Rais Samia tunaomba usimamie ujenzi wa nyumba imara na sio upakaji rangi nzuri kwenye genge

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,494
41,002
Mh. Rais Samia, kwa muda mfupi ametenda mema mazuri. Yanaonekana ni mazuri ya pekee kutokana na utawala uliotangulia kuwa mbaya sana.

Kama umeshinda siku mbili bila kula, siku ya tatu ukapewa uji usio hata na sukari, utauona mtamu sana, siyo kwa sababu ni mtamu bali ni kutokana na hali uliyo nayo kabla.

Awamu ya tano iliua mfumo mzima wa utawala wa mihimili mitatu. Baada kufanikiwa kufanya hilo, uliweza kuwaonea watu na kuwapendelea watu kwa namna yoyote ambayo mtawala alitaka. Hakuna aliye hoji wala kuzuia.

Mama Samia amejaribu kurudisha yaliyostahili kuwa, lakini kwa sababu udikteta wa awamu ya tano uliyaondoa, sasa yanaonekana ni mapya na lulu.

Rais Samia kama analipenda Taifa hili, kama anawapenda watanzania, aongoze juhudi za kujenga nyumba imara na siyo kupaka rangi kwenye nyumba genge au banda chakavu. Hata atumie rangi nzuri namna gani, kupaka genge/banda, uzuri wa rangi hautaonekana.

Yote mabaya anayoyasahihisha sasa, kwa kiasi kikubwa yalifanywa na mtangulizi wake kwa kutumia udhaifu wa mifumo ya kiutawala ya Taifa letu.

Mh. Samia asiishie kufungulia bank accounts ambazo zilifungiwa na utawala mbaya wa awamu iliyopita, bali aweke mfumo utakaozuia mtawala yeyote kufungia account za watu kwa uonevu na ubabe. Hakuna njia ya kuhakikisha hilo isipokuwa KATIBA NA SHERIA NZURI

Mh. Samia asiishie tu kuwaachia waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi na utawala wa awamu ya tano, bali asimamie ujengaji wa mifumo itakayozuia kabisa mtawala kuwaonea watu kwa kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi. Jibu ni KATIBA NA SHERIA NZURI.

Mh. Samia asiishie tu kumkamata Sabaya na kumfikisha mahakamani kwa kutumia cheo chake kufanya ujambazi, bali ajihusishe zaidi katika kujenga mfumo utakaozuia kabisa mtawala kuwateua majambazi waende wakawatese raia kama ulivyofanya utawala wa awamu ya tano. Suluhisho ni KATIBA NA SHERIA NZURI.

Rais Samia asiishie tu kuwazuia watu wasiojulikana kuteka, kutesa, kuua na kupoteza watu wanaomkosoa Rais na serikali bali atengeneze mfumo unaomzuia kabisa kiongozi wa nchi kutengeneze magenge ya wahalifu ili kuwadhulumu mahasimu wake wa kisiasa, kama ilivyokuwa kwenye utawala wa awamu ya tano.

Mh. Rais Samia, wanaodai ubadilishaji wa katiba na sheria, siyo maadui zako bali ni watu wema kwako na kwa Taifa, maana wanakukumbusha unachostahili kufanya ili jitihada zako, manufaa yake yasiishie tu leo bali yaishi na Taifa wakati wote.

USIPAKE RANGI NZURI KWENYE GENGE BALI JENGA NYUMBA IMARA, KISHA PAKA RANGI NZURI.
 
Mh. Samia asiishie kufungulia bank accounts ambazo zilifungiwa na utawala mbaya wa awamu iliyopita, bali aweke mfumo utakaozuia mtawala yeyote kufungia account za watu kwa uonevu na ubabe. Hakuna njia ya kuhakikisha hilo isipokuwa KATIBA NA SHERIA NZURI
Mkuu siyo kwamba hafahamu hili. Analifahamu sana. Lkn tatizo ni ulafi wa madaraka wake mwenyewe na walionzunguka.

Wana hofu ya kwamba katiba mpya itapoka uwezo wa ccm kusalia mamlakani.
 
Huu Ni utumbo. Mama anawashauri wengi wenye akili, na sio nyie majuha ambao hamjui lolote
Wewe unaamini kuna washauri wenye akili timamu na walio wakweli wa nafsi zao huko Serikalini? Tafakari:

Hapo mwanzo:

CCM haiwezi kushinda uchaguzi huru. Katibu mpya ni muhimu kwa ustawi wa Taifa letu - Polepole

Katiba mpya ndiyo itakayojenga mustakabli wa Taifa - Kabudi

Tanzania inahitaji katiba mpya, hii ya sasa ilikuwa ya chama kimoja - Bashiru

Siku za karibuni

Wananchi wanataka maji, wanataka matibabu, wanataka umeme, siyo katiba mpya - Polepole

Katiba yetu hii ya sasa ni nzuri na imara, imetuvusha hata wakati wa matatizo - Kabudi

Haki za wananchi ni muhimu kuliko Katiba - Bashiru

Hivi watu wanafiki kama hawa unaweza kusimama na kusema wanaweza kumshauri kiongozi yeyote?

Ndani ya CCM na serikali, kuna watu wanafiki wengi sana. Rais Samia akitaka kujua utawala wake unaonekana vipi asikilize maoni ya watu nje ya CCM na nje ya Serikali yake. Kinyume cha hapo ataambiwa ambayo wanafiki wanaamini anataka kuyasikia.
 
Nilichokiona kwa mama, ni kama hana maamuzi kama rais, kwani urais wake ni wa kurithi. Lile genge la jamaa bado linamtisha kufanya kilicho nje ya faida ya ccm. Ukiwatazama ccm vizuri, ni watu wanaichukulia katiba mpya kama nyaraka ya uchaguzi, na wanaogopa ikienda kama inavyotakiwa lazima watapoteza dola, kwani hawana tena uwezo wakushindana.
 
Back
Top Bottom