Rais Samia, Tanzania ni moja na hakuna mpasuko wowote. Tupo wamoja sana

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,288
2,000
Nchi ya Tanzania ina watu takribani milioni 60, kila mtu ana vipaumbele vyake, hivyo huwezi kumridhisha kila mtu mama.

Asilimia 90 ya watanzania ni maskini: hawahitaji magari ya benzi wala nyumba za kishi baada ya kustaafu kushika chaki na kazi zingine za umma.

Wanahitaji maji safi na salama, huduma bora za afya, elimu bora na huduma zingine za kijamii.

Ukitaka kuwafurahisha baadhi ya watu kwenye asilimia 15 iliyobakia utapotea! Utabaki kukumbukwa kwa kuharibu nchi na hatma yake utakutana na mkono wa Allah aliyekupa nafsi hiyo.

Mama Samia, hutapendwa kwa kwenda kinyume na mtangulizi wako kwenye mambo yenye maslahi ya nchi. Mwenzako kamaliza zamu yake. Nadhani umeshuhudia namna umma wa watanzania ulivyompokea licha ya madhaifu yake kama binadamu.

Kikubwa timiza wajibu wako ukiingozwa na katiba na uzalendo wa hali ya juu.

Tumia nguvu uliyopewa, usipende kufanyiwa maamuzi na watu. Wengine baadhi ya washirika wako sio wema.

Wapinzani ni wapinzani tu, lengo lao kuchukua nchi hivyo kuwa nao makini.

Usiingie mkenge kwa kivuli cha kujenga umoja wa kitaifa. Nchi hii ni moja na hakuna mpasuko wowote labda mitandaoni ila uraiani tupo wamoja sana. Na hayati Magufuli ametupa nguvu sana kiasi kwamba tunajua kipi kizuri na kipi kibaya.

Mwisho nakutakia kila la kheri.

Happy Mothers' Day!
 
UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
11,452
2,000
Naona kabisa huko mbele atakuja kupata lawama kutokana na jinsia yake kuwa ndio tatizo.
 
Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,402
2,000
Tr
Maza naona km simuelewi elewi!!!!!
Truth be told, hata yeye mwenyewe hajielewi elewi. Imagine hata hotuba akishamaliza kuandaliwa, utasikia anaambiwa: ^Mheshimiwa, hii itakuwa tamu sana this time; ukifika hapa baada ya hizi takwimu hapa, weka kichekesho kidogo kwa ajili ya waandishi wa habari na ili kuwasahaulisha wananchi the things that matter the most.^
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,262

Mtateseka saaana nyie ,mama piga kazi,ondoa mazagazaga yote yaliotaka kugawa nchi vipande kwa kisingizio uchwara eti uzalendo what a joke?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
9,043
2,000
Ukweli mchungu:

1. Mama kuleta maridhiano - hapo yuko vizuri.
2. Mama kuwasikiliza wataalamu na hasa tume yake ya magonjwa - hapo yuko vizuri.
3. Mama kutaka ripoti za CAG kuhusiana na BOT na TPA March 2021 - Mama yuko vizuri. Hapo mwendelezo unakosekana.
4. Mama kuwashughulikia wavunja katiba bila kuangalia makunyanzi. Hapo kuna ukakasi hasa kwa kutoyachukulia hatua hadi sasa yale manyang'au yote yaliyotaka kumzibia yeye riziki, March 2021.

Haya mengine sasa ya mzee Mwinyi na magari, JK na manyumba, mama ajitafakari hii nchi ni maskini mno. Anaweza kufanya vyema zaidi kuliko alivyofanya.

Ni wazi kuwa kwa wafuasi kindaki ndaki wa mwendazake, mama ni mzigo mkubwa wa miiba kwao.

Binadamu hajawahi kuwa mkamilifu. Yote kwa yote mama yuko vizuri.

Kazi iendelee!
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
4,780
2,000
Usimtishe Rais SSH kwa sababu ya umati uliokuja kumuaga Mwendazake, hiyo ni sababu dhaifu Sana.

Watu mtaani kwenda kuaga maiti ya marehemu ni mila za Kiafrika. Hapa Dar hata Marehemu Stephen Kanumba naye alifunga mtaa kwenye msiba wake.

Hata Ruge Mutahaba naye alifunga nyomi.

Kwa taarifa yako Rais SSH anakubalika kwa 80+% kwa namna tu anavyosimamia Utawala wa Sheria, Uhuru wa kujieleza, na namna anavyotaka kuboresha uchumi.

Nchi tayari imeponywa, na wala usimhusishe kabisa na yule Shetani wa Chato. Tuko na maisha mapya na mtazamo mpya, hakuna watu kuuliwa, kutekwa na kunyang'anywa fedha zao
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,800
2,000
Nchi ya Tanzania ina watu takribani milioni 60, kila mtu ana vipaumbele vyake...hivyo huwezi kumridhisha kila mtu mama.

Asilimia 90 ya watanzania ni maskini: hawahitaji magari ya benzi wala nyumba za kishi baada ya kustaafu kushika chaki na kazi zingine za umma.

Wanahitaji maji safi na salama, huduma bora za afya, elimu bora na huduma zingine za kijamii.

Ukitaka kuwafurahisha baadhi ya watu kwenye asilimia 15 iliyobakia utapotea! Utabaki kukumbukwa kwa kuharibu nchi na hatma yake utakutana na mkono wa Allah aliyekupa nafsi hiyo.

Mama Samia, hutapendwa kwa kwenda kinyume na mtangulizi wako kwenye mambo yenye maslahi ya nchi. Mwenzako kamaliza zamu yake...nadhani umeshuhudia namna umma wa watanzania ulivyompokea licha ya madhaifu yake kama binadamu.

Kikubwa timiza wajibu wako ukiingozwa na katiba na uzalendo wa hali ya juu.

Tumia nguvu uliyopewa, usipende kufanyiwa maamuzi na watu. Wengine baadhi ya washirika wako sio wema.

Wapinzani ni wapinzani tu...lengo lao kuchukua nchi hivyo kuwa nao makini.

Usiingie mkenge kwa kivuli cha kujenga umoja wa kitaifa. Nchi hii ni moja na hakuna mpasuko wowote labda mitandaoni ila uraiani tupo wamoja sana. Na hayati JPM ametupa nguvu sana kiasi kwamba tunajua kipi kizuri na kipi kibaya.

Mwisho nakutakia kila la kheri.

Happy Mothers' Day!
Wewe ni mnyarwanda habari za rais wa Tanzania zinakuhusu nini?
Au unadhani hatukujui kuwa uliingilia mkoani kagera?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom