Rais Samia tunaomba unapolihutubia Bunge ueleze sera zako za Awamu ya Sita, ya Awamu ya Tano yashapita

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Rais Mama Samia Suluhu kwanza nikupongeze kwa kuomba kulihutubia Bunge na Mh Spika akakubalia.

Ombi langu ni kuwa sekta zote zinaosubiri kwa hamu hotuba yako hasa wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Sekta Binafsi ni sehemu muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote kwa sasa duniani hata China.

Pia nigeomba uzungumzie suala la kutapakaa kwa wanaojiita wamachinga mitaani hasa katika pavement za wapita kwa miguu (pedestrians). Watoto wetu, wazee kwa vijana kutokana na zahma hizo wanapita barabarani kabisa,matokeo yake wanagongwa na magari,bodaboda na bajaji.

Hawa machinga wawekewe sehemu za kufanyia biashara.Mfano nchi ya Tunisia wamewaekea kila kitongoji sehemu ya machinga. Sie tunaweza kuiga kwa wataalam wetu mikoani kuwaandalia maeneo maalum. Mfano Dar ilala kuwe na sehemu kubwa ambapo wote watakuwepo, utapata kila kitu hapo.

Hayo ni maoni yangu kutokana na kutembelea nchi mbalimbali. Kifupi masoko haya yana wauzaji wa vyakula,nguo n.k mpaka vipuri vya magari utapata huko lakini mitaa yote nadhifu na salama.
 
Kwavhiyo atakachozungumzia ni kutengeneza madege na ma submarine na kwenda kwenye sayari au atasema kipi tofauti na mabarabara maji na umeme afya elimu na skills ?
 
nyie umbwa mnakera sana kwakweli.

IMG_0324.jpg
 
Mleta mada nenda kasome ILANI YA CCM 2020-2025, machache sana yatakuwa nje ya Ilani ya chama
 
hili wala si la kumuomba. siku pekee ya Rais kianika sera za serikali yake ni siku ya kukanyaga bungeni. sema bunge lenyewe la sasa limejaa vyura.
 
Back
Top Bottom