kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 118
- 237
"Sisi hapa Tanzania tumeamua kuizingatia misingi hiyo (haki) na nataka niwahakikishie kwamba tutajitahidi kuijenga Tanzania yenye Haki, Demokrasia , Usawa na Mafanikio. Na ndio maana katika kipindi hiki tumekuja na idea ya zile 4R's". - Rais Samia Suluhu
Rais Samia ameyasema hayo katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, Aidha katika kuzingatia misingi hiyo Serikali yake imekua ikikutana na vyama mbalimbali vya siasa na kuzungumza mambo mbalimbali yanahusu nchi. Rais Samia ana amini nchi yoyote ili ifikie maendeleo ya kweli lazima ifate misingi ya haki.
“Nataka nisisitize kwamba kutenda haki na kuheshimu utawala bora ni misingi ambayo Serikali yoyote inayotokana na watu haina budi kuifuata bila shinikizo lolote kutoka nje. Kama Serikali ni ya watu [..] haina budi Serikali hiyo kufuata misingi hiyo.”
Katika hotuba yake pia aliwahusia wanasheria kuzingatia misingi ya haki kwa kuhakikisha hawapokei rushwa na kuonea watu wengi kwa kuwapa makosa ambayo hawajayafanya. Pia amekihusia chama hiko kuonyesha nia dhati ya kusaidia nchi zao na kutumikia mataifa zao lakini sio kama ilivyokua awali kwa chama cha wanasheria Tanzania.
“Tanzania miaka minne mitano iliyopita tulikuwa na Tanganyika Law Society ambayo kwa kuwa muwazi ilikuwa siyo Chama cha wanasheria, kilikuwa ni chama cha wanaharakati, na mapambano yao ilikuwa ni dhidi ya Serikali.” -Rais Samia Suluhu Hassan
Pia Rais Samia Suluhu ameonyesha nia ya kushirikiana na kila mtu mwenye nia ya kweli ya maendeleo.
"Kama unataka tufanye kazi vizuri come with clean hands, mine is clean. Come clean. Let's work together".-Rais Samia Suluhu