Rais Samia, Tanzania ni moja na hakuna mpasuko wowote. Tupo wamoja sana

Nchi ya Tanzania ina watu takribani milioni 60, kila mtu ana vipaumbele vyake...hivyo huwezi kumridhisha kila mtu mama.

Asilimia 90 ya watanzania ni maskini: hawahitaji magari ya benzi wala nyumba za kishi baada ya kustaafu kushika chaki na kazi zingine za umma.

Wanahitaji maji safi na salama, huduma bora za afya, elimu bora na huduma zingine za kijamii.

Ukitaka kuwafurahisha baadhi ya watu kwenye asilimia 15 iliyobakia utapotea! Utabaki kukumbukwa kwa kuharibu nchi na hatma yake utakutana na mkono wa Allah aliyekupa nafsi hiyo.


Mama Samia, hutapendwa kwa kwenda kinyume na mtangulizi wako kwenye mambo yenye maslahi ya nchi. Mwenzako kamaliza zamu yake...nadhani umeshuhudia namna umma wa watanzania ulivyompokea licha ya madhaifu yake kama binadamu.


Kikubwa timiza wajibu wako ukiingozwa na katiba na uzalendo wa hali ya juu.

Tumia nguvu uliyopewa, usipende kufanyiwa maamuzi na watu. Wengine baadhi ya washirika wako sio wema.

Wapinzani ni wapinzani tu...lengo lao kuchukua nchi hivyo kuwa nao makini.

Usiingie mkenge kwa kivuli cha kujenga umoja wa kitaifa. Nchi hii ni moja na hakuna mpasuko wowote labda mitandaoni ila uraiani tupo wamoja sana. Na hayati JPM ametupa nguvu sana kiasi kwamba tunajua kipi kizuri na kipi kibaya.

Mwisho nakutakia kila la kheri.

Happy Mothers' Day!
Angalizo lingine kwa mama,ukiona watu wote wabakusifia,wabakupenda na hata wapinzani sugu wa serikali ya CCM wanakuona u Bora kuwa ya kuwa waneona upenyo(udhaifu) wako.
Tuwe wakweli toka enzi za Mwl Nyerere,Mwinyi,Mkapa,na Magufuli,hatujawahi kuwa na urafiki,wa dhati na Kenya.Siku zote urafiki wetu,ujirani wetu,matendo ya Wake ya kwa Watanzania siku zote ni ya mashaka.
Chunga mama naenda polepole kwa tafakuri Pana.Waliokutangulia wakiona Nini mpaka hawakuwa na ukaribu mkuu na Wakenya?
Rostam alikupa angalizo kwamba alionana na wakuu wa Kenya tokea meals 2017, mpaka leo anazungushwa kupata kibali cha uwekezaji Kenya.
Wakenya walituambia mahindi yeti tana simu hayafai kuliwa na Wakenya ,Leo bila ichunguzi Kama simu imeondolewa,mahindi hayo hayo,sasa yanaruhusiwa.Tuna urafiki wa mashaka,Wenzetu wanakuona sisi hambanazo na wanaweza kutuburuza,njia ambayo naiona tunaifuata tusikipokuwa na angalizo la kina.
 
Tr


Truth be told, hata yeye mwenyewe hajielewi elewi. Imagine hata hotuba akishamaliza kuandaliwa, utasikia anaambiwa: ^Mheshimiwa, hii itakuwa tamu sana this time; ukifika hapa baada ya hizi takwimu hapa, weka kichekesho kidogo kwa ajili ya waandishi wa habari na ili kuwasahaulisha wananchi the things that matter the most.^
Wewe ndiyo hujielewi kwa njaa zako.
Safari hii hakuna nafasi kwa mataga na sukuma gang kuonekana ikulu .

Mkifika mnaishia getini maana zama zenu zimekwisha.
 
Mtateseka saaana nyie ,mama piga kazi,ondoa mazagazaga yote yaliotaka kugawa nchi vipande kwa kisingizio uchwara eti uzalendo what a joke?
Kundi hilo ni hatari sana maana kwao kila kitu anacho kifanya mama wao wanakikosoa na kusahau maovu yaliyokuwa yanafanywa na baba yao.
 
Wewe unaongea kama nani? nchi inaongozwa na wazenji hii sasa wewe shobo zako zinatoka wapi?
Hata kama ni wazenji lakini pia ni wanafamilia ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mkome kumkwamisha rais mpenda amani na mshikamano.
 
Rais ametumia akili kumpa Mpango umakamu, atamsaidia sana akiwa ni mtu anayeijua serikali na anaijua bara vyema.

Pia asije kushawishika kumtosa Majaliwa hata iweje. Jamaa ni mchapa kazi na mzalendo.
 
Tr


Truth be told, hata yeye mwenyewe hajielewi elewi. Imagine hata hotuba akishamaliza kuandaliwa, utasikia anaambiwa: ^Mheshimiwa, hii itakuwa tamu sana this time; ukifika hapa baada ya hizi takwimu hapa, weka kichekesho kidogo kwa ajili ya waandishi wa habari na ili kuwasahaulisha wananchi the things that matter the most.^
haha story za kusadikika. umetia chumvi sana
 
Una akili kubwa Sana wewe, huyu mama tunakwenda naye akianza kupuyanga tu tutamchana live mchana kweupe.Afanye ziara mikoani ajionee live matatizo ya wananchi siyo kukaa tu ofisini na kufanya ziara za nje ya nchi.
 
Ukweli mchungu:

1. Mama kuleta maridhiano - hapo yuko vizuri.
2. Mama kuwasikiliza wataalamu na hasa tume yake ya magonjwa - hapo yuko vizuri.
3. Mama kutaka ripoti za CAG kuhusiana na BOT na TPA March 2021 - Mama yuko vizuri. Hapo mwendelezo unakosekana.
4. Mama kuwashughulikia wavunja katiba bila kuangalia makunyanzi. Hapo kuna ukakasi hasa kwa kutoyachukulia hatua hadi sasa yale manyang'au yote yaliyotaka kumzibia yeye riziki, March 2021.

Haya mengine sasa ya mzee Mwinyi na magari, JK na manyumba, mama ajitafakari hii nchi ni maskini mno. Anaweza kufanya vyema zaidi kuliko alivyofanya.

Ni wazi kuwa kwa wafuasi kindaki ndaki wa mwendazake, mama ni mzigo mkubwa wa miiba kwao.

Binadamu hajawahi kuwa mkamilifu. Yote kwa yote mama yuko vizuri.

Kazi iendelee!
Mkuu mama anaenda taratibu ,manyangau yalikuwa yamejipanga mnooo
 
Una akili kubwa Sana wewe, huyu mama tunakwenda naye akianza kupuyanga tu tutamchana live mchana kweupe.Afanye ziara mikoani ajionee live matatizo ya wananchi siyo kukaa tu ofisini na kufanya ziara za nje ya nchi.
Aliefanya ziara tanzania nzima alifanikiwa kupunguza umaskini kiasi gani?
 
Back
Top Bottom