasa hasa barabara ya Mbezi hadi Mpigi majohe na ile ya Mbezi hadi Darajani
Unajiuliza maswali mengi hadi hupati jibu. Inakuwaje mabasi yaende madale ndo yaende bunju then kaskazini, lakini kumbe yangeweza kupita shortcut ya mbezi high school then mpigi magoe to bunju. Sijui aliyeweka plan ya madale aliwaza nini.
 
YAANI ukonga mi balaa. Banana KUPUNGUZA matembele ya KWANZA mpaka kitunda SHULE yelewiiiiiiii maweeeeee. Kivule SHULE, ccm, frame KUMI Hadi msongola Mmmmmmm. Yote KUMI Kuna ukonga BARABARA ya zamani MAARUFU BARABARA ya NGOMBE au BARABARA ya Zambia, nako majanga.
 
Back
Top Bottom