Rais Samia: Tumewaondoa Wamachinga kwasababu Wageni Wanaogopa Kuja Tanzania

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,672
2,000


Mama asithamini sana Wageni akatusahau wazawa. Awe mzalendo na sio kila kitu anawaza kumfurahisha Mzungu tu

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app

Nilisema zamani kuwa kwasasa tunaongozwa na mwana NGOs. Kila mara utasikia tuandae mradi tuwaombe wenzetu watusaidie. Hutasikia tena tunaweza

Safi sana. CCM mbere kwa mbere
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,368
2,000
Ndio yale yale kama ya corona, hatuwezi kusema ipo kwa sababu wageni wataacha kuja....matatizo hayatatuliwi kwa kuyafunika chini ya kapeti View attachment 1999996
Mfano wako haulo relevant covid no pandemic hata ukija kwangu bila kuwa natadhari nakukataa, nakumbuka kipindupundu tulikuwa tulikkuwa tuna wanachukuwa tahadhari
 

BlackPanther

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
8,243
2,000


Mama asithamini sana Wageni akatusahau wazawa. Awe mzalendo na sio kila kitu anawaza kumfurahisha Mzungu tu

Sent from my TECNO P704a using JamiiForums mobile app

Nilisema zamani kuwa kwasasa tunaongozwa na mwana NGOs. Kila mara utasikia tuandae mradi tuwaombe wenzetu watusaidie. Hutasikia tena tunaweza


Acha ubaguzi kamanda....nchi zilizoendelea na hata za uchumi wa kawaida wanathamini wageni, wageni ni nuru, wageni wanawekeza na kuwapatia ajira wazawa....Mheshimiwa Rais, tenda haki sawa kwa wote bila kujali dini, ukabila na utaifa
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,265
2,000
Lini nchi hii haikuwahi kuwategemea wageni kwa MIKOPO NA MISAADA?!!!!

Wakati mwingine tunaweza kudhani "siasa za kizalendo" ndizo nguzo ya kutukomboa....kumbe ni "kelele nyingi tu zinazomchanganya mbwa".....

Dunia ilipofikia hatuwezi kujifungia na kujitenga na dunia......

Huko China balozi wetu mh.Komredi Mbelwa Kairuki anaturai tuongeze nguvu katika kilimo cha kahawa kwani masoko yamejaa tele......

SIEMPRE JMT
NCHI KWANZA
Kwani kutojifungia au kutojitenga na dunia ndiyo ufanye mambo yako kwa kuangalia wageni? Nyie mnachukulia simple tu lakini madhara yake ni makubwa sana kwenye fikra na utu wa mtu.

Ukianza kufanya kitu kwa kureference wageni, au kwa jirani, hufiki popote. Na kimtokacho mtu kinywani ndicho kimjazacho. Huyo mama hana tofauti na JK, wote ni dizaini za mtumikie kafiri upate mradi wako.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,817
2,000
Kwani kutojifungia au kutojitenga na dunia ndiyo ufanye mambo yako kwa kuangalia wageni? Nyie mnachukulia simple tu lakini madhara yake ni makubwa sana kwenye fikra na utu wa mtu.

Ukianza kufanya kitu kwa kureference wageni, au kwa jirani, hufiki popote. Na kimtokacho mtu kinywani ndicho kimjazacho. Huyo mama hana tofauti na JK, wote ni dizaini za mtumikie kafiri upate mradi wako.

FB_IMG_16332143456548674.jpg
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,337
2,000
Ikifika 2025 wazungu watakuja kumpigia kura.
Nafikiri hakujifunza kwa JK umaarufu wake ulivyoporomoka kwa Kasi ya umeme.
 

BlackPanther

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
8,243
2,000
Magufuli alifunga viwanda na migodi na kusababisha maelfu ya raia kupoteza ajira zao, unadhani alichokifanya ni sawa! Huyo ndiye mlikuwa mnasema rais wa wanyonge! Kama rais wa wanyonge asingefunga viwanda/migodi ili raia wake waendelee na ajira
 

KateMiddleton

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,875
2,000
Hivi Jangwani kama bonde kwa nini lisiachwe wazi hilo eneo hasa ukizingatia kuwa kuna mafuriko kila mwaka?. 🤔
Labda watanyanyua juu sana
Vinginevyo tutawashangaa
Mana mafuriko yashaharibu vya kutosha mabasi kwenye Yard ya mwendokasi
 
  • Love
Reactions: BAK

IQup

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
633
1,000
HUYU NAYE NI DHAIFU SANA, ATAKUJA KUUZA NCHI YETU KWA HIZI KAULI ZAKE......SISI HATUKUMCHAGUA YEYE ACHA AENDEE KUTUVURUGA MAANA BADO TUPO KWENYE MAOMBOLEZO YA RAIS WETU MPENDWA JPM. AONGEZE BIDII KWA KAULI HIZO
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,640
2,000
Hivi hawa waturuki wanaotuletea vyombo vya ndani hadi maofisini na wenyewe wanachukuliwa kama wawekezaji, iweje wazawa wanafurushwa kwamba wanatia aibu kwa wageni ili hali waturuki, wachina hawana mtaji unaowafanya kuitwa wawekezaji badala yake wanafanya umachinga......hii inanifanya nikumbuke sera ya uzawa aliyotaka kuileta hayati Idd Simba, kumbe wazawa wanatakiwa wafungiwe mahala wasiwatishe na kuwabuguzi wageni na kuaibisha watawala kwa wageni wao wa kibeberu......​
Ndiyo maana kwenye komenti yangu namba 31, nimeandika kuwa katika hii awamu Mungu anawaona.

Hivi, Waturuki , Wachina na Wasomalia wanauza bidhaa mitaani , maofisini, vyuoni , shuleni , halafu Bibi Kilemba anasema tunaondoa wamachinga ili wageni wasiogope kuja Tanzania!?

2025 atapigiwa kura na hao wageni, au Bibi atuuze kabisa huko nje ya nchi ili wageni awalete waishi huku Tanzania!

Yaani, Waturuki nasikia huko Tanzania hasa Jijini Mwanza wanapita taasisi kwa taasisi ,chuo hadi chuo , mtaa hadi mtaa wakiuza vyombo halafu yeye Bibi anaona ni sawa alivyosema!?

Awaondoe hawa Wamachinga wa kigeni ndiyo tujue kweli ameamua kuondoa machinga huko kwenye majiji/miji.

Ni Tanzania ambako wageni wanapewa thamani kuliko wenyeji.

Hakika, ukimpa mtu cheo anakuona hufai hasa baada ya kushiba, miezi sita tu Bibi kashiba anatuona hatufai.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Bora wapeleke hilo soko kwingine au wataadhirika. Jangwani wamehangaika nayo mara nyingi lakini hawajafanikiwa.
Mi naamini pakiwa designed kwa juu inawezekana
Sidhani km lile ni eneo lililoshindikana kwa teknolojia za dunia ya leo

Vinginevyo litageuka eneo la kuua watu pale
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
6,250
2,000
Kilichofanyika ni sahihi ila sababu aliyosema nadhani ina walakini...

Haina maana tutaacha kufanya yaliyo mema kwetu ili kufurahisha Umati
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,817
2,000
Ikifika 2025 wazungu watakuja kumpigia kura.
Nafikiri hakujifunza kwa JK umaarufu wake ulivyoporomoka kwa Kasi ya umeme.
🤣🤣
Pamoja na umaarufu wake mkubwa kwani hayati El Comandante JPM alichaguliwa kwa asilimia ngapi za kura?!!!

CCM haiwezi kutepeteshwa kirahisi....

Siempre JMT
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom