Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Jana Usiku nilipokea Meseji moja kutoka kwa Rafiki mkubwa kutoka Uganda akielezea Kufurahishwa Kwake na 'Kiingereza ' kizuri alichonacho Rais wa Tanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.

"Mr. Generalist are you sure that this President of yours Mama Samia she's not a Briton? She speaks fluent English, very articulate, attractive and comfortable with it unlike other so called intellectuals with their doctorates on hand "

Na Waganda hawakuishia hapa tu kwa huyu Rafiki yangu Kunitumia hiyo Meseji bali hata ukienda huko Ugandans On Twitter ( UOT ) Wachangiaji wengi wamevutiwa na Uwezo mkubwa wa Kuongea Kiingereza ' kilichonyooka ' cha Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Wameenda mbali zaidi na Kuhoji inakuwa Marais wengine (hasa Barani Afrika) wana Elimu Kubwa lakini walipokuwa wakiwasikiliza (wanapowasikiliza) huwa wanaongea Viingereza 'vibovu vibovu' tu wakati Makabatini mwao wamehifadhi Vyeti vya ' PhD ' zao.

Kongole sana Kwako Rais Mama Samia.
 
Wameenda mbali zaidi na Kuhoji inakuwa Marais wengine ( hasa Barani Afrika ) wana Elimu Kubwa lakini walipokuwa wakiwasikiliza ( wanapowasikiliza ) huwa wanaongea Viingereza ' vibovu vibovu ' tu wakati Makabatini mwao wamehifadhi Vyeti vya ' PhD ' zao.

Kongole sana Kwako Rais Mama Samia.
Siyo wote wanaoongea Kiingereza wana elimu mkuu,Kiingereza ni lugha na wala siyo elimu.

Ukisema English ni Elimu utaonekana huna elimu

Kuna Warusi, Wataliano, Wafaransa hawazungumzi Kiingereza sio kwamba hawana elimu...KIINGEREZA NI LUGHA
 
Bado tunasafari ndefu kama nchi.
Yaani mtu kuzungumza Kingereza kizuri nalo ni swala la kujisifia?

Ningeshangaa sana kama Uzi huu usingevamiwa na wasiokijua ' Kiingereza ' na najua mtajitokeza wengi tu.

Ninachojua tu ni kwamba duniani kuna Lugha nyingi na nzuri ila hakuna ambayo hadi hivi leo imeweza kuwa ni Kiungo ' Kikuu ' cha Mataifa yote duniani iwe Kiuchumi na hata Kidiplomasia kama cha Kiingereza.

Kama Mchina, Mrusi, Mjerumani na Mchina pamoja na Jeuri zao zote za kuwa ' Super Powers ' ulimwenguni na Lugha zao pia ni Kubwa lakini bado hao hao wanakizungumza Kiingereza Wewe Mpuuzi Mmoja wa Kiswahili usiye na mbele wala nyuma ni nani ukipinge?

Itatuchukua muda mrefu sana na huenda pia hata isitokee kwa Mataifa mengi duniani Kuachana na Lugha ya Kiingereza kwani kama kuna Mafanikio makubwa ambayo nchi ya Uingereza ilipata tokea Kipindi cha ' Colonialism ' ni kuhakikisha Lugha yao si tu inaendelea kutumika bali pia inapendwa na kuendelea Kuaminiwa na Vizazi na Vizazi.

Kama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere pamoja na kutowakubali Wazungu ( hasa kwa Sera zao na Matendo yao kwa Waafrika ) lakini Mwenyewe kwa Mdomo wake (na Clips zipo Mitandaoni) alikiri kuwa Kiingereza ni Lugha muhimu, siyo ya Kuepukwa duniani na ya Kibiashara zaidi.
 
Back
Top Bottom