Rais Samia: Tanzania tutakuja kwa nguvu yote Kenya kuwekeza

Kwenye Biashara Jamaa hawana Ukabila acha uongo, Wakikuyu wanafanya Baishara na Wajaluo, Ukabila sana kule unachagizwa na wanasiasa
Nawe bhana! Ukabila hata hapa kwetu upo, itakuwa Kenya. Nenda Moshi mjini uone kama kuna soda ya pepsi. Uliza kama kuna maji ya uhai. Yote hiyo ni ukabila ktk biashara. Eti hawataki mtu alete biashra aisiyomilikiwa na mchaga. Moshi ni Coca na maji ya kilimanjaro ya Bonite.

Tukiwasema wao wanadhani wanaonewa. NI WABAGUZI!
 
Huwa nakuamini ila kwa hili umeniangusha
Kuwekeza mahali inategemea na vivutio vilivyopo; na sio sisi kupanga cha kuwekeza
Think Big brother
Sawa.
Lakini si nimeuliza sisi tuna nini cha kuwekeza Kenya…

Unajua?
 
Rais Samia: Zipo kampuni 30 za Tanzania ambazo zimewekeza mtaji ndani ya Kenya wenye thamani wa shilingi za Kenya, Bilioni 19 na kutoa ajira kwa watu 2,640 lakini nikaweka ahadi kwamba, Tanzania sasa tutakuja kwa nguvu yote kuwekeza Kenya ili kukuza ujazo wa biashara

Awali Rais Samia alisema Kenya inashika nafasi ya tano kwa uwekezaji ndani ya Tanzania ambapo imewekeza miradi 513 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.7 ambayo imetoa ajira zipatazo 51 elfu kwa watanzania.

Kenya kuna kitu gani cha kuwekeza kama sio njia ya kutaka kuhalali kutorosha maliasili ya Tanzania?

We can't buy this kind of political trick at all
 
Azam pekee?
kwaufupi, watanzania hawana elimu na EAC.
namini kama hili litaenda vizuri bila ya hila kati ya nchi zetu hizi mbili naamin watanzania tutafanya mapinduzi makubwa kiuchumi.

UMAKINI UNAHITAJIKA JUU YA HILI. MAANA FUKARA KUJIPENDEKEZA AU KUWEKEZA KWA ALIE NA UKWASI,ASILIMIA KUBWA FUKARA ATEGEMEE KUUMIA.
 
Kama kuna makampuni 30 yapo yana operate, it means na yanaweza ongezeka hadi 60 au 90.

Angalao tumepata Rais SSH anayesema tukawekeze Kenya ili kulipa kisasi, kuliko kuliko aliyekuwa analipa kisasi kwa uwekezaji wa Kenya kwetu kwa kufunga na kuharibu biashara za Kenya.

"It always seems impossible until it is done"- Nelson Mandela
Naomba nkufungue macho, hotuba ya leo ya SSH ni kama aliyoitoa hayati JPM wakiwa na Kenyata. Mkuu fuatilia mambo. Dhamira ni njema, lakini Kenya si wema kwetu Watanzania. Nakumbuka namna walivyomtesa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete walikuwa wanamtenga mpaka kwenye Vikao. Walikuwa wanaitishana wao tu. Pia maziwa ya TZ yalikuwa yanazuiwa kuingia Kenya. JPM naye akawapiga block. Mtakumbuka walizuia ndege zetu kuingia nchini kwao, JPM akabamiza ukutani wakarudi katika Mstari. Mimi nasema hivi Wakenya si wa kwenda nao kipole pole, watatuendesha mpaka tukome.

Uganda nao wameshakaliwa kooni na Wakenya. Ujirani Mwema ni Muhimu lakini Ujirani mwema wenye manufaa. Si huwa mnaona Marekani akikaliwa kooni na China anafanyaje? Analipiza na Yeye halafu China wanakaa wanazungumza na Marekani. Ndiyo namna ya kwenda nao. Watanzania tusiwe Wanyonge sana.

Wao wakiwekeza sana kwetu ni faida pia maana wanalipa kodi. Niwakumbushe tu CRDB alipata shida sana kuingia Kenya kufanya biashara ya Banking, sijui kama alifanikiwa.

Utanzania kwanza ndugu zangu. Tusiwe Wanyonge. Mazungumzo ya Biashara yakiwepo tunakaa na Wakenya, wakituzingua, tunawazingua ndiyo Biashara inatakiwa kwenda hivyo.

Pia niwakumbushe Issue ya EPA, nahisi Nchi zote za Afrika Mashariki hazikusaini na Umoja wa Ulaya, Kenya wakaamua ku saini kivyao kitu ambacho si Kizuri kwa Africa Mashariki.
 
Nawe bhana! Ukabila hata hapa kwetu upo, itakuwa Kenya. Nenda Moshi mjini uone kama kuna soda ya pepsi. Uliza kama kuna maji ya uhai. Yote hiyo ni ukabila ktk biashara. Eti hawataki mtu alete biashra aisiyomilikiwa na mchaga. Moshi ni Coca na maji ya kilimanjaro ya Bonite.

Tukiwasema wao wanadhani wanaonewa. NI WABAGUZI!
Pepsi moshi zipo bhana, mbona nazipiga kila siku? Sema siyo Dominant kama Cocacola, ila Market share yao bado ni kubwa pia kuna mpaka Depot. Ila miaka ya 94 pale walikuwa hawana Chao kwasababu ya kiwanda cha Bonite Bottlers.
 
Naomba nkufungue macho, hotuba ya leo ya SSH ni kama aliyoitoa hayati JPM wakiwa na Kenyata. Mkuu fuatilia mambo. Dhamira ni njema, lakini Kenya si wema kwetu Watanzania. Nakumbuka namna walivyomtesa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete walikuwa wanamtenga mpaka kwenye Vikao. Walikuwa wanaitishana wao tu. Pia maziwa ya TZ yalikuwa yanazuiwa kuingia Kenya. JPM naye akawapiga block. Mtakumbuka walizuia ndege zetu kuingia nchini kwao, JPM akabamiza ukutani wakarudi katika Mstari. Mimi nasema hivi Wakenya si wa kwenda nao kipole pole, watatuendesha mpaka tukome.

Uganda nao wameshakaliwa kooni na Wakenya. Ujirani Mwema ni Muhimu lakini Ujirani mwema wenye manufaa. Si huwa mnaona Marekani akikaliwa kooni na China anafanyaje? Analipiza na Yeye halafu China wanakaa wanazungumza na Marekani. Ndiyo namna ya kwenda nao. Watanzania tusiwe Wanyonge sana.

Wao wakiwekeza sana kwetu ni faida pia maana wanalipa kodi. Niwakumbushe tu CRDB alipata shida sana kuingia Kenya kufanya biashara ya Banking, sijui kama alifanikiwa.

Utanzania kwanza ndugu zangu. Tusiwe Wanyonge. Mazungumzo ya Biashara yakiwepo tunakaa na Wakenya, wakituzingua, tunawazingua ndiyo Biashara inatakiwa kwenda hivyo.

Pia niwakumbushe Issue ya EPA, nahisi Nchi zote za Afrika Mashariki hazikusaini na Umoja wa Ulaya, Kenya wakaamua ku saini kivyao kitu ambacho si Kizuri kwa Africa Mashariki.
Unaweza ukawa na facts nzuri kuhusu mahusianao ya nchi hizi 3, lakini bado approach ya Mwendazake ilikuwa ya HOVYO tu.

