Rais Samia, tunaomba msaada wa Kivuko Kigamboni

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
67
248
Mama Samia tunaomba Huruma yako Kigamboni:

Kwanza naanza kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano WA Tanzania..., Natumai umeitikia "Kazi iendelee.."

Pili nakupa pole kwa kazi ngumu ya kuongoza Tanzania, nchi yenye Mazonge ya kila rangi kila uchao,

Na Tatu nakupa pongezi kwa siku hii ya leo, tarehe 8 March, maalum kwa ajili ya wanawake Duniani, maalum kwa ajili yako wewe ambaye unaangaliwa leo kama kielelezo cha siku hii kwa wanawake wengine, Happy women's Day to you, hakika mnaweza.

Sasa nirudi kwenye hoja wangu ya msingi, mheshimiwa natamani ningekuwa Bungeni pengine Bunge lote kama sio Tanzania nzima ingesimama kwa muda kunisikiliza nasema nini kuhusu Kigamboni yangu na watu wake, au pengine ningekuwa na HOJA binafsi kuliomba bunge liijadili hali ya Kigamboni na kuiundia Tume au kutolea maelekezo muhimu.

Lakini si tatizo, huu ukurasa wangu wa Facebook inatosha kuwa microphone yangu kuniwezesha kusema na kusikia na masikini yako sikivu.

Kwanza nianze kuwasilisha Nasikitika yetu wana wa Kigamboni, hatufurahishwi na hali ya mambo inavyokwenda. Tunajisikia kutengwa na kunyanyasika na kutojaliwa au kupuuzwa ndani ya Jamhuri yetu huru.

Kigamboni tunaishi kama tupo nchi ya jirani ambayo kwa sasa huwezi kuingia Tanzania (Dar es Salaam) isipokuwa kwanza ukipie VISA ya kutoka na kuingia. Ni nazungumzia Tozo za daraja, haziko sawa kwa namna zote, kikatiba na kisheria , kiutu, kijamii na hata kidini, Dini zote nizijuazo, hata nisizoziamini, hakuna inayoruhusu UBAGUZI.

KWA Hili sisemi mengi kwa sababu linajulikana, ninaomba CHONDE mimi raia uniachie dhima yangu kuu moja tu ya kulipa KODI, DHIMA ya ujenzi wa miindombinu na huduma zingine za kijamii hiyo ni kazi ya msingi ya serikali unayoisimamia wewe, na ndio mantiki ya kukukabidhi fedha zote za nchi, silaha na majeshi yote ya ulinzi kuwa chini yako wewe ambaye unatajwa na kuitwa Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Ulinzi hata kama hujui kushika hata manati.

Kwa sababu ya Fani yangu ya Sheria, ningeweza kunukuu na vifungu vya sheria na katiba vyenye maelekezo hayo, lakini nahofia kulifanya andiko langu lisikuchoshe.

Kigamboni hatuyafurahii maisha kwa sababu nyingi, lakini hili la usafiri ndilo kubwa hasa.

Kwa hali ilivyo Sasa Kigamboni binafsi ninathubutu kuita ni JANGA, yaani ni zaidi ya hali isiyo kuwa ya kawaida. Kila aliyepo Kigamboni anatumia na kulia machozi yake kimya kimya. Lakini licha ya kwamba tunaoumia no wote, lakini wanawake, watoto na wazee ndio wanaoumia zaidi, ni nazungumzia MSONGAMANO wa kihistoria katika vivuko vyetu.

Kwa sasa pale Ferry tuna vivuko vitatu, lakini vinavyofanya kazi ni viwili tu, tena na hivyo viwili wakati wowote utasikia habari tofauti kwa sababu kile kidogo kinaendeshwa kwa kiwashwa Injini Tatu badala ya Nne kama inavyotakiwa, sijui sababu ninini!

Hali hii ya kutumia Injini Tatu imekifanya kivuko hiki kuwa na mwendo mdogo sana isivyo kawaida unaokadirikwa kwa wastani wa dakika arobain na tano mpaka saa nzima kila kinapoondoka upande wa pili ba kurudi.

Mama yetu, Rais wetu mpendwa, Kwa idadi ya watumiaji wa vivuko vya ferry kwa sasa ni kubwa sana tofauti na ilivyokadiriwa, licha ya wakaazi wa Kigamboni kuongezeka lakini pia abiria wengi wa maeneo ya Mbagala, kongowe na Mwandege nao wanatumia vivuko vya Kigamboni wakikwepa foleni katika barabara ya Kilwa ambayo husababishwa na ujenzi unaendelea wa Flyover ya eneo la mkutano ya barabara ya Kilwa na Mandela.

Mama yetu na Rais wetu msikivu, NINAKUAPIA KWA JINA la MUNGU mwenye Dunia yake aliyekuwa madaraka hayo, kwa sasa utaratibu WA abiria kupanda vivuko vya Kigamboni hautofautiani na ule wa Sigara kukaa au kupangwa kwenye pakiti lake, hali ambayo kiusalama na kiafya si SAWA.

HAKI hii ya MSONGAMANO, kubanana na kushonana kwenye kivuko kimoja si tu hatari kiusalama na kiafya, lakini pia kijinsia na kidini dada zetu na mama zetu ambao ni wanawake wenzio wanafedheheka sana kwa sababu faragha ya miili Yao haipo tena kutokana na kujikuta wakilazimika kugusana au kuguswa, kuminyana maungo Yao na wanaume ambao si halali Yao,naamini unanielewa hapo mama yangu Msikivu.

Sasa kama nilivyodokeza awali, hali ya Kigamboni kwa sasa binafsi ninaichukulia ni JANGA na ninaomba wewe binafsi na serikali yako muichukulie kwa uzito Huohuo.

Na kwa kuwa MAJANGA huchukuliwa kwa uzito wa peke yake na udharura, tunaomba hili la Usafiri Kigamboni lipewe hadhi hiyo na hatua za haraka zichukuliwe kutunusuru na hali hii.

Nini kifanyike?
Kwa sasa hali ya Kigamboni kama nilivyoeleza, ni JANGA, na ukweli wenyewe ndio huo,hatua za kidharura zinapaswa kuchukuliwa kuinusuru Kigamboni na MAJANGA zaidi yanayoweza kutokea. Yafuatayo yafanyike kumrudisha furaha ya maisha kwa wana Kigamboni:

1. Kuongeza Kivuko
Kwa idadi kubwa ywa wanaKigamboni kwa sasa ambao ni wafanyakazi wa serikali na mashirika na makampuni binafsi na Wanafunzi na wafanyabiashara ambao wote kwa ujumla wao wanapaswa kuwahi mapema maofisini vivuko viwili haviwatoshi.

Hata kikirudi kile kinachosemwa kipo matengenezo bado hakitofaa kuondoka MSONGAMANO uliopo Sasa. Dawa pekee kwa hali hii ni kupatikana kwa kivuko cha nne tena kikubwa.

2. Lakini zaidi ya kupatikana kwa vivuko hivyo vinne, msimamizi wa vivuko hivi TEMESA anapaswa kumulikwa na kuangalia upya uwezo na ufanisi wake. Kila leo hali ya ubovu wa vivuko huwa kama ni jambo la kustukiza kwao kama vile wamekabidhiwa kazi hiyo Jana yake.

Injini za vivuko hivyo inahisiwa hazifanyiwi huduma na marekebisho madogo mpaka pale itakapokuwa na tatizo kubwa la kulazimisha kuondosha chombo husika baharini.

3. Vivuko vya dharura
Kwa ilivyo kwa sasa huduma ya Vyombo vya dharura inahitajika kuokoa hali tuliyo nayo. Kuna wakati siku za nyuma tulitumia kivuko cha Jeshi, nadhani kwa sasa tunahitaji kivuko kile kuliko wakati mwingine wowote, na kwa udharura tulinao hilo linapaswa kufanyika kazi kwa haraka zaidi.

Kwa maaana ya dharura, hata ilibidi kukodi au kuazima kivuko kutoka nchi ya jirani hebu iwe hivyo, tupo katika dharura hali si salama!

Binafsi ni nafahamu kama taifa tunao mfuko wa dharura, Sasa kwa hali ilivyo Kigamboni kwa sasa ndo wakati muafaka fedha hiyo itumike.

4. Vivuko binafsi
Nashawishika kwa sasa kuliomba serikali yako iruhusu zile boti ndogo za wavuvi zitumike kuvusha watu chini ya usimamizi maalum wa serikali wenye kuhakikisha usalama wetu,hatuna namna, hali ya mambo kote so shwari.

5. Kubinafsisha huduma ya ferry
Hii naomba nikukumbushe na bila shaka utakubaliana na mimi kwamba serikali haipo kwa ajili ya kufanya biashara, serikali hutoa huduma tu. Kwa maana hiyo sioni sababu kwa nini serikali iendelee kuishikilia huduma ya uvushaji abiria Kigamboni ilhali kwa mizania yote ilikwishashindwa miaka Mingi nyuma.

Kwa maana ya kuboresha huduma serikali inaweza kubinafsisha huduma hiyo kwa mwekezaji mwenye uwezo ambao binafsi ninaamini wapo wengi sana, au inaweza kuingia mkataba wa Ubia na mwekezaji binafsi jambo ambalo ninaamini litaleta tija kwetu kama Kigamboni na taifa kwa ujumla.

Mbona Zanzibar tunakwenda kwa kutumia huduma za kampuni binafsi za Meli, mbona ATCL(shirika nyeti kabisa) ilibinafsishwa, mbona mabasi ya mwendo kasi yanaendeshwa kwa Ubia, why not Ferry ya Kigamboni?

Ninaimani sana na wewe Mama yetu, Rais wetu, Jina lako unaitwa 'SAMIA' , katika kiarabu maana yake ni MSIKIVU, au mwenye kusikia, sifa katika sifa za Mwenyezi Mungu hizo, ninaamini utalitendea haki Jina lako kwa faida ya Wana Kigamboni.

Haitoleta maana tukikubali kusubiri litokee tatizo, madhara yatupate halafu tuishie kuunda TUME kuchunguza, au kuwajibisha a kwa kufukuzana kazi na kupelekana mahakamani, haitobadili hali ya mambo.

Andiko hili LITABAKI kuwa shahidi kama hatotochukua hatua leo za haraka.

Tamko lako moja tu mama yetu SAMIA linatosha kubadili hali ya mambo Kigamboni.

Ninaomba kuwasilisha

M. Majaliwa.

_20220308_091615.JPG
 
Tupunguze kelele, kile kivuko kidogo kiko kwenye utengenezaji pale kwa songoro. Muda ukikamilika kitarejea kutoa Huduma.

Hizo mbili tuvimilie tuu kwa sasa huku tukitumia daraja. Kama tumeweza vumilia ccm madarakani zaidi ya 40 years hatuwezi shindwa vumilia kipindi kifupi cha kivuko kutengenezwa
 
Kama ilishindikana kujenga daraja kubwa hapo feri basi ni bora wangejenga hata daraja simple la kuvuka abiria peke yake halafu magari yavuke kwa pantoni.
Binafsi ninaamini haishindikani kujengwa daraja kubwa eti kwa kisingizio cha meli kushindwa kupita, ninachoamini kupitia hio mipantoni yao kuna pesa mingi sana inapigwa hapo, hivyo lazima vipingamizi vya ujenzi wa daraja viwepo ili wajanja wachache waendelee na upigaji.
Kwa kasi ya ukuaji wa kigamboni najenga picha laiti ferry kungekua na daraja halafu barabara kuu za kigamboni zikapata mradi wa mabasi ya mwendo kasi, hakika kigamboni ingenoga sana.
 
Wapunguze bei pale Darajani sio mbaya ikiwa 500/=
 
Umeshajiuliza wakijenga daraja meli zitapitia wapi maana kama ni daraja basi lie refu kupitiliza meli zipite chini kumbuka pale ni njia ya kupitia meli zinazoingia na kutoka bandarini
 
Tupunguze kelele, kile kivuko kidogo kiko kwenye utengenezaji pale kwa songoro. Muda ukikamilika kitarejea kutoa Huduma.

Hizo mbili tuvimilie tuu kwa sasa huku tukitumia daraja. Kama tumeweza vumilia ccm madarakani zaidi ya 40 years hatuwezi shindwa vumilia kipindi kifupi cha kivuko kutengenezwa
Mkuu sijui Kama umesoma bandiko lote.Kuna mahali mtoa hoja kaeleza kuwa hata kikija hicho kilichoko matengenezo bado hali haitatengemaa.Kwa ujumla vitakuwa vitatu wakati yeye kapendekeza walau viwe vinne.
 
Umeshajiuliza wakijenga daraja meli zitapitia wapi maana kama ni daraja basi lie refu kupitiliza meli zipite chini kumbuka pale ni njia ya kupitia meli zinazoingia na kutoka bandarini
Linaweza kujengwa daraja refu meli zikapita chini au daraja linaloweza kufunguka kuruhusu meli ingawa hii itasababisha foleni.
1646723040994.png
1646723040994.png
 
Hapa serikali inatakiwa iwalipe nssf hela yao iliobaki kwa kutumia kodi zetu na watu wapite bure pale darajani.
Hili ni suluhisho la kudumu.Mh rais SSH na serikali yake hata wakilipa kwa awamu watakuwa wamefanya Jambo la kukumbukwa.
 
Mama Samia tunaomba Huruma yako Kigamboni:

Kwanza naanza kukusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano WA Tanzania..., Natumai umeitikia "Kazi iendelee.."

Pili nakupa pole kwa kazi ngumu ya kuongoza Tanzania, nchi yenye Mazonge ya kila rangi kila uchao,

Na Tatu nakupa pongezi kwa siku hii ya leo, tarehe 8 March, maalum kwa ajili ya wanawake Duniani, maalum kwa ajili yako wewe ambaye unaangaliwa leo kama kielelezo cha siku hii kwa wanawake wengine, Happy women's Day to you, hakika mnaweza.

Sasa nirudi kwenye hoja wangu ya msingi, mheshimiwa natamani ningekuwa Bungeni pengine Bunge lote kama sio Tanzania nzima ingesimama kwa muda kunisikiliza nasema nini kuhusu Kigamboni yangu na watu wake, au pengine ningekuwa na HOJA binafsi kuliomba bunge liijadili hali ya Kigamboni na kuiundia Tume au kutolea maelekezo muhimu.

Lakini si tatizo, huu ukurasa wangu wa Facebook inatosha kuwa microphone yangu kuniwezesha kusema na kusikia na masikini yako sikivu.

Kwanza nianze kuwasilisha Nasikitika yetu wana wa Kigamboni, hatufurahishwi na hali ya mambo inavyokwenda. Tunajisikia kutengwa na kunyanyasika na kutojaliwa au kupuuzwa ndani ya Jamhuri yetu huru.

Kigamboni tunaishi kama tupo nchi ya jirani ambayo kwa sasa huwezi kuingia Tanzania (Dar es Salaam) isipokuwa kwanza ukipie VISA ya kutoka na kuingia. Ni nazungumzia Tozo za daraja, haziko sawa kwa namna zote, kikatiba na kisheria , kiutu, kijamii na hata kidini, Dini zote nizijuazo, hata nisizoziamini, hakuna inayoruhusu UBAGUZI.

KWA Hili sisemi mengi kwa sababu linajulikana, ninaomba CHONDE mimi raia uniachie dhima yangu kuu moja tu ya kulipa KODI, DHIMA ya ujenzi wa miindombinu na huduma zingine za kijamii hiyo ni kazi ya msingi ya serikali unayoisimamia wewe, na ndio mantiki ya kukukabidhi fedha zote za nchi, silaha na majeshi yote ya ulinzi kuwa chini yako wewe ambaye unatajwa na kuitwa Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Ulinzi hata kama hujui kushika hata manati.

Kwa sababu ya Fani yangu ya Sheria, ningeweza kunukuu na vifungu vya sheria na katiba vyenye maelekezo hayo, lakini nahofia kulifanya andiko langu lisikuchoshe.

Kigamboni hatuyafurahii maisha kwa sababu nyingi, lakini hili la usafiri ndilo kubwa hasa.

Kwa hali ilivyo Sasa Kigamboni binafsi ninathubutu kuita ni JANGA, yaani ni zaidi ya hali isiyo kuwa ya kawaida. Kila aliyepo Kigamboni anatumia na kulia machozi yake kimya kimya. Lakini licha ya kwamba tunaoumia no wote, lakini wanawake, watoto na wazee ndio wanaoumia zaidi, ni nazungumzia MSONGAMANO wa kihistoria katika vivuko vyetu.

Kwa sasa pale Ferry tuna vivuko vitatu, lakini vinavyofanya kazi ni viwili tu, tena na hivyo viwili wakati wowote utasikia habari tofauti kwa sababu kile kidogo kinaendeshwa kwa kiwashwa Injini Tatu badala ya Nne kama inavyotakiwa, sijui sababu ninini!

Hali hii ya kutumia Injini Tatu imekifanya kivuko hiki kuwa na mwendo mdogo sana isivyo kawaida unaokadirikwa kwa wastani wa dakika arobain na tano mpaka saa nzima kila kinapoondoka upande wa pili ba kurudi.

Mama yetu, Rais wetu mpendwa, Kwa idadi ya watumiaji wa vivuko vya ferry kwa sasa ni kubwa sana tofauti na ilivyokadiriwa, licha ya wakaazi wa Kigamboni kuongezeka lakini pia abiria wengi wa maeneo ya Mbagala, kongowe na Mwandege nao wanatumia vivuko vya Kigamboni wakikwepa foleni katika barabara ya Kilwa ambayo husababishwa na ujenzi unaendelea wa Flyover ya eneo la mkutano ya barabara ya Kilwa na Mandela.

Mama yetu na Rais wetu msikivu, NINAKUAPIA KWA JINA la MUNGU mwenye Dunia yake aliyekuwa madaraka hayo, kwa sasa utaratibu WA abiria kupanda vivuko vya Kigamboni hautofautiani na ule wa Sigara kukaa au kupangwa kwenye pakiti lake, hali ambayo kiusalama na kiafya si SAWA.

HAKI hii ya MSONGAMANO, kubanana na kushonana kwenye kivuko kimoja si tu hatari kiusalama na kiafya, lakini pia kijinsia na kidini dada zetu na mama zetu ambao ni wanawake wenzio wanafedheheka sana kwa sababu faragha ya miili Yao haipo tena kutokana na kujikuta wakilazimika kugusana au kuguswa, kuminyana maungo Yao na wanaume ambao si halali Yao,naamini unanielewa hapo mama yangu Msikivu.

Sasa kama nilivyodokeza awali, hali ya Kigamboni kwa sasa binafsi ninaichukulia ni JANGA na ninaomba wewe binafsi na serikali yako muichukulie kwa uzito Huohuo.

Na kwa kuwa MAJANGA huchukuliwa kwa uzito wa peke yake na udharura, tunaomba hili la Usafiri Kigamboni lipewe hadhi hiyo na hatua za haraka zichukuliwe kutunusuru na hali hii.

Nini kifanyike?
Kwa sasa hali ya Kigamboni kama nilivyoeleza, ni JANGA, na ukweli wenyewe ndio huo,hatua za kidharura zinapaswa kuchukuliwa kuinusuru Kigamboni na MAJANGA zaidi yanayoweza kutokea. Yafuatayo yafanyike kumrudisha furaha ya maisha kwa wana Kigamboni:

1. Kuongeza Kivuko
Kwa idadi kubwa ywa wanaKigamboni kwa sasa ambao ni wafanyakazi wa serikali na mashirika na makampuni binafsi na Wanafunzi na wafanyabiashara ambao wote kwa ujumla wao wanapaswa kuwahi mapema maofisini vivuko viwili haviwatoshi.

Hata kikirudi kile kinachosemwa kipo matengenezo bado hakitofaa kuondoka MSONGAMANO uliopo Sasa. Dawa pekee kwa hali hii ni kupatikana kwa kivuko cha nne tena kikubwa.

2. Lakini zaidi ya kupatikana kwa vivuko hivyo vinne, msimamizi wa vivuko hivi TEMESA anapaswa kumulikwa na kuangalia upya uwezo na ufanisi wake. Kila leo hali ya ubovu wa vivuko huwa kama ni jambo la kustukiza kwao kama vile wamekabidhiwa kazi hiyo Jana yake.

Injini za vivuko hivyo inahisiwa hazifanyiwi huduma na marekebisho madogo mpaka pale itakapokuwa na tatizo kubwa la kulazimisha kuondosha chombo husika baharini.

3. Vivuko vya dharura
Kwa ilivyo kwa sasa huduma ya Vyombo vya dharura inahitajika kuokoa hali tuliyo nayo. Kuna wakati siku za nyuma tulitumia kivuko cha Jeshi, nadhani kwa sasa tunahitaji kivuko kile kuliko wakati mwingine wowote, na kwa udharura tulinao hilo linapaswa kufanyika kazi kwa haraka zaidi.

Kwa maaana ya dharura, hata ilibidi kukodi au kuazima kivuko kutoka nchi ya jirani hebu iwe hivyo, tupo katika dharura hali si salama!

Binafsi ni nafahamu kama taifa tunao mfuko wa dharura, Sasa kwa hali ilivyo Kigamboni kwa sasa ndo wakati muafaka fedha hiyo itumike.

4. Vivuko binafsi
Nashawishika kwa sasa kuliomba serikali yako iruhusu zile boti ndogo za wavuvi zitumike kuvusha watu chini ya usimamizi maalum wa serikali wenye kuhakikisha usalama wetu,hatuna namna, hali ya mambo kote so shwari.

5. Kubinafsisha huduma ya ferry
Hii naomba nikukumbushe na bila shaka utakubaliana na mimi kwamba serikali haipo kwa ajili ya kufanya biashara, serikali hutoa huduma tu. Kwa maana hiyo sioni sababu kwa nini serikali iendelee kuishikilia huduma ya uvushaji abiria Kigamboni ilhali kwa mizania yote ilikwishashindwa miaka Mingi nyuma.

Kwa maana ya kuboresha huduma serikali inaweza kubinafsisha huduma hiyo kwa mwekezaji mwenye uwezo ambao binafsi ninaamini wapo wengi sana, au inaweza kuingia mkataba wa Ubia na mwekezaji binafsi jambo ambalo ninaamini litaleta tija kwetu kama Kigamboni na taifa kwa ujumla.

Mbona Zanzibar tunakwenda kwa kutumia huduma za kampuni binafsi za Meli, mbona ATCL(shirika nyeti kabisa) ilibinafsishwa, mbona mabasi ya mwendo kasi yanaendeshwa kwa Ubia, why not Ferry ya Kigamboni?

Ninaimani sana na wewe Mama yetu, Rais wetu, Jina lako unaitwa 'SAMIA' , katika kiarabu maana yake ni MSIKIVU, au mwenye kusikia, sifa katika sifa za Mwenyezi Mungu hizo, ninaamini utalitendea haki Jina lako kwa faida ya Wana Kigamboni.

Haitoleta maana tukikubali kusubiri litokee tatizo, madhara yatupate halafu tuishie kuunda TUME kuchunguza, au kuwajibisha a kwa kufukuzana kazi na kupelekana mahakamani, haitobadili hali ya mambo.

Andiko hili LITABAKI kuwa shahidi kama hatotochukua hatua leo za haraka.

Tamko lako moja tu mama yetu SAMIA linatosha kubadili hali ya mambo Kigamboni.

Ninaomba kuwasilisha

M. Majaliwa.

View attachment 2143003
Mtabaki kumpongeza rais na kumsujudia kila siku hadi mwisho, huku mkitetea chama kibovu kilichopo pamoja na katiba mbovu.
 
aisee watu wa kigamboni mnalalamika sana.....subirini kivuko kipone au piteni darajani...simple tu.....yaani serikali iwekeze tena hela kujenga daraja au kununua vivuko vipya badala ya kupeleka sehemu nyingine kwa wenye uhitaji na hawalalamiki kama nyie..what is so special mlichonacho...
 
Wampe bakhresa hapo na Kilimanjaro zake .magogoni dakika 2.
Kigamboni dakika 2.
HAKUNA foleni chapu kwa haraka.
Tena atapiga hela sana
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom