Rais Samia: Tuache migongano, kusengenyana, uvivu na uzembe ili tufanye kazi za watu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifunga Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) Jijini Arusha, leo tarehe 04 Machi, 2023

RAIS SAMIA ANAZUNGUMZA
Yapo mataifa ambayo yana watu wachache na ardhi yao ni ndogo lakini kwa kuwa uongozi wao ni bora yameendelea na furaha ndani ya Nchi ni kubwa, naamini sisi viongozi katika nafasi zetu tukibadilisha mitazamo yetu na kuacha mazoea tunaweza kuleta mafanikio makubwa.

Mitazamo yetu ikibadilika ni wazi migongano na mapambano sehemu ya kazi havitakuwepo, ubadhirifu utaisha, utendaji wa kazi utaimarika.

Niwasihi baada ya mafunzo haya twende tukaache migongano, kusengenyana, tukaaminiane, tuache uvivu, uzembe ili tukafanye kazi za watu kubwa zaidi tukaache dharau.

Tunawahudumia Wananchi wenye nchi, wala tusidharauliane wenyewe kwa wenyewe.

MAWASILIANO NDANI YA SERIKALI
Twende ngazi kwa ngazi, kosa kubwa tunalofanya ndani ya Serikali ni kudhani mawasiliano yamefanyika, tunasahau taarifa na mawasiliano.

Taarifa ni pale unapolisema jambo lakini haina maana itafika kule unapokusudia, ili ifike lazima kuwe na mawasiliano, pia hakikisha jambo lako limefika usidhani.

JIAMINI
Kama ukijiamini utafanikiwa, usipojiamini unajiwekea vikwazo mwenyewe, ukijiamini utapata mbinu, nendeni mkafanye kazi kwa kujiamini, aminini uwezo wenu, mnapofanya maamuzi sema haya ni maamuzi yangu.

Sema nimeamua haya kutoka na hali hii au hii, tusielekee kusema ‘haya ni maelekezo kutoka juu’, hiyo utakuwa haujiamini, fanya mamuzi kwa kujiamini na uwe tayari kutetea maamuzi yako
Huku ni kufuja pesa za walipa kodi tu .mpaka mtu anateuliwa kuwa waziri hajui majukmu yake tu mpaka tukamfundishe tena
 
Ni kweli

Maana awamu ya 5 kila kitu walisingizia ni amri kutoka Juu kumbe urongo mtupu

Mfano uwepo wa akina Halima Mdee walisingizia ni amri kutoka kwa Shujaa, lakini mbona bado wanadunda bungeni hadi Kesho!!
Wewe unapajua juu ni wapi?
Juu ni Ikulu inayokaliwa na mwenyekiti wa CCM taifa.
Wewe unataka Halima Mdee na genge lake la Covid 19 wafukuzwe bungeni ili CCM iaibike.
 
Mh Rais Samia amewaasa watumishi wa serikali kuhakikisha wanajiamini wanapotekeleza majukum yao.
Amesisitiza watende kwa kuzingatia sheria na wawe tayari kuwajibika kwa maamuzi hayo huku wakizingatia sheria zinasemaje.

Mh Samia amewaonya wasielekee kule tuliko toka kwa kudai ni amri kutoka juu. Hiyo ni dalili ya kutojiamini.
Ameyasema hayo akizungumza na mawaziri, manaibu waziri na makatibu wakuu na viongozi mbali mbali wa juu ktk serikali.
Well said, kuna watu wa ovyo sana utasikia amri kutoka juu, ukimuuliza juu kwa nani nimuone hasemi, uoga na kutokujiamini
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amefunga Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Jijini Arusha ambapo amewataka viongozi baada ya kurejea kwenye majukumu yao wakaache migongano, kusengenyana, kuhujumiana, uvivu na uzembe ili wakaaminiane na kushirikiana kufanya kazi za Watu (Wananchi)

Rais Samia amesisitiza kuwa WANANCHI NDIO WENYE NCHI NA HAWAFAI KUDHARAULIWA lakini pia amewataka viongozi kutodharauliana wao kwa wao.
 
Mh Rais Samia amewaasa watumishi wa serikali kuhakikisha wanajiamini wanapotekeleza majukum yao.
Amesisitiza watende kwa kuzingatia sheria na wawe tayari kuwajibika kwa maamuzi hayo huku wakizingatia sheria zinasemaje.

Mh Samia amewaonya wasielekee kule tuliko toka kwa kudai ni amri kutoka juu. Hiyo ni dalili ya kutojiamini.
Ameyasema hayo akizungumza na mawaziri, manaibu waziri na makatibu wakuu na viongozi mbali mbali wa juu ktk serikali.
Tatizo ni mifumo mibovu, kikifanyika nzuri ni cha Rais, kibovu cha watendaji
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amefunga Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Jijini Arusha ambapo amewataka viongozi baada ya kurejea kwenye majukumu yao wakaache migongano, kusengenyana, kuhujumiana, uvivu na uzembe ili wakaaminiane na kushirikiana kufanya kazi za Watu (Wananchi)

Rais Samia amesisitiza kuwa WANANCHI NDIO WENYE NCHI NA HAWAFAI KUDHARAULIWA lakini pia amewataka viongozi kutodharauliana wao kwa wao.
mwigulu alitudharau eti tuende Burundi
 
Dharau ipi kusengenyana ni kawaida.. Aanze na chama chake viongozi aliowateua… Hawa ndio wanawadharau sana wananchi kwa ubadhirifu wa mali na kodi za wananchi. Wamejawa viburi hawa ndio wamewafanya wananchi kuwa maskini kupindukia… Hawajali kwa ufupi… Hawa ndio wanadharau sio wananchi
Kusengenya si jambola kulalamikiwa ni jambo la kawaida katika jamii…
 
Mama yupo sahihi ,Viongozi hawana budi kufanya kazi kwa kufuata Katiba,sheria,taratibu na miongozo ya kazi,lakini moja ya nyenzo MUHIMU kabisa ni kupata KATIBA ILIYO BORA na ambayo upatikanaji wake utakuwa shirikishi

KATIBA MPYA BORA itazaa sheria nzuri,zitakazoleta KANUNI bora kwa wateule wa serikali..

Kanuni hizi zitaelezea kwa ufahasama kazi na mipaka ya kila mteule,anawajibika kwa nani,lakini vile vile itakuwa rahisi kwa mamlaka yake ya uteuzi ,kumpima

Rai kwa Mh Rais,harakisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya iliyobora kwa kuwa itakurahisishia utendaji wako wa kazi
 
Kutwaaaa ni msifanye mtajua wenyewe si uwafute kazi ukitiuambia sisi hatuwajui hao amri kutoka juu ni akina nani
 
Back
Top Bottom