Rais Samia: Tunaandaa mradi wa kuomba hela za kujenga stendi. Hayati Magufuli asingethubutu kusema kitu cha kujitweza utu wetu namna hiyo... never!

Hivi kuna raisi WA tz aliyekopa hela nyingi Kwa muda mfupi kama Rais Magufuli?

Pitia hotuba ya Dr mpango 2019 kuhusu deni la Taifa akituambia kuwa linavumilika Kwa sababu inawekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Mpaka sasa Magufuli anashikiria rekodi ya kukopa pesa nyingi kuliko raisi yoyote Tanzania katika kipindi kifupi.
Angalia mikopo serikali ya Magufuli iliyokopa world Bank.

All News

List of all news about the World Bank’s development work in Tanzania, including press releases, loans and credits, speeches, blog posts, and more.
www.worldbank.org

Standard gauge ela imekopwa Kwa mabeberu Sweden na Norway kupitia standard chartered Bank.
Tanzania signs $1.46 billion loan for standard gauge railway construction

Mpaka mwaka 2020 deni la Taifa lilifika Zaid ya shilling trilioni 70 Sawa na 54% ya uchumi wetu.
Tanzania's debt surging, but government says it’s still sustainable | The East African

Wakati mtangulizi wake alikuwa deni la Taifa mwaka 2005 ni Dola bilioni 7 ndani ya miaka 10 deni la Taifa likaongezeka mpaka dola bilioni 18,2015 yaani ongezeko la Dola bilioni 11.

Wakati raisi Magufuli deni la Taifa lilifika Dola bilioni 30.63, ongezeko la bilioni 12 ndani ya miaka mitano Tu.
countryeconomy.com

Tanzania National Debt 2015


countryeconomy.com

Tz ni nchi masikini sana na tupo ndani ya nchi 33 masikini zaidi duniani Kwa kuzingatia GNI per capita, kutembeza bakuli hakuepukiki. Karibu miradi yote ya Magufuli imejengwa Kwa pesa za mkopo.
Alafu kwenye hotuba zake anatuambia kuwa ni fedha zetu za ndani.

Ni mahera yetu maana sisi ni matajiiiiriiii sana.
 
Kuna tetesi kuwa kuna systema JPM (R.I.P) alitengenezewa yakuangalia performance ya ukusanyaji mapato na utekelezaji wa miradi pamoja na transactions zake nchini at any time t.

Sina hakika kama system hiyo ipo active kama tetesi ni za kweli.
SASAHIVI WAMWIUA..WANATUMIA MANUALS
 
WanaCCM mmezoea unafiki na mnaona Mtu muwazi anawadhalilisha. Huyo u ayemsifia ndo kaua mashirika ya Umma Kwa mikopo kamdamizi, ndo kapaisha deni la Taifa kimyakimya Hadi nchi inanula madeni. Acheni unafiki.
Watanzania wengi ni wanafiki hasa wale wa lumumba
 
Huu ndio ukweli , jamaa alikuwa muongo ni balaa, ameicha nchi kwenye umaskini mkubwa, na Kama Ange kaa miaka kumi , vazi la Taifa lingekuwa ni kaniki
Na wana ccm wangeshangilia tu
 
Katika miaka kumi ya utawala wa awamu ya nne, kwa taarifa hiyo, deni liliongezeka kwa $ 11 bilioni. Swali la kujiuliza "hilo deni lilitumika kufanya nini?" Vivyo hivyo tujiulize deni, katika utawala wa awamu ya tano, liliongezeka maradufu ($12 bilioni), ndani ya miaka 5, limetumikaje? Je, awamu ya sita tunakopa kwa ajili ya nini?
Awamu ya 5 hawakufanya lolote zaidi ya majisifu tu .

Miradi mingi ilikuwa ni ya awamu ya mh Kikwete.
 
Achana na habari ya Magufuli, huyu 'Maza Mizinguo' ni mzinguaji kweli kweli!

Sasa anakwenda kuomba hela wapi?

Hata hivi vi-stendi tu navyo mpaka twende kupiga magoti? Miaka sitini baada ya kujitawala wenyewe? Sisi tunaweza kitu gani!
India/Pakistani kwa umri wa miaka chini ya 40, tayari walishakuwa na mabomu ya nuklia, sisi hata mashimo ya vyoo rais anakwenda kuomba hela!

Matokeo ya misimamo ya aina hii utaiona tu muda sio mrefu. Tumekuwa 'cheap' sana.

EeeeenHeeee, nakumbuka ile safari ya New York na jinsi tulivyoshushuliwa na wakubwa wa huko!

Waziri anakwenda kuweka kambi kabisa, lakini wapi, hakuambulia chochote. Sasa wanatutazama tu jinsi tunavyohangaika huku wakitupangia arobaini za kutuweka dole.

Hovyo kabisa!
Zenji ina meremeta
 
Huyo ni Chifu Matonya baada ya kutawazwa rasmi na wagogo na kupewa Uchifu. Ndege wanadai tunanunua kwa cash lakini wakati huo huo pesa ya kujenga stendi ya mabasi hatuna!!! Chifu Matonya inabidi atembeze bakuli lake!!! 😂😂

Akiwa anajibu kero za wananchi kuhusu stendi ya Arusha, Rais Samia Hassan leo amesema "kuna mradi tunaundaa wa kuomba hela hizi za stendi, tukipewa tuna nia maeneo mengi yawe na stendi za kisasa"

_______________________________________________

Magufuli anabiringika kaburini...

Tulikuwa tunaambiwa tembeeni kifua mbele, sisi ni matajiri... na kama ni kukopwa hela wanazileta wenyewe, hatuombi...

Sasa tutatembea vichwa chini mbele ya dunia...

Mpaka stendi tunaomba hela?

Hivi stendi ya Mbezi tulipata wapi hela ?

Nimesikitika kupita maelezo.... tunarudi kule kule kwenye kuishi kwa kuomba omba kwa enzi za bwana yule wa Bagamoyo...


 
Akiwa anajibu kero za wananchi kuhusu stendi ya Arusha, Rais Samia Hassan leo amesema "kuna mradi tunaundaa wa kuomba hela hizi za stendi, tukipewa tuna nia maeneo mengi yawe na stendi za kisasa"

_______________________________________________

Magufuli anabiringika kaburini...

Tulikuwa tunaambiwa tembeeni kifua mbele, sisi ni matajiri... na kama ni kukopwa hela wanazileta wenyewe, hatuombi...

Sasa tutatembea vichwa chini mbele ya dunia...

Mpaka stendi tunaomba hela?

Hivi stendi ya Mbezi tulipata wapi hela ?

Nimesikitika kupita maelezo.... tunarudi kule kule kwenye kuishi kwa kuomba omba kwa enzi za bwana yule wa Bagamoyo...



Hajatamka anakopa wapi? Inawezekana ikawa kwenye mabenki ya Ndani ya Tanzania. Siasa za kuwambia wananchi ukweli ni nzuri zaidi kuliko kuwambia uwongo na kuwachukulia wananchi kama hawana uwelewa wa mambo ya dunia.
 
Katika miaka kumi ya utawala wa awamu ya nne, kwa taarifa hiyo, deni liliongezeka kwa $ 11 bilioni. Swali la kujiuliza "hilo deni lilitumika kufanya nini?" Vivyo hivyo tujiulize deni, katika utawala wa awamu ya tano, liliongezeka maradufu ($12 bilioni), ndani ya miaka 5, limetumikaje? Je, awamu ya sita tunakopa kwa ajili ya nini?
Sina takwimu Ila barabara nyingi za lami na madaraja Ni kipindi Cha JK. Kuliko awamu zote kwa uwiano.
 
Dah!! Magufuli alitufanya tuwe Proud sana na nchi yetu.. sasa huyu ametugeuza kuwa ombaomba.. maisha yanaenda kasi sana..
 
Magufuli alikuwa MWONGO na akasababisha hata wa chini yake kuwa waongo. Na hata alipokufa tuliendelea kuambiwa uwongo na Majaliwa kuwa yuko ofsini anapitia mafaili.

Rais SSH endelea kuwa mkweli, penye hatuna pesa ongeza tozo au kakope, period
…..eti yupo ofisini anapitia mafaili…ahhaaaaaa!
 
Back
Top Bottom