Rais Samia Suluhu umeanza vizuri mno, ukitimiza haya hakika enzi yako haitasahaulika

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
MAMA SAMIA SULUHU UMEANZA VIZURI MNO, UKITIMIZA HAYA HAKIKA ENZI YAKO HAITASAHAULIKA

Na Emmanuel Kasomi

Kila mtu ni yeye, ameumbwa kwa fikra na vipawa tofauti kabisa na hakuna kama yeye Duniani pote.

Wapo wanaomtaka Rais SAMIA SULUHU kuwa kopi ya Mtangulizi wake na wapo wanaomwambia awe Hivi ama vile, kalamu ya Mwana wa Lufunga, kwa kuamini kuwa huyu ni SAMIA na si mwingine yeyote, inabainisha mambo makuu yatakayomfanya Mwana Mama huyu kuibuka nguli wa Afrika na Kuandika historia itakayobaki alama kuu katika historia za awamu za uongozi wa nchi yetu nayo ni haya;

1. KUPITIA UPYA SEKTA YA AJIRA.
Wasomi wapya wanalia, vijana vyuoni hawana natumaini na serikali yao kuhusu upatikanaji wa Ajira rasmi, mashirika yamejaza watu wanaofanya kazi za vibarua miaka mingi bila kupata Ajira rasmi zakuwanufaisha na kuongezea serikali walipa kodi, hakika hali ya Ajira ni mbaya bin taabani

Kibaha zaidi ni kwamba, wakati serikali inapambana kudhamini masomo ya vyuo na kuondoa ada ya sekondari BADO wasomi hawa hawawawekewi misingi bora ya kujikimu baada ya masomo na kuweza kurejesha pesa za umma MAPEMA wakati huohuo ikiwa walimu, madaktari, wahandisi hata wataalam mbalimbali wamejaa mtaani bila Ajira BADO SEKTA nyingi zikiwemo za umma na binasfi zinao uhaba mkubwa wa watu haohao.

Rais SAMIA SULUHU akiangalia suala hili, SEKTA za umma na binasfi ziwe na utaratibu maalumu kuwaajiri watu kwa muda fulani badala ya kuwafanya wengine kuwa vibarua wa maisha, mfumo wa kuwezesha vijana wahitimu kusimama na kujitegemea na kuanza kurejesha mkopo wao na kumaliza tatizo la uhaba wa watumishi ambao wapo mtaani ataandika legasi kubwa Sana

2. KUUNGANISHA JAMII YA WATANZANIA.
Ni KWELI wapo wanalia na wengine wanashangilia wakati madai yao wanaolia yanatatulika.

Sitofahamu za kisiasa, dhoruba za uchaguzi, mifumo ya uratibu wa haki ya uchaguzi kwa raia na taasisi za kisiasa na sheria kuu za nchi kwa maana ya tume ya uchaguzi, katiba ya nchi, kero za Muungano na mengi ya aina hii.

Hapa Rais SAMIA SULUHU akiangalia vema, akawaita Ikulu ama ukumbi utakaopendekezwa wanasiasa wa vyama vyote, tawala, wapinzani na asasi za kiraia wakiwemo wawakilishi wa taasisi za dini Ili kujadili kitakachoitwa Maridhiano ya Mustakhabali wa Umoja wa taifa, akaongoza mabadiliko ya katiba na kuundwa kwa mfumo mpya wa tume ya uchaguzi ikiwemo kuruhusu mgombea binasfi, hakika ataandika legasi kubwa Sana ambayo hatasahauliwa nayo milele

3. KUJENGA NGUVU YA TAASISI DHIDI YA NGUVU YA BINADAMU.
Kwa muda, jamii yetu inaongozwa kwa utashi wa walio na mamlaka na si malengo na dira ya taasisi husika.

Bunge halina meno ila matakwa ya anayeongoza Bunge ndiyo zaidi licha ya kuwa na wabunge bora na wasio bora, Leo hata chama cha siasa kimtoe mwakilishi wake bungeni kama spika anamanufaa na mbunge huyo ataendelea kuula tu, Mahakama na serikali vilevile uhusiano wake si mzuri Sana kwani Mtazamo wa aliyeko juu ndio umekuwa ukiamuru mifumo iweje. Huu ni ukosefu wa dira ya jamii bali nguvu ya mtu.

Hapa Rais SAMIA SULUHU akiangalia vema na kuzitaka taasisi kufanya kazi kwa weledi, kuwa na sera zake zenye dira na matarajio yaliyo wazi basi ataandika legasi kubwa Sana ambayo hatasahauliwa nayo.

4. KUANGALIA MFUMO WA ELIMU, UPYA.
Elimu yetu unalalamikiwa kila leo, mitaala kutokuendana na wakati, malengo ya elimu kutokuvaa uhalisia wa mahitaji ya wanaoipata elimu yetu, mjadala wa lugha nk.

Hili, Rais SAMIA SULUHU akiangalia vema akawaita wadau, wakaanza na muda wa kuisaka elimu kama miaka 7 ya primari, 4 ya seko, 2 kidato cha 5 &6 hadi taaluma za vyuoni.

Na zaidi uwekwe ufafanuzi juu ya kufeli na kufaulu kwa elimu ya sekondari, Hadi leo mtu mwenye faraja la IV hadi daraja la 1 huhesabiwa amefaulu lakini cha ajabu watoto wanaoangukia daraja la 1V wameendelea kuungana na wanaopata daraja la 0 yaani wote huonekana kama waliofeli tu kwakuwa serikali haina biashara nao tena ispokuwa wenye sifa za kwenda kidato cha tano ndio bado huendelea kupangiwa shule na mifumo ya elimu. Hapa Rais SAMIA SULUHU anaweza kutumia wadau kushauriana basi hawa wenye 1V nao wakapangiwa vyuo ama mafunzo mbalimbali kama ambavyo watakuwa wamachagua katika fomu zao baada ya kuhitimu sekondari

5. KUIMARISHA ULINZI WA NDANI NA NJE YA NCHI.
Licha ya uzuri wa serikali iliyopita, ulinzi ulijisahau kidogo hasa ndani ya nchi kwani serikali ilichafuliwa na kilichoitwa "watu wasiojulikana" ambao waliteka watu maeneo mbalimbali ya nchi, watu walitwangwa Risasi hadharani mchana kweupe (LISSU), vitisho Hivi vilitia doa serikali na hata mawaziri wa mambo ya ndani kubadilishwa mara kadhaa Ili kukabili janga hili, Mama Samia Suluhu akidhibiti vema haya, amani, haki na furaha kwa wote hakika legasi yake haitafutika.

Yapo mengi, yakiwemo kujirishisha na teuzi zake kabla Ili asijetoa aliyesahihi akaweka asiyesahihi, kudhibiti mianya ya rushwa na ufisadi, kukabiliana na mitego ya mabeberu dhidi yetu, hakika Mama Suluhu SAMIA SULUHU utaandika wino katika Mwamba wa Jiwe litakalodumu milele na ndivyo kalamu ya Mwana wa Lufunga inaishiwa wino nikikutakia Uongozi mwema uliotukuka kwani umeanza vyema na uko katika njia inayotia matumaini;✍️

Instead of being photocopy of someone's character, build your own empire.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Wafuasi wa magufuli mpaka muda huu hata hawaelewi kilichotokea! Yaani kutoka kwenye kampeni ya kumuongezea malaika wao miaka ya kutawala nchi!

Mpaka kutakiwa kumkubali Rais mpya, na ambaye hawakumtarajia kabisa katika maisha yao! Yaani waliamini magufuli was the next PK and Mu 7!!

Mataga, where are you crying? 🥵
 
Nyie watu mna dhambi kweli mumemlia jambazi Sabaya fedha ili mumsafishe mumekutana na resistance kubwa mpaka mnabadilisha route sasa. Mama hadanganyiki Sukuma Gang wote mumeshajulikana na nia yenu ovu.
 
Nyie watu mna dhambi kweli mumemlia jambazi Sabaya fedha ili mumsafishe mumekutana na resistance kubwa mpaka mnabadilisha route sasa. Mama hadanganyiki Sukuma Gang wote mumeshajulikana na nia yenu ovu.
Haya bana mkuu.
From now nitakuwa Sabaya au Mchengerwa
 
Wafuasi wa magufuli mpaka muda huu hata hawaelewi kilichotokea! Yaani kutoka kwenye kampeni ya kumuongezea malaika wao miaka ya kutawala nchi!

Mpaka kutakiwa kumkubali Rais mpya, na ambaye hawakumtarajia kabisa katika maisha yao! Yaani waliamini magufuli was the next PK and Mu 7!!

Mataga, where are you crying? 🥵
😂😂😂
 
Huwezi amini SijaelewA etii🤣🤣,nahisi hujazungumzia maslahi ya watumishi wa umma ambayo JOPOMA aliyapuuzia!
 
Eti hawa ndio vijana wa Tanzania, ambao full vigeugeu na wananunulika kirahisi kuliko hata Malaya wanaojiuza. Hata hajui wasimamie nini, wapo kunusanusa kama Mbwa wapi watapata nyama na kuanza kumlamba miguu magawa nyama. Labda Vijana(sio hawa) ni Taifa la Kesho Kutwa.
 
Watu wa kanda ya mwendazake wamejazwa mno kila sekta wapunguzwe ni hatari inachochea ukabila.
 
Eti hawa ndio vijana wa Tanzania, ambao full vigeugeu na wananunulika kirahisi kuliko hata Malaya wanaojiuza. Hata hajui wasimamie nini, wapo kunusanusa kama Mbwa wapi watapata nyama na kuanza kumlamba miguu magawa nyama. Labda Vijana(sio hawa) ni Taifa la Kesho Kutwa.
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom