Rais Samia tengua kauli ya Waziri Ummy Mwalimu ya kusimamisha uhamisho wa watumishi

Lkkl

Member
Dec 25, 2020
25
12
Mama samia tuaomba uwe unasikiliza kauli za mawazili unazitafakari, unapata a maoni ya wale wanao athiriwa na matamko hayo ili kubalance.

Mheshimiwa Rais uhamisho ni haki ya kiutumishi kwa mujibu wa sheria na katiba .

Mheshimiwa rais kauli ya Ummy kuzuia uhamisho wa watumishi ni kinyume na utaratibu.

Ni kweli hii ni kazi ya vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu kulaani tamko hilo kuomba kukuona lakini wameshindwa acha tutumie jukwaa hili kufikisha kilo chetu.

Mheshimiwa Rais ajira siyo utumwa, Kupangwa kijijini isiwe jinai

Kuna mtu ana genuine reasons za kuhama ambazo zingine ni kunusuru uhai wake, au watoto wake.

Sasa unamzuiaje kama bila yeye kuwepo pale matatizo ni mazito?

Mheshimiwa Ili mtu aombe ruhusa ya kuhama akubaliwe lazima astate sababu zinazojitosheleza.

Ni vizuri waziri ujue nature ya viongozi wetu wa chini ni waoga sana ukisema huko huku mtu anaweza kufa au kufiwa ofisin na asipewe uhamisho.

Jua familia zetu zina haki, watoto wetu wana haki ya kupata malezi ya wazazi au mzazi. mfano mzazi ni mmoja ataacha familia peke yake kwel?

Tunaomba vibali vyote vilivyo pitishwa na wakurugenzi vimekwama mikoani vitolewe.

Wakuu hao wapewe mamlaka ya kuona sababu ya uhamisho kwa kipindi hiki tukisubiri waraka utakao toa sifa za mtu kuhama

Mheshimiwa Rais mwambie waziri Ummy atengue kauli au ifute wewe, watumishi tunaumia huku na matamko. tuishi kwa hakI na sheria jamani inawezekana
 
Mama samia tuaomba uwe unasikiliza kauli za mawazili unazitafakari, unapata a maoni ya wale wanao athiriwa na matamko hayo ili kubalance.

Mheshimiwa Rais uhamisho ni haki ya kiutumishi kwa mujibu wa sheria na katiba...
Acha kazi kutwa kulia lia tu .

Nyie ndiyo mnahamasisha vijana wajiajiri alafu nyie mmekomalia ofisi
 
Mama samia tuaomba uwe unasikiliza kauli za mawazili unazitafakari, unapata a maoni ya wale wanao athiriwa na matamko hayo ili kubalance.

Mheshimiwa Rais uhamisho ni haki ya kiutumishi kwa mujibu wa sheria na katiba...
Hakuna kauli ya kutenguliwa,mnataka Vijijini aende nani? Hutaki acha Kazi,..Uhamisho kwenda mjini marufuku.
 
Hakuna kauli ya kutenguliwa,mnataka Vijijini aende nani? Hutaki acha Kazi,..Uhamisho kwenda mjini marufuku.
Serikalini Wana deka mno mfanyakazi anajihamisha ohh Mimi hapa staki nataka kule aiseeeee!!!

Hadi Raisi kasema Hadi Askari wanajiamlia nipange Traffic au Bandari sio kwingineko!!!

Barua za ajira mikataba hivi huwa zinaandikwaje? hazisemi.kuwa mtu Yuko Tayari kufanya kazi popote atajapopangiwa ? Au barua na mikataba inasema mwajiriwa atakapojipangia?

Wewe mleta mada gebu kasome barua yako ya ajira na mkataba wako wa ajira umeandikwa Nini? Ni wewe utakapojipangia au mwajiri atakapokupangia?
 
Hii ya lini Tena mkuu,Kuna waraka au ,mbona huku kwetu watumishi wanahama tu
Mkuu Kuna siku alitangaza kusimamisha Ila alisema kuwa anasimamisha wanaohamia kwenye miji manispaa na majiji, Ila sio kijijini.....huyu mleta mada ka generize na pengine huko kwako wanaohamia vijijini au ndio Yale ya MKONO MTUPU SIJUI HAULAMBWI.
 
Huyu Waziri bado ana akili za ndiyo kichwani mwake anafikiria ataendelea kuwa Waziri miaka yake yote... Ina yeye na familia yake wametika kwao kijijini wanaishi mjini lkn anakuja kutoa kauli ya ajabu eti hakuna mtu kuhama toka kijijini kwenda mjini.

Mimi Nina miaka zaidi ya minne kwenye ndoa sikuwahi kukaa na familia yangu zaidi ya mwezi mmoja tunafanya kazi mikoa tofauti. Alafu bado mke wangu na Baba yangu ni Wagonjwa lkn kamjitu kamoja kanasema kauli za ajabu eti Lisa yupo na madaraka Ila Waziri wa Tamisemi akumbuke Madaraka ni koti Leo hii amelivaa ipo siku atalivua.

Kuhama ni haki ya kila mtumishi . Kazi kisiwe kisingizio Cha kufanya watu wateseke na kushindwa kusaidia familia zao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom