Rais Samia: Timu ya Olimpiki ya Tanzania ina Viongozi wengi kuliko wachezaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Kamati ya Olimpiki kujitathmini na kuja na mkakati utakaowezesha kuongeza idadi ya washiriki katika mashindano mbalimbali tofauti na ilivyo sasa ambapo timu husafiri na viongozi wengi zaidi ya wachezaji.

Ametoa maelekezo hayo wakati akipokea Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 23 (CECAFA Challenge Cup 2021), katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Agizo hilo limekuja siku chache tangu kumalizia kwa mashindano ya Olimpiki 2020 nchini Japan ambapo Tanzania ilipeleka wachezaji watatu, ambapo kati yao Alphonce Simbu ndiye alifanya vizuri zaidi kwa kushika nafasi ya saba katika mbio ndefu (42km) kwa wanaume.

Rais pia ametaka kuangaliwa vyema kwa wanamichezo nchini ili pindi wanapostaafu au kuumia wawe na maisha bora tofauti na hali ilivyo sasa ambapo wengi wao wamekuwa na maisha duni yasiyo akisi mchango wao kwa Taifa.

Ameitaka sekta binafsi kuwekeza zaidi kwenye michezo nchini kwasababu imekuwa ni biashara kubwa duniani na kuipongeza Kampuni ya Azam Media Limited kwa namna inavyojitahidi kuwekeza kwenye mchezo wa mpira wa miguu na ndondi (vitasa) nchini.


Swahili Times
 
Hivi nchi yetu huwa haina sera?

Mambo mengi huishia kuagizwa tu, na huishia hapo hapo kwenye maagizo...
 
Ili waende kutalii sio? Hatutakaa tupate hata medali moja labda dunia hii igeuke! Simbu aliyeotaga kipindi kile kaenda awamu hii kapokea za uso! Ngumi patupu, kuogelea patupu, mpira patupu....etc yani completely nothing
 
Simbu mzee sasa ilitakiwa kuwe vijana miaka 20 bado Simbu tu ? Hakuna warithi???
 
Viongozi wengi kuliko wachezaji🤣🤣🤣🤣🤣
Wachezaji wenyewe watatu😂😂😂😂😂
Hadi raha🤪🤪🤪🤪🤪
Asante sana 👍👍👍
 
Hivi Rais wa Tanzania kwenye safari zake za nje ya nchi uwa anaambatana na watu wa sekta mbali mbali kama vile wajasiriamali wadogo wadogo ili wakapate exposure na kutafuta fursa!? Au ni government officials tuu ndio wanaruhusiwa?
 
BBC wamezungumzia la muonekana wa vifua vya wachezazi. Isije ikawa wamemlisha maneno Mh Rais JMT. Hao wachezaji wote hamna aliye olewa mpaka ikasababisha hiyo concern.
 
Back
Top Bottom