Rais Samia: Tumewachagua viongozi hawa kulingana na mfumo wa kisiasa ulivyo nchini

markp

Senior Member
Sep 26, 2013
181
299
Unaweza kujiuliza maswali mengi kwa kauli ya mwenyekiti wa CCM ambaye ametoa kauli yenye kuleta maswali kuhusu mfumo wa kisiasa uliopo sasa hapa nchini. Hebu tuangalie kwanza.

1. Nani mshauri wa mwenyekiti wa CCM na rais wa nchi yetu?

Ni mshauri pekee anayeweza kuona toafuti ya mifumo ya kisiasa katika awamu tofauti tofauti na akaona mfumo huu kuna mwana CCM atauweza na mwana CCM huyu ataushindwa.

2. Je, wanatuamisha kuwa mfumo wa kisiasa uliopo unafanana kabisa na uliokuwa kwa rais wa awamu ya 4? Kwakuwa ile timu ya awamu ya 4 inayohusika na usimamizi wa chama na timu ya uchaguzi ni kama yote imerudi vilevile.

3. Kwanini mama ndiye amchague wa kumsaidia na si wajumbe!?

Kwa mujibu wa kinana anasema alipigiwa simu na mama kuwa anamuhitaji awe makamu mwenyekiti wa CCM na kinana anasema hakuwa na hiyana yeye ni nani hata amkatalie mwenyekiti wake.

4. Je, kamati yenye wajumbe kibao ina kazi gani kama makamu mwenyekiti anawekwa au kupitishwa au kuteuliwa na mtu moja? Rejea maelezo swali la 3.

Wanahubiri demokrasia haipo chadema ila CCM ipo je hiyo ya kinana kupigiwa simu na kuhakikishiwa umakamu ndio demokrasia?

5. Hii timu mpya ya viongozi hawa wapya ni kwa ajili ya uchaguzi? Au kukusanya ela za uchaguzi? Maana kwenye suala la upigaji wapo vizuri. Au ni kwaajili ya kupoza huu moto wa katiba mpya!? Maana mfumo wa sasa unahitaji katiba mpya kama ulivyokuwa kwa Kikwete.

Kalamu inateleza kuliko kasi ya mkono huyu mama kwa ujumla kama ananichanganya mimi raia wa kawaida ni kama hanijali au kwakuwa hatukumchagua.
 
Tuendelee kuwa wavumilivu, kila kitu kitakuwa wazi njano inabaki kuwa njano na nyeusi ibaki kuwa hivyo.

Hii issue ya kupigiwa simu inaharibu dhima ya demokrasia na kutiwa hofu wenyeviti wa mikoa kubaki kama mabox tupu.
 
Tunaenda kushuhudia siasa TAMU za majukwaani ndugu!!Kujuana na Rushwa kuna Rudi upya kabisa na Bunge live TAMU la minyukano linarudi upya kabisa!!katiba itapatikana kwasababu katiba Sio ajenda ya ccm bali ya the state YOTE yatakamilika 2025! Baadae 2025/2030 tutakuwa na serikali mseto!!
 
Tunaenda kushuhudia siasa TAMU za majukwaani ndugu!!Kujuana na Rushwa kuna Rudi upya kabisa na Bunge live TAMU la minyukano linarudi upya kabisa!!katiba itapatikana kwasababu katiba Sio ajenda ya ccm bali ya the state YOTE yatakamilika 2025! Baadae 2025/2030 tutakuwa na serikali mseto!!
Bungeni wamejaa CCM tupu hakuna jipya na yeyote atakayejaribu kunyanyua mdomo atashughulikiwa kama Ndugai.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom