Rais Samia, Tshs 100 inasambaza COVID-19, inatumika kutuibia, inasababisha urasimu na inaweza kumnyima mwenye mamilioni huduma ya kupata fedha zake

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
505
1,000
Utaratibu wa Sasa wa mabenki Ni lazima uwe na salio la kwenye line ya simu ndipo uweze kufanya miamala, Kwanza tu hii idea na mfumo wake unaonyesha Tanzania tuna wamiliki wa benk wasiotumia akili na wasiofanya utafiti au wanaoburuzwa. Kwasababu "Nina zaidi ya milioni kumi kwenye akaunti au hata laki moja lakini ili niitoe hiyo hela ambayo ni ya kwangu Hadi nikatafute shs mia niweke kwenye simu?

Mlipelekwa shule kufanya Nini? Kwamba nikipata tatizo sehemu ambapo siwezi kupiga simu au kuomba kuwekewa salio lakini Nina pesa kwenye akaunti nisizitoe? Kwanini hii shs mia msiikate kwenye miamala yangu au mganga wa maarifa mzee Mwigulu ndio kawatuma kwamba anataka mia ya kupitia vocha na siyo makato ya benki?

Yapo mambo mnapaswa kumkatalia Waziri na serikali kwa sababu hayana logic, yeye Kama anataka kuchukua mia mpeni option mkate kwenye transaction au njia nyingine lakini si huu ujinga unaoendelea Sasa. Yaani niende dukani kununua vocha niweke kwenye simu kisa nataka kulipa mia? This nonsense service kwa karne hii na inamfanya mtu mwenye fedha benki kushindwa kusaidiwa na fedha yake. Waziri akifeli kufikiri tusifeli wote kufikiri tuwe na alternative way yakulipa shs mia yake bila kuathiri huduma nyingine.

Lakini nirudi kwenu mabenk, mtu anaweka shs kwenye simu kwa ajili ya kufanikisha muamala mara network sijui service inakatika, inalazimu uweke Tena shs mia kufanya service ile ile bila mafanikio, huu siyo wizi? Kwanini mia isikatwe kwenye finalized transactions? Mnajisikiaje services zenu zipo down lakini mnawakata wananchi mia isiyo na justification? Huu wizi unawanufaisha nini? Je, huu siyo mpango wakuwarudisha watu wakapange foleni kwenye mabenki? Je mfumo huu wakutujaza kwenye mabenki hauwezi kuwa chanzo Cha kusambaa kwa maambukizi ya Covid kwa wananchi?

Dunia nzima kwa Sasa inarahisisha huduma kudhibiti mikusanyiko sisi tunatengeneza huduma zakuongeza mikusanyiko. Elimu ndogo hivi inawashinda wizara na mabenki kwanini? Shs mia ikaaambukize covid kwa sababu tu watu wachache wameshindwa kufikiri sawasawa.

Je, kuruhusu makato ya shs mia for unfinalized transaction si wizi ambao serikali inauunga mkono? Let us think kwa mapana la sivyo tusipofikiri nakuwaonyesha watawala tunavyowaza wao hawana uwezo Tena wakufikiri.

Mabenki tuambieni huu wizi mnaoshirikiana na serikali, hii mikusanyiko mnayotengeneza benki na huu urasmu wa uchumi mnotengeneza mnamkomoa nanini? Serikali imekataa kutusikiliza Basi ninyi si muwahurumie au wafanyakazi wenu mnowalazimisha watoe huduma atarishi? You will kill your employees just because of individual who can not speak for us and for you, think again and restructure the services. If someone wish that 100tsh to be deducted from sim card or if will be deducted from finalized bank transaction fine.

Taifa langu tutapata lini Uhuru wakusikiliza walioelimika wakiwaelewesha wasioelimika?
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,671
2,000
Dunia nzima kwa Sasa inarahisisha huduma kudhibiti mikusanyiko sisi tunatengeneza huduma zakuongeza mikusanyiko. Elimu ndogo hivi inawashinda wizara na mabenki kwanini? Shs mia ikaaambukize covid kwa sababu tu watu wachache wameshindwa kufikiri sawasawa.

Je kuruhusu makato ya shs mia for unfinalized transaction si wizi ambao serikali inauunga mkono? Let us think kwa mapana la sivyo tusipofikiri nakuwaonyesha watawala tunavyowaza wao hawana uwezo Tena wakufikiri.
Ni kama wamesema yupo kwa jirani, sijui kama atakusikia, akakuelewa, tuna kilometa 9 mbele ya safari
 

jeipm

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
378
1,000
Serikali ya awamu ya 2,4 na 6 hysee!! Hizi awamu zote ni pasua kichwa.

Lakini hii awamu ya sita ya huyu mama yetu mpendwa imefeli asubuhi sana.

Kama nchi imemshinda ajiuzulu
 

mazagazagatza

Senior Member
Jul 15, 2021
104
225
Serikali ya awamu ya 2,4 na 6 hysee!! Hizi awamu zote ni pasua kichwa..

Lakini hii awamu ya sita ya huyu mama yetu mpendwa imefeli asubuhi sana.

Kama nchi imemshinda ajiuzulu
Naona una chuki binafsi na maraisi waislamu. Unasumbuliwa udini tu huna lolote.

Hebu tuambie mambo ya msingi ambayo yanamtofautisha Samia na Magufuli mpaka uhitimishe Samia emefeli.
 

aldeo

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,553
2,000
Piga chini mobile bank tumia kadi yako kufanya muamala hapo utakuwa umejiondoa kwenye huo usumbufu.

Kwangu Airtel money, m-pesa watanisikia tuu, mobile bank watanisikia tuu sitoi pesa yangu kizembe
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,062
2,000
Ooh mi sitaki pesa za dhuluma, je hizi unazotuchukulia kinguvu sio dhuluma? maza umefeli mapema sana na utawala wako utakua mgumu sana maana wanakunung'unikia
 

Maji kupwa

JF-Expert Member
Jan 20, 2019
301
500
Wale wa sauth afrika tulikuwa tunawaona wajinga lakini mambo kma haya ya kijinga watayasikia kwa majirani ila sio kwa nchi yao maana huyo atayefikilia tu ujinga ndio watanza nae mapema sn kabla hilo jambo halijifaka kwa wananchi na likifika tu kwa rai mapema sn kesho wapo barabarani!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom