Rais Samia tafadhali acha kumnanga kila mara kimafumbo Hayati Dkt. Magufuli

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
"Tunasifiwa kwamba adjustment tulizozifanya awamu ya Tano kidogo zimekuza heshima ndani ya social service, heshima iliyokuzwa ni heshima ya uwoga, kwa sababu kulikuwa na simba wa yuda, ambaye alikuwa ukimgusa sharubu anakurarua...heshima inayotakiwa iwe ya moyoni".Rais Samia.

Chanzo: ITV Tanzania

Nami GENTAMYCINE nasema huu muda mwingi ambao unautumia Kumnanga tena Kimafumbo aliyekuwa Boss wako Rais Hayati Rais Dkt. Magufuli ungeutumia katika Kutatua Changamoto nyingi za Kijamii zinazowakabili Watanzania kwa sasa ningekuona wa maana na una Tija hapo Ikulu.

Sasa kama kumbe ulikuwa ukiyajua yote haya kwamba Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa sijui ni Yuda au Simba Mraruaji kwanini ulifanya nae Kazi muda wote ule na hukutaka Kujiuzuru ili umuachie nchi Mwenyewe au amteue mbadala wako?

Marais wote waliokutangulia walipoingia Madarakani walikuta kuna Changamoto nyingi zilizoachwa na Watangulizi Wao zingine ni za Kibinadamu na zingine ni za Asili / Kimazingira je, uliwahi kuwaskia akina Mzee Mwinyi au Mkapa au Kikwete au hata Mtangulizi wako Hayati Rais Dkt. Magufuli wakiwasema Watangulizi wao 'Kimafumbo' kuwa walikuwa na Uongozi / Utawala mbaya?

Tafadhali Rais Samia Watanzania tunaojitambua Kifikra ( Kichwani ) na Kimaono si tu hatupendi bali sasa tunaanza Kuchoshwa na 'Mipasho' yako isiyokuwa na Tija hasa kwa 'Kumnanga' Kwako Hayati Rais Dkt. Magufuli na tunakuomba uachane na hii tabia kwani kama unadhani inakujenga basi Mimi GENTAMYCINE nakuambia kuwa inakuharibia, inakufanya Udharaulike na haina Afya ya Kiutawala na Kiuongozi sana sana utaanza kutengeneza Chuki na Mgawanyiko usio wa maana ndani ya Jamii ya Watanzania.

GENTAMYCINE nakiri hapa kuwa kama Binadamu ( Mwanadamu ) Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa na Mapungufu yake kama ambavyo hata akina Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete nao walikuwa nayo ila si busara na hekima kuanza 'Mipasho' ya Kizanzibari dhidi ya Watangulizi wako tena ukimlenga hasa Hayati Rais Dkt. Magufuli na Kuwaacha wengine ambao tena ndiyo Waliiharibu zaidi Tanzania yetu hii wakiongozwa na huyo Mstaafu na Mshauri wako Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Huna hata miaka Miwili ( Madarakani ) umeanza kuwa na 'Majungu' na 'Mipasho' kwa Mtangulizi wako je, ukikaa miaka Minne itakuwaje? Hayati Rais Dkt. Magufuli amekukosea nini Rais Samia? Kwa hiki ukifanyacho Kwake ( tena akiwa amepumzika ) Kaburini Kwake Chato tukikuita Wewe ni 'Mnafiki' na ulikuwa humpendi ulipokuwa nae na pengine hata Kifo chake ulikifurahia na labda hata kukifanyia Sherehe Chumbani au Sebuleni Kwako tutakuwa tunakosea / tunakukosea?

Namalizia tu kwa kukuambia kuwa kama kuna Watu ambao GENTAMYCINE sioni Uwoga kuwaita Wapumbavu ( Mapopoma ) ndiyo Wanakushauri uwe Unamnanga kwa Mipasho yako aliyekuwa Boss wako na Rais Hayati Dkt. Magufuli basi jua ya kwamba Wanakuharibia na wanakusababishia upate Laana yake ambayo huenda ipo Siku itakuharibia.

Na kwa Kitendo tu cha Yeye kukuteua Wewe uwe Mgombea Mwenza wake na kuja kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania ( Kitu ambacho nina uhakika hukukitegemea ) leo Wewe hukupaswa kuwa ndiyo Kinara wa Kumsema ( Kumnanga ) vibaya tena Kimipasho Hayati Rais Dkt. Magufuli wakati mlikuwa Wote Serikalini na mara kwa mara hata ulipokuwa ukiongea katika Hafla mbalimbali za Ikulu Kipindi chake ulikuwa Ukikiri kuwa Maamuzi mengi mlikuwa mkiyafanya pamoja sasa iweje leo Kafa ( Kafariki ) unamgeuka? Hii ni Dhambi kubwa mno ya 'Unafiki' ambayo hata Mwenyezi Mungu haitaki hivyo nakushauri achana nayo tafadhali.

Kwangu Mimi GENTAMYCINE Kiongozi / Mtawala mzuri ni yule ambaye akikuta Mtangulizi wake ameharibu ( amekosea ) basi analibeba Yeye kama Yeye tena Kimya Kimya kwa Kulisahihisha kwa Kuliboresha, anasamehe, anaomba Radhi ikibidi kwa Mapungufu hayo na anasonga mbele kwa Yeye pia Kuboresha ili kutengeneza 'Legacy' yake lakini siyo kupoteza muda Kumnanga kwa Mipasho ili kutafuta Sifa za Kipumbavu kwa Watu ( Wananchi ) ukidhani ndiyo utapendwa nao na kuonekana ni maana Kwao wakati huenda Mioyoni mwao na Rohoni kwao ukawa Umeshadharaulika na unaonekana tu Kituko na pengine hata Mtu wa hovyo hovyo ambaye haufai.

Huwa sina Uvumilivu kwenye Upuuzi.

R.I.P Hayati Rais wetu Dkt. Magufuli.
 
HUYU MAMA MNAFIKI SANA, KAMA MAGU ALIKUWA ANAKOSEA YEYE AMA ANGEMSEMA WAKATI ULE AMA ANGEJIVUA CHEO CHAKE KUONESHA HAKUWA SAWA NA MAAMUZI YA MAGU
Hakika Mkuu hata Mimi nimeshangaa, nimesikitika na nimeumia pia kwani anachokifanya sasa ni 'Unafiki' na kutaka Kutuaminisha Watanzania kuwa Hayati Rais Dkt. Magufuli alikuwa ni Mtu Mbaya na kwanba Yeye ndiyo Mtu mzuri wakati hata hivi anatuongoza lakini bado anatembelea Nyota ya yale mazuri na mema yote aliyoyafanya aliyekuwa 'Boss' wake Hayati Rais Dkt. Magufuli.

Hii tabia itamharibia na aiache tu upesi.
 
Unatuboa Sana we mama simamia lako tu siyo kukaa una mnanga shujaa wetu magufuli ili kujijengea credibility kwa watanzania, speech zako nyingi za kukaa un mnanga shujaa wetu magufuli ili kujiinua inua ziache ,yaani tunakosa mvuto was kufuatilia speech zako na kuzitilia maanani maana my wetu tuliye mpenda kila saa kumnanga utadhani wewe umetokea sayari ya ndani ya chupa ambayo haikuwemo awamu ya tano unatuboa tunampenda magufuli wewe simamia lako Kama uko vizuri si na wewe tutakuona ??? Lakini siyo kila saaa magufuli sijui Nini,fanya lako nawewe tukupende,ila siyo hayo eti kufoka foka,sijui Simba wa yuda sijui Nini,wewe piga kazi zako zionekane ili tu kujudge , magufuli Ali inculcate vitu vingi vizuri mioyoni mwetu kwako hatuvioni,Ni vya kumulika kwa tochi ndo vionekane
 
Back
Top Bottom