Daah mama yupo vizuri mno kwa kweli Mungu akulinde kwa kweli nilikua najiuliza Watanzania wenye moyo huu walienda wapi mpaka tukaangukia kwenye adhabu mbaya kabisa kuwahi kutokea kwenye Nchi pendwa ya Tanzania...
 
Imagine, cases kama hizi:

Nimemsikia mama akisema TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizowabambikia watu. Pigia mstari neno KUBAMBIKIA. Yani TAKUKURU wanakiri mbele ya Rais kuwa waliwabambikia watu kesi na wamekubali kuzifuta. Nimewaza sana kuhusu hao waliobambikiwa, familia zao, watoto wao na ndugu zao.

Nimemkumbuka rafiki yangu Abraham Ngoti ambaye TAKUKURU walimkamata huko Dodoma wakidai kuna kiasi kikubwa cha pesa kimeingizwa kwenye account yake. Akatakiwa kujieleza ni za nini? Wakamsafirisha usiku kama jambazi wakamleta Dar. Wakamuweka mahabusu yao kule Upanga.

Baada ya siku mbili TAKUKURU wakasema amejinyonga akiwa mahabusu. Familia haikukubaliana na taarifa hiyo kutokana na mazingira ya kukamatwa kwake hadi kufariki. Alijinyongaje mahabusu? Hakukua na ulinzi? Je inawezekana kujinyonga kwa kutumia suruali ya jeans? Inawezekana kujinyonga dirishani hadi kufa bila kujitetea kwa kushika nondo za dirisha? Inawezekana kujinyonga miguu ikiwa imegusa chini?

Maswali haya ndio yaliyofanya familia yake kuomba iundwe tume huru ifanye uchunguzi juu ya kifo cha ndugu yao. Lakini hakuna kilichofanyika. Waliambiwa maiti yenu hiyo hapo, mkazike.

Nimejaribu kuwaza hivi kama alibambikiziwa kesi kama hawa 147 anajisikiaje huko alipo. Kama wafu wanaona yanayoendelea duniani pengine anawalaani sana TAKUKURU.

Nampongeza mama kwa jitihada zake za kuibadilisha TAKUKURU. Nampongeza pia kwa kutoa maelekezo kwenye vyombo vingine kama Polisi na ofisi ya DPP. Lakini naomba atilie mkazo maelekezo hayo maana kuna wengi wamebambikiwa kesi na wanasota gerezani.

Mdude Nyagali anateseka rumande zaidi ya mwaka mmoja. Kila siku Jamhuri inaomba kesi isogezwe mbele kwa sababu ushahidi haujakamilika. Lakini ni Jamhuri hiyohiyo iliyosema imemkamata Mdude na kete za heroine nyumbani kwake. Kama kweli walimkamata na heroine ni ushahidi gani zaidi wanatafuta mwaka mzima?

Mazingira kama haya ndio yanafanya familia ya Mdude ihisi kwamba huenda kesi ya ndugu yao ni ya kubambikiziwa pia. Mama tafadhali ingilia kati. Taifa limepita kipindi kigumu sana wakati wa mwendazake, ni wakati sasa wa kuponya majeraha. We need truth and reconciliation.! MALISA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====

Rais Samia Suluhu: Kwenye suala la wingi wa mahabusu, labda niseme kwamba jana nikiapisha majaji nililigusia hili, uharakishwaji wa kesi na nimezitaka taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi ambalo uchunguzi unaanza kwenu kuharakisha chunguzi za kesi mbalimbali zilizopo ili kuharakisha kesi kusikilizwa na iadha kufutwa au mtu kuhukumiwa ipasavyo lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.

Niombe sana, nilizungumza hili na TAKUKURU, wameweza kufuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu, kwahiyo nanyi Jeshi la polisi jikagueni kama kuna za aina hiyo nazo zifutwe ili tupunguze wingi wa mahabusu kwenye majela yetu.

Ikiwa rais wa nchi ametamka hadharani kuwa kuna watu wako jela au mahabusu kwa kesi za kubambikiziwa, inaashiria kuwa anakubali kuwa jeshi la polisi na tikururu kumejaa askari wachafu mno, jee ana mpango gani wa kuwachukulia hatua waliowabambikizia wenzao kesi hizo? Pia ana mpango gani wa kulitakasa jeshi zima la polisi?
 
Kwakweli Samia suluhu amejifunza mambo mengi kupitia mapungufu ya mtangulizi wake. Hapendi kuendeleza mabaya. Tutarajie hata sheria kandamizi hapo mbeleni zitakuja kupelekwa Bungeni kwa marekebisho
Tangu mwanzo wa binadamu hakuna binadamu malaika na ndio maana kuna mamlaka zinatumia Sheria na Kanuni tuishi kwa amani. Binadamu wakwanza Adam na Hawa walidanganyika, itakuwa sisi kizazi chao.

Kwa msingi huo bila usimamizi wa karibu na wananchi kutii sheria bila shurti (kitendawili) maneno ya Rais SSH yenye kutia matumaini, hakuna shaka Tanzania itarudi kuwa shamba la bibi. Matokeo yake ni kujenga tabaka la wachache walio nacho.
 
Nimemsikia mama akisema TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizowabambikia watu. Pigia mstari neno KUBAMBIKIA. Yani TAKUKURU wanakiri mbele ya Rais kuwa waliwabambikia watu kesi na wamekubali kuzifuta. Nimewaza sana kuhusu hao waliobambikiwa, familia zao, watoto wao na ndugu zao.

Nimemkumbuka rafiki yangu Abraham Ngoti ambaye TAKUKURU walimkamata huko Dodoma wakidai kuna kiasi kikubwa cha pesa kimeingizwa kwenye account yake. Akatakiwa kujieleza ni za nini? Wakamsafirisha usiku kama jambazi wakamleta Dar. Wakamuweka mahabusu yao kule Upanga.

Baada ya siku mbili TAKUKURU wakasema amejinyonga akiwa mahabusu. Familia haikukubaliana na taarifa hiyo kutokana na mazingira ya kukamatwa kwake hadi kufariki. Alijinyongaje mahabusu? Hakukua na ulinzi? Je inawezekana kujinyonga kwa kutumia suruali ya jeans? Inawezekana kujinyonga dirishani hadi kufa bila kujitetea kwa kushika nondo za dirisha? Inawezekana kujinyonga miguu ikiwa imegusa chini?

Maswali haya ndio yaliyofanya familia yake kuomba iundwe tume huru ifanye uchunguzi juu ya kifo cha ndugu yao. Lakini hakuna kilichofanyika. Waliambiwa maiti yenu hiyo hapo, mkazike.

Nimejaribu kuwaza hivi kama alibambikiziwa kesi kama hawa 147 anajisikiaje huko alipo. Kama wafu wanaona yanayoendelea duniani pengine anawalaani sana TAKUKURU.

Nampongeza mama kwa jitihada zake za kuibadilisha TAKUKURU. Nampongeza pia kwa kutoa maelekezo kwenye vyombo vingine kama Polisi na ofisi ya DPP. Lakini naomba atilie mkazo maelekezo hayo maana kuna wengi wamebambikiwa kesi na wanasota gerezani.

Mdude Nyagali anateseka rumande zaidi ya mwaka mmoja. Kila siku Jamhuri inaomba kesi isogezwe mbele kwa sababu ushahidi haujakamilika. Lakini ni Jamhuri hiyohiyo iliyosema imemkamata Mdude na kete za heroine nyumbani kwake. Kama kweli walimkamata na heroine ni ushahidi gani zaidi wanatafuta mwaka mzima?

Mazingira kama haya ndio yanafanya familia ya Mdude ihisi kwamba huenda kesi ya ndugu yao ni ya kubambikiziwa pia. Mama tafadhali ingilia kati. Taifa limepita kipindi kigumu sana wakati wa mwendazake, ni wakati sasa wa kuponya majeraha. We need truth and reconciliation.!
 
Sio Takukuru au Polisi tu bali pia wao kwa wao wasioneane, yaani viongozi ktk taasisi zote za serikali waache tabia ya kuwaonea walio chini yao, waache tabia ya kuwabambikizia tuhuma zisizo za kweli kwa chuki binafsi.

huu sio utawala wa kiongozi kuwaonea walio chini.
 
Watanzania wengi wakishapewa kimadaraka fulani hata kama ni uchwara, kitu cha kwanza kinachowakaa kichwani ni kuwaharass watu wa chini yao, nahiyo kwao ndiyo uongozi. Watu wakilalamika kuonewa, hiyo kwao ndiyo utendaji uliotukuka, hawajui unaweza kuongoza watu kwa tabasamu kila mmoja akafurahi na mambo yakaenda vizuri.

cc chalamila, hapi na wengineo
 
Watanzania wengi wakishapewa kimadaraka fulani hata kama ni uchwara, kitu cha kwanza kinachowakaa kichwani ni kuwaharass watu wa chini yao, nahiyo kwao ndiyo uongozi. Watu wakilalamika kuonewa, hiyo kwao ndiyo utendaji uliotukuka, hawajui unaweza kuongoza watu kwa tabasamu kila mmoja akafurahi na mambo yakaenda vizuri

cc chalamila, hapi na wengineo
Ndiyo akili za akina Makonda
 
sio Takukuru au Polisi tu bali pia wao kwa wao wasioneane, yaani viongozi ktk taasisi zote za serikali waache tabia ya kuwaonea walio chini yao, waache tabia ya kuwabambikizia tuhuma zisizo za kweli kwa chuki binafsi.

huu sio utawala wa kiongozi kuwaonea walio chini.
Sure
 
Kiongozi wetu Amiri Jeshi Mkuu Mama samia amebaini vitendo vya ubambikizwaji wa kesi vinavyo fanywa na baadhi ya maafisa/vionhozi ktk taasisi za TAKUKURU na POLISI lkn pia inawezekana kabisa pia na taasisi/idara zingine za serikali zinatabia ya kuwaonea na kuwabambikizia tuhuma watumishi walio chini yao.

ni vyema Waziri wa Utumishi wa umma Mhe. Mchengelwa akafuatilia na kuchinguza kuna uonevu mkubwa unao fanywa na viongozi dhidi ya watumishi wao walio chini na hakuna wa kuwa tetea, uonevu huo unafanywa kwa chuki binafsi, kuna watu wanalia na wananyanyasika kisa tu hana mkubwa wa kumtetea n.k
 
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====

Rais Samia Suluhu: Kwenye suala la wingi wa mahabusu, labda niseme kwamba jana nikiapisha majaji nililigusia hili, uharakishwaji wa kesi na nimezitaka taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi ambalo uchunguzi unaanza kwenu kuharakisha chunguzi za kesi mbalimbali zilizopo ili kuharakisha kesi kusikilizwa na iadha kufutwa au mtu kuhukumiwa ipasavyo lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.

Niombe sana, nilizungumza hili na TAKUKURU, wameweza kufuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu, kwahiyo nanyi Jeshi la polisi jikagueni kama kuna za aina hiyo nazo zifutwe ili tupunguze wingi wa mahabusu kwenye majela yetu.

DAMU NA VILIO VYA WALIO BAMBIKIWA IWAFUATE WATOTO WAO NA VIZAZI VYAO VINNE.
 
NIMEUTAFUTA NA KUUPANDISHA WAKUU ,
Je Mama yetu mpendwa anayaishi maneno yake?
 
Je watuhumiwa wamedai au kulipwa fidia?!
 
Back
Top Bottom