Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,735
- 6,292
“Tanzania tuna wagonjwa wa wimbi la Tatu la Corona. Hili jambo bado lipo, tuchukue hadhari zote na tunawaomba viongozi wa dini mseme hili kwa sauti kubwa"
Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na baraza la maaskofu katoliki (TEC) #Tanzania #COVID19
=========
Rais Samia Suluhu: Wahashamu, baba Maaskofu kama mnavyofahamu, dunia kwasasa inakabiliwa na mlipuko wa Covid-19 na nafahamu kanisa tangu mwanzo limekuwa na msimamo Thabit katika kupambana na ugonjwa huu hivyo basi niwaombe sana Maaskofu msisahau kuwakumbusha waumini kuhusu wa kujikinga na kuchukua Tahadhari zote zinazoelekewa na wataalam wa Afya dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Kwakuwa Kinga ni Bora kuliko Tiba, tusiache kutumia kila kitakachotukinga na maradhi haya ili kuepesha vifo vya makundi.
Kama tunavyojua, duniani sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia, limekwenda limepungua kidogo, tumeingia Wimbi la Pili tumekwenda nalo na sasa kuna Wimbi la Tatu.
Ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika kwenye wimbi hili la Tatu. Kama mnakumbuka siku nilitembelea hospitali ya Mwananyamala, kuna wodi daktari mfawidhi alikuwa ananiingiza akaniambia humu kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, nikamwambia hebu kuwa muwazi, ni covid, akaniambia ndio Covid wakati wapiga picha wangu tayari wameshatangulia, nikawaambia nyie tokeni haraka huko.
Kwahiyo ni kusema kwamba hili jambo bado lipo, tusijiche, bado lipo tuchukue hadhari zote na tunawaomba sana viongozi wa Dini mliseme hili kwa sauti kubwa, kwa waumini wetu ili tujiepushe na vile vifo vya makundi.
Pamoja na yote hato, ni vyema pia tumuombe Mungu kwa kiasi kikubwa aendelee kutuepusha na kutupa hifadhi yake kutokana na maradhi hasa Janga hili la Corona kwakuwa yeye ndio Muweza wa Yote.