Suala la maziwa kumbe alikuwa anatengeneza mazingira ya kiwanda chake alichozindua Bukoba mwaka jana Desemba
 
Sawa.
Lakini si nimeuliza sisi tuna nini cha kuwekeza Kenya…

Unajua?
Umekuwa ukisikia tukialika wawekezaji tuna waambia fursa zilizopo. Vivyo hivyo kenya nao wanatakiwa waseme nafasi zilizopo
Kimsingi Kenya sio Tajiri zaidi ya Vile viwanda vichache vya wazungu hivyo ina fursa nyingi tu za uwekezaji
Kwa haraka kuna mambo mengi tu mf

1. Kenya inategemea tanzania kwa mazao ya Kilimo hivyo mtanzania akiekeza kuprocess mazao yanayotoka tz ni rahisi kwani yeye anajua pa kuyapata kwa urahisi ( mahindi, parachichi, Juice, Viungo nk); kumbuka juice zao nyingi ni artificial
2. Kuanzisha Mabenki - kwa kuwa watanzania/wakenya wapo pande mbili ) hiyo pia ni Fursa
3. Nyama/Ngozi nk
 
Je Kenya wana ardhi kusema tutalima?, Je Wana upungufu wa viwanda vya bidhaa kama sabuni, mafuta ya kula dawa za meno nk kiasi ndo tunaenda kwa nguvu kuwekeza? Sioni chochote tunaweza kuwekeza Kenya zaidi ya wao kutugeuza sisi soko la bidhaa zao watakazozalisha kwa gas yetu tuliyo wawezesha.

Ktk eneo hili naona tukiua sera yetu ya viwanda na vijana wanaoshangilia hili on the other hand wawe tayari kuondoa lawama za ajira kwa Serikali pia. Because hauwezi ukaunga mkongo mpango unaokwenda kuua mgango wa Mapinduzi ya viwanda wa ndani ya nchi yako huku ukitarajia kupata ajira zilizotengenezwa na serikali.
 
NI KWENDA NAO JINO KWA JINO USIWE NA SHAKA.

Sisi pia mmoja mmoja, jamii na serikali tunapaswa kuamka na kuchakarika kama wao na kushindana nao kwa uora wa bidhaa. Kuna baadhi ya vitu vinayotengenezwa Kenya ambavyo sisi pia tunatengeneza (cement, mafuta, maziwa, etc. ) ila kuna vyao vilivyo bora kuliko vyetu (mimi napenda sana maziwa ya Brookside, sijui kama kuna maziwa mazuri zaidi East Africa) ila vingine ni vya kiwango cha chini zaidi ya vyetu (naona chai na kahawa ya TZ ni bora kuliko za Kenya, pombe zetu ziko vizuri, ndizi, maparachichi, mchele na unga ni bora kuliko kwao nk..) Hata tasnia ya muziki miaka ya karibuni nimeona tunakubalika kule kuliko wanavyojikubali wenyewe na kuliko sisi tunavyowakubali wasanii wao. Hili si suala dogo.

Nadhani cha kwanza serikali yetu kutusaidia watz ni kutuwekea mazingira mazuri na nafuu mfano kupunguza kodi kwa viwanda au shughuli za kilimo za wazawa. Wafanye iwe rahisi kutengeneza bidhaa hapa na kuzisafirisha kwenda Kenya na nchi zingine zilizotuzunguka (tunaweza kushindana nao bila kutegemea soko lao tu) na ikiwezekana hata wafike mahali waweze ku'subsidize' bidhaa zetu ziende kwao kwa bei nafuu ili zisambae kwao, (nadhani korosho, karanga maziwa, mafuta ya alizeti, maji ya kunywa, etc vingefaa kwa kitu kama hiki). Ila picha tuliyozoea huku ni kuwa serikali inakomaa kutoza mikodi na kuchota hela za waTz kwa namna yoyote mpaka hata waTz wanaona bora wafunge biashara zao.

Ukiingia kwenye utalii, mbuga zote za maana, milima, maziwa na mito n.k. yaani utachokuta kwao huku tuna zaidi yao (nahisis hata wale wanyama wanaohama huwa wanakaa upande wao muda mchache kuliko huku) na bado kuna upande wa utu wetu na hali ya utulivu tulionayo huku inayofanya mtu ajihisi faraja kutembelea nchi yetu. Makabila na tamaduni kibao ila 'cultural tourism' hatujaipa kipaumbele vya kutosha. Wakenya wamepaisha kabila la kimaasai mpaka walio nje wanadhani kabila hilo liko Kenya tu na akiona rubega wazo la kwanza linalomjia...anawaza 'Kenya'. Tunaweza kuhakikisha mtu aliye akiona rubega awaze 'Tanzania'. Hata kuna watu nchi za Magharibi wanaodhani Mt. Kilimanjaro uko Kenya, Olduvai Gorge iko Kenya na Great Rift Valley iko Kenya tu (huku TZ kuna great rift valley 2 sio moja tu ila uliza nani anajua hili) mpaka watu wanasafiri kwenda kule wakifikiri watavikuta hivi kule. Kuna vingine vingi.

Kikubwa ninachoona kwa Wakenya ni wako aggressive kwenye biashara, ni watu wa kujimwambafy na kujipaisha (Mkenya mweye laki 5 ukikaa nae utadhania ana milioni, sisi ni kinyume, tunapenda kujishusha mno) na wanauzalendo. Jamaa wanapenda vya kwao bhana. Nairobi ingia mtaani, benki, duka la Safaricom...utakuta warembo wametupia vibangili vyao... Nakumbuka nilisikia zamani (early 2000s) kuwa South African Breweries waliweza kupenyeza Uganda na Tanzania ila Kenya hawakuweza kwa sababu Mkenya hanywi bia ya nje hivi hivi tu na hii ni moja ya changamoto katika kupeleka bidhaa zetu kwao ila isiwe tabu, tukiamua tunaweza.

kenya bead.jpg

tusker.jpg
 
kwaufupi, watanzania hawana elimu na EAC.
namini kama hili litaenda vizuri bila ya hila kati ya nchi zetu hizi mbili naamin watanzania tutafanya mapinduzi makubwa kiuchumi.

UMAKINI UNAHITAJIKA JUU YA HILI. MAANA FUKARA KUJIPENDEKEZA AU KUWEKEZA KWA ALIE NA UKWASI,ASILIMIA KUBWA FUKARA ATEGEMEE KUUMIA.
Nawe jielimishe kwanza. EAC siyo jumuiya ya nchi makini. Ni bhla bhla tu! Angalia Sudan ya kusini, Angalia uhusiano wa Burundi na Rwanda. Angalia uhusiano wa Uganda na Rwanda. Angalia uhusiano wa TZ na Kenya. Angalia uhusiano wa Kenya na Uganda. Ni mzunguko wa kufanyiana vituko tu! Hili ni kundi la mazungumzo tu hadi wanakosa mishahara kwa nchi kushindwa kuchagia. Nchi pekee zinazopendana ni TZ na Uganda na TZ na Burundi. Rwanda hana jinsi lakini anatuangalia kwa tahadhari ya kuwinda nafasi.

Jumuiya makini kwa upande wetu TZ ni SADC . Tusipotezeane muda na mambo ya EAC. Tunajua ni majirani lakini ni washindani wetu, hakuna ushirikiano.
 
NI KWENDA NAO JINO KWA JINO USIWE NA SHAKA.

Sisi pia mmoja mmoja, jamii na serikali tunapaswa kuamka na kuchakarika kama wao na kushindana nao kwa uora wa bidhaa. Kuna baadhi ya vitu vinayotengenezwa Kenya ambavyo sisi pia tunatengeneza (cement, mafuta, maziwa, etc. ) ila kuna vyao vilivyo bora kuliko vyetu (mimi napenda sana maziwa ya Brookside, sijui kama kuna maziwa mazuri zaidi East Africa) ila vingine ni vya kiwango cha chini zaidi ya vyetu (naona chai na kahawa ya TZ ni bora kuliko za Kenya, pombe zetu ziko vizuri, ndizi, maparachichi, mchele na unga ni bora kuliko kwao nk..) Hata tasnia ya muziki miaka ya karibuni nimeona tunakubalika kule kuliko wanavyojikubali wenyewe na kuliko sisi tunavyowakubali wasanii wao. Hili si suala dogo.

Nadhani cha kwanza serikali yetu kutusaidia watz ni kutuwekea mazingira mazuri na nafuu mfano kupunguza kodi kwa viwanda au shughuli za kilimo za wazawa. Wafanye iwe rahisi kutengeneza bidhaa hapa na kuzisafirisha kwenda Kenya na nchi zingine zilizotuzunguka (tunaweza kushindana nao bila kutegemea soko lao tu) na ikiwezekana hata wafike mahali waweze ku'subsidize' bidhaa zetu ziende kwao kwa bei nafuu ili zisambae kwao, (nadhani korosho, karanga maziwa, mafuta ya alizeti, maji ya kunywa, etc vingefaa kwa kitu kama hiki). Ila picha tuliyozoea huku ni kuwa serikali inakomaa kutoza mikodi na kuchota hela za waTz kwa namna yoyote mpaka hata waTz wanaona bora wafunge biashara zao.

Ukiingia kwenye utalii, mbuga zote za maana, milima, maziwa na mito n.k. yaani utachokuta kwao huku tuna zaidi yao (nahisis hata wale wanyama wanaohama huwa wanakaa upande wao muda mchache kuliko huku) na bado kuna upande wa utu wetu na hali ya utulivu tulionayo huku inayofanya mtu ajihisi faraja kutembelea nchi yetu. Makabila na tamaduni kibao ila 'cultural tourism' hatujaipa kipaumbele vya kutosha. Wakenya wamepaisha kabila la kimaasai mpaka walio nje wanadhani kabila hilo liko Kenya tu na akiona rubega wazo la kwanza linalomjia...anawaza 'Kenya'. Tunaweza kuhakikisha mtu aliye akiona rubega awaze 'Tanzania'. Hata kuna watu nchi za Magharibi wanaodhani Mt. Kilimanjaro uko Kenya, Olduvai Gorge iko Kenya na Great Rift Valley iko Kenya tu (huku TZ kuna great rift valley 2 sio moja tu ila uliza nani anajua hili) mpaka watu wanasafiri kwenda kule wakifikiri watavikuta hivi kule. Kuna vingine vingi.

Kikubwa ninachoona kwa Wakenya ni wako aggressive kwenye biashara, ni watu wa kujimwambafy na kujipaisha (Mkenya mweye laki 5 ukikaa nae utadhania ana milioni, sisi ni kinyume, tunapenda kujishusha mno) na wanauzalendo. Jamaa wanapenda vya kwao bhana. Nairobi ingia mtaani, benki, duka la Safaricom...utakuta warembo wametupia vibangili vyao... Nakumbuka nilisikia zamani (early 2000s) kuwa South African Breweries waliweza kupenyeza Uganda na Tanzania ila Kenya hawakuweza kwa sababu Mkenya hanywi bia ya nje hivi hivi tu na hii ni moja ya changamoto katika kupeleka bidhaa zetu kwao ila isiwe tabu, tukiamua tunaweza.

View attachment 1774008

View attachment 1774016
Kwa ujumla ulichoonesha ni upuuzi waa Wakenya. Tabia yako ya kupenda maziwa ya Brookside sijui kama ulijiuliza ni nini unachokunywa. Brookside sasa hivi inaendeshwa na shares za Newzealand. Unakunywa mchanganyiko wa maziwa ya unga toka Newzealand.

Tabia ya kugomea kununua bia ya nje ya Kenya, ndo tabia inayosababisha usiweze kuwekeza Kenya. Siyo uzalendo ni ubaguzi na ukabila. Leo hii kuna wa-TZ wana akaunti KCB, lakini ukifungua tawi la NBC Kenya wanaisusia. Ni ubaguzi unaoanzia kwenye familia, wao kwa wao, then kwa waafrika wengine. Lakini ni wadhaifu sana kwa ngozi nyeupe, hadi kuchapwa viboko. Hapa kwetu pia hili lipo kwa makabila fulani, tukubali wazi.
 
Back
Top Bottom