Rais Samia Suluhu umeanza vizuri lakini naomba uyafanyie kazi mambo kumi

Jan 28, 2020
86
125
Amani ya M/mungu iwe nanyi waungwana wa jamii forum.
Kwanza naomba kudeclare interest mimi naamini maendeleo ya mahala popote yanaletwa iwapo kutakuwa na mawzo mbadala/upinzani,hivyo hata nchi yetu Tanzania ili iweze kusonga mbele ni lazima kuwepo na mawazo mbadala au upinzani.

Sasa naomba niende kwenye mada, ni kwamba kwa namna mama etu Samia Suluhu Hassan alivoanza uongozi wake ameleta matumaini kwa watanzania kiasi kwamba naona hata zile tofauti zetu kama wananchi zimepungua na sote kwa kiasi kikubwa tuko nae mama etu katika juhudi za kulijenga taifa letu.Hata hivyo napenda nimshauri yafuatayo (nyuma ya key board) ili mambo yawe mazuri zaidi:-

1.USIWACHUKULIE WAPINZANI WAKE/VYAMA MBADALA KAMA MAADUI WA SERIKALI YAKE
Miongoni mwa sababu zilizomuharibia JPM ni pamoja na kuamini kuwa vyama vya upinzani ni maadui katika harakati za maendeleo ya Tanzania.Na hapa ndipo palileta hali ya watu kubaki na sumu au vinyongo kiasi kwamba hata kulipotokea matukio mabaya dhidi ya serikali badala ya kuchukia walikuwa wanafurahia.Mama kupitia hotuba yako ya mwanzo ulionesha maridhiano ya kitaifa kama ajenda yako muhimu hivyo nakuomba ulizingatie hili na ukiona wasaidizi wako hawapendi wafukuze mara moja(una power ya kufanya hivyo).


2.WAPE WATU UHURU WA KUZUNGUMZA NA KUKOSOA SERIKALI YAKO
Mama naamini umepitia madrasa ambako tunafundishwa kuwa miongoni mwa njia za kuondosha uovu ni pamoja na kuzungumza kwa maana iwapo mmoja wetu ataona tatizo (munkari) basi akataze au akosoe kadri iwezekanavyo.Mbali ya huko madrasa tu hata katika maisha yetu ya kawaida ukikosoa kwenye tatizo utakuwa umemsaidia mwenye makosa kisha atajirekebisha,hivyo serikali yako isione haya kukosolewa ndo sehemu ya maisha mama.Assurance inafanywa na third party kwa hiyo nakuomba uache watu waone madhaifu ya serikali yako na wakizungumza utajua lipi la kurekebisha,kuliacha au kuboresha.

3.WAPE WATU HAKI ZAO KWA MUJIBU WA KATIBA NA SHERIA
Naamini kuna baadhi ya maamuzi yalifanywa na serikali ambayo wewe mama ulikuwa makamu wa rais hukuyapenda kwa sababu yalikiuka katiba na sheria za nchi yetu lakini hukuwa na jinsi ya kufanya kwa sababu mtu wa mwisho alikuwa mwendazake.Lakini kwa sasa wewe ni mwenye mandate ya maamuzi ya kitaifa kwa hiyo nakuomba zingatia matakwa ya kikatiba na nchi yetu itakuwa salama zaidi.Mfano tarehe 01/05 mwaka huu natarajia utazingatia takwa la kisheria kwa watumishi wako wa umma kwa kuwaongezea mishahara na kuwapandisha madaraja.

4.EPUKA KUJIONA WEWE NI BORA KULIKO WENGINE.
Tunafundishwa(kwa sisi waislamu na samahani kama nitaeleweka vibaya kwa kutaja uislamu) kuwa mwenye kujishusha basi M/Mungu humpandisha.Kwa hiyo na wewe mama nakuomba usijikweze na kudharau wenzako kwa mfano viongozi wastaafu hawa ni watu muhimu sana kwani wana exposure kuhusu maswala mbalimbali ya kiuongozi.Hapa nakuomba urejee maneno ya JK siku ya mazishi ya JPM.Wasikilize halafu za kuambiwa changanya na zako ufanye uamuzi.

5.MAMA PENDA SANA WANANCHI WAKO KWA MATENDO NA SIYO MANENO
Mama wapende watanzania kwa dhati na siyo propaganda na uwaepuke watu wabaya ambao huzalisha chuki kwa watu na kuwachonganisha wenzao (mfano DAR DAB Somalia na yule mmiliki wa vikaratasi vya kufungia mandazi ya mama lishe dah samahani kama nimekwaza mtu hapa),Wape maneno yenye faraja kwenye shida,waondoshee dhiki ya kimaisha kadri uwezavyo na uwalinde bila kujali tofauti zao kisiasa,dini na maeneo.

6.JITAHIDI SERIKALI YAKO IAJIRI WAFANYAKAZI WAPYA KADRI IWEZEKANAVYO
Ajira ni sehemu ya kuhakikisha watanzania wanapata mkate wao wa siku hivyo nakuomba mama serikali yako iajiri ama iweke mazingira wezeshi ya kupata ajira kwa kuipa nguvu sekta binafsi ambapo ni rahisi zaidi kuajiri watu wengi kuliko ajira za serikali.
Mama hapa nakutahadharisha usisubiri sana kwa dhana ya kwamba utaajiri kesho,kesho na kesho yawezekana hata mwendazake alitamani aajiri lakini labda alikuwa anasubiria kesho mwishowe hakuipata kesho yake.Linalowezekana ulilisubirie kesho na wewe mwenyewe ulisema zege hailali au siyo mama!


