kookolikoo

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
2,690
2,000
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====Rais Samia Suluhu: Kwenye suala la wingi wa mahabusu, labda niseme kwamba jana nikiapisha majaji nililigusia hili, uharakishwaji wa kesi na nimezitaka taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi ambalo uchunguzi unaanza kwenu kuharakisha chunguzi za kesi mbalimbali zilizopo ili kuharakisha kesi kusikilizwa na iadha kufutwa au mtu kuhukumiwa ipasavyo lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.

Niombe sana, nilizungumza hili na TAKUKURU, wameweza kufuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu, kwahiyo nanyi Jeshi la polisi jikagueni kama kuna za aina hiyo nazo zifutwe ili tupunguze wingi wa mahabusu kwenye majela yetu.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,360
2,000
Leo katika hafla ya juwaapisha majaji wapya Mh Rais Samia Suluhu Hasani amewataka jeshi la polisi, ofisi ya mwendesha mashtaka na Mahakama kuhakikisha wanaharakisha michakato ya kesi mbali mbali ili kutoa haki wa watuhumiwa badala ya kuchelewesha haki za watu.

Hili linakuja ikiwa ni kiasi cha mwezi mmoja tu ambapo Tito Magoti afisa ktk Shirika ka haki za binadamu HRLC alitoa siri na kuelezea kadhia wanazopata watuhumiwa wa kesi mbali mbali huku barua hiyo ikielekezwa kwa Mh Rais.m
 
Last edited:

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
505
1,000
Didhani Kama Kuna umuhimu wa kuwa na TAASISI YA KUPAMBANA NA RUSHWA TANZANIA. Tunapaswa kuwa na mkuu wa nchi ambaye ndiye atasimama nafasi ya mapambano dhidi ya Rushwa.

Kwa ripoti za TAKUKURU wanazotoaga kwa viongozi wa nchi ukilonganisha na Hali ilovyo Bora tufute chombo hiki kinachonyanyasa watu nakuunda mamlaka nyingine yenye nidhamu.
 

Kwisense

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
430
1,000
Mama ana matamanio fulani lakini mifumo yetu imekaa kibabe, kibaguzi na mingi haifuati sheria na katiba ya nchi. Kuna watu wana roho mbaya sana nchi hii, wanateswa wenzao kwa sababu ya kutofautiana vitu vidogo sana hasa upande wa siasa. Ili watu wetu wapate haki na fikra huru inatakiwa tupate katiba mpya na kubadilisha upatikanaji wa Jaji mkuu, Spika wa bunge, majaji, wakuu wa taasisi i.e takukuru, police, etc na pia kubadilisha mfumo wa usalama wa taifa ili wawe kwa maslahi ya nchi na siyo chama
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,660
2,000
Leo katika hafla ya juwaapisha majaji wapya Mh Rais Samia Suluhu Hasani amewataka jeshi la polisi, ofisi ya mwendesha mashtaka na Mahakama kuhakikisha wanaharakisha michakato ya kesi mbali mbali ili kutoa haki wa watuhumiwa badala ya kuchelewesha haki za watu.

Hili linakuja ikiwa ni kiasi cha mwezi mmoja tu ambapo Tito Magoti afisa ktk Shirika ka haki za binadamu HRLC alitoa siri na kuelezea kadhia wanazopata watuhumiwa wa kesi mbali mbali huku barua hiyo ikielekezwa kwa Mh Rais. View attachment 1789532 m View attachment 1789532
Hoja si kuongea nao, hiyo ni hisani. Swala ni kufutwa kwa sheria zilizotumika (kama zipo), au kuwachukulia hatua waliotumia madaraka yao vibaya.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,038
2,000
Kwakweli Samia suluhu amejifunza mambo mengi kupitia mapungufu ya mtangulizi wake. Hapendi kuendeleza mabaya. Tutarajie hata sheria kandamizi hapo mbeleni zitakuja kupelekwa Bungeni kwa marekebisho
Huoni hata leo IGP kajikakamua kusema mapato ya usalama barabarani yamepungua kwa vile watu hawafanyi makosa tena. Akidhani ni ujiko kukusanya fine za barabarani. Mh. Rais kamzodoa kwamba wasitegemee fine kama chanzo cha mapato. Bali watoe elimu watu wasifanye makosa.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,360
2,000
Huoni hata leo IGP kajikakamua kusema mapato ya usalama barabarani yamepungua kwa vile watu hawafanyi makosa tena. Akidhani ni ujiko kukusanya fine za barabarani. Mh. Rais kamzodoa kwamba wasitegemee fine kama chanzo cha mapato. Bali watoe elimu watu wasifanye makosa.
Nchi ikikosa Rais mzuri mifumo yote inakuwa ya kishetani. Akina Igp siro leo wanafanya kazi kwa uhuru kwa mujibu wa sheria za nchi. Wametukosea sana kwa kushiriki maovu na vitendo vibaya wakati wa Ibilisi Jiwe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom