Rais Samia: Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi unakua kwa kasi. Tumepunguza kiwango cha umasikini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi 10 za Afrika ambazo Uchumi unakua kwa kasi. Pia, imekuwa na utulivu wa Mfumuko wa Bei na Thamani ya Fedha.

Ameeleza, "Tumeona viashiria vya Maendeleo kwenye Maendeleo ya mtu. Tumeweza kupunguza kiwango cha umasikini kutoka 28.6 mwaka 2015 hadi 26.2 mwaka 2020. Tumeweza kuingia Uchumi wa Kati Julai mwaka jana"

Amesema hayo katika Ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha Nchini.

B7B7A101-1FC2-4B49-9884-A0B54F8BA342.jpeg

1A98C9A6-9625-43A5-B3B3-DD01074A5127.jpeg

4617D6EE-3C86-4FE5-B40C-3ACD559F956D.jpeg
 
Ni kweli kwa 2015 hadi 2020 hali ilikuwa kama alivyosema bila shaka ila kuanzia June 2021 hadi hii November kuna mfumko wa bei kiwango cha SGR hadi tumeanza kupoteana sisi wananchi.

Bidhaa toka viwandani ni vya moto sana mfano saruji iliuzwa 18,000 kwa kilo 50 kunako Februari 2021 ila leo hii ni 23,000 kwa mfuko huo.

Bar soap B29 iliuzwa 250 ila leo ni 500 kwa kipande.

Kilo ya ngano iliuzwa kwa sh. 1200 na leo inauzwa kwa sh 1500 hadi 1,700

Nondo mm 12 iliuzwa kwa sh. 16,000 leo inauzwa kwa sh. 26,000

Wapangishaji wa nyumba nao wameamua. Wauza matunda nao mwendo ule ili tu wapate pesa ya kutosha kumudu ongezeko la bei kwa bidhaa za viwandani wanavyohitaji kila siku kama vile mafuta, chumvi, ngano, n.k
 
Yaani nimejikuta napata hasira tu...☹️
Yaani kwakua anakula na kusaza basi anadhani mitaani pia ni kama white house..🙃
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi 10 za Afrika ambazo Uchumi unakua kwa kasi. Pia, imekuwa na utulivu wa Mfumuko wa Bei na Thamani ya Fedha...
Tangu Samia ameshika madaraka maisha ya watanzania walio wengi yamezidi kuwa magumu kuliko wakati wowote huko nyuma

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
kweli kabisa uchumi umekua mpaka tumeamua kujitegemea wenyewe hatutegemei mabeberu,mvua,umeme sisi ni dona kant bana
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni miongoni mwa Nchi 10 za Afrika ambazo Uchumi unakua kwa kasi. Pia, imekuwa na utulivu wa Mfumuko wa Bei na Thamani ya Fedha.

Ameeleza, "Tumeona viashiria vya Maendeleo kwenye Maendeleo ya mtu. Tumeweza kupunguza kiwango cha umasikini kutoka 28.6 mwaka 2015 hadi 26.2 mwaka 2020. Tumeweza kuingia Uchumi wa Kati Julai mwaka jana"

Amesema hayo katika Ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha Nchini.

View attachment 2023075

View attachment 2023076
View attachment 2023077
Tunaenda vizuri
 
Watumishi wa umma wanashindwa kuwaongezea mishahara mwaka 6 sasa.
 
Back
Top Bottom