7.EPUKA UBABE NA KAULI ZA HOVYO
Mama mtangulizi wako alicheza vibaya sana eneo hili na ni miongoni mwa sababu baadhi ya wananchi kufurahia mabaya kwa serikali yao hivyo nakuomba uwe na hekima mama etu.Achana na yale maneno ya "mimi sijaleta tetemeko la udongo'kwani maneno haya hayatakiwi kuzumzwa na kiongozi tena wa juu kama ulivyo wewe. Kuwa rahima mama utapendwa na wananchi na Tanzania itarudisha nuru yake iliyopotea kwa miaka mitano nyuma.

8.IKIKUPENDEZA FIKIRIA ZAIDI KUHUSU KATIBA MPYA
Japo nimetumia neno ikikupendeza lakini hili jambo ni la msingi mno kwa ajili ya kuweka mifumo imara katika nchi yetu.Kwa kuzingatia kuwa na wewe mama ulikuwa miongoni mwa viongozi wakati wa mchakato wa kuandaa katiba iliyopotezewa nakuomba usihofu na usione aibu kuliendeleza jambo hili.Maana utaisaidia nchi yetu dhidi ya viongozi walafi,wahafidhina na wababe (japo yawezekana hata katiba mpya ikiwepo wapo watu ambao wanaweza wasiiheshimu) lakini timiza wajibu wako iwekee kipaumbele hao watu wakitokea na kutoiheshimu katiba M/Mungu atafanya jambo lake.

9.USIIPUUZE MITANDAO YA KIJAMII HUSUSANI JAMII FORUM
Hapa mama kuna malegendary na wasomi wakutosha katika kukosoa,kukuhabarisha,kukushauri n.k.Japo nyuma ya key board lakini utapata mambo mengi ya msingi ambayo yanaweza kukusaidia katika uongozi wako.Epuka kutamani malaika waje waizime mitandao kwa sababu tupo katika (SOFT WORLD) ambako mitandao ndo wakati wake.Ukiizima tutakuwa gizani wewe na sisi wananchi wa kawaida kwa hiyo ngoma itakuwa draw wote tutapasa ili kuona kitanda,chakula na vingine.

10.MTANGULIZE M/MUNGU
Haya yote ili uweze kufanikiwa huna budi kumtanguliza Mungu kwa Kumuomba na kuwa mnyenyekevu kwake.Mtangulize M/mungu kweli kweli na yasiwe maneno tu mama etu. Muombe yeye akupe hekima na busara ya kuongoza taifa kubwa lenye watu,tamaduni na makabila tofauti.Kumbuka iwapo utamtanguliza M/Mungu atakufanyia wepesi katika harakati ya kutuongoza.

HITIMISO.
Mama nimekushauri hayo mambo kumi ya kuyafanya katika serikali yako, hata hivyo simaanishi kila kitu uwe hewallah.Wewe ni Amiri Jeshi Mkuu kuna wakati kama kiongozi unatakiwa uwe strong ( but WATCH OUT NOT TO THAT EXTENT 😂😂😂) hata hivyo usiumize watu pasi na hatia.Jitahidi kuzingatia mipaka yetu inakuwa salama,kama kuna chawa wenye kujipendekeza kwako ili wapate uteuzi achana nao maana hawapo kwa ajili ya maslahi yetu sisi Watanzania.

KAMA IKIKUPENDEZA MAMA WALE COVID -19 waondoke pale bungeni maana hawawakilishi chama chochote hivyo wanalihujumu taifa letu.Natamani sana pesa ambazo wanalipwa bora zingetumika kwa mambo mengine ya msingi maana uwepo wao pale ni kinyume na katiba ya JMT ambayo umeapa utailinda,kuifuata na kuiheshimu.
Mama hii ni lugha ya mama na mwanae kama nimenena vibaya naomba unisamehe mama angu lakini nimekuandikia kwa sababu sina access ya kuonana na wewe mama.

Masalam wako katika ujenzi wa Tanzania mpya.

Doctor Ngariba.
 

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,330
2,000
  • Mlishauri serikali inunue ndege leo mnaiponda serikali hiyo hiyo kwa kununua ndege
  • Mlishauri serikali iwanyime motisha ya msamaha wa kodi wawekezaji sasa nyiye ndiyo mnailaumu serikali kwa uwekezejai kudorora
  • mliishauri CCM imuache Lowassa kuwa ni nani sijui nyinyi mkampa ugombea urais
  • tuliposema tutaishida corona kwa kumtegemea Mungu + tiba asilia + tiba za kisasa isipokuwa lockdown nyie mlisema Mungu si kitu barakoa inatosha na ikwekwa lockdown tumepona
nk n k
Mama Samia wasikie tu usiwasikilize
 

Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,370
2,000
Kwa jinsi SSH alivyo na consistency ya kutibua tibua mienendo ya JPM nahisi anaweza kufanya 7/10.
 

Karaoke

Senior Member
Nov 22, 2019
120
250
Hapo namba 6, ni ngumu serikali kuajiri sana sio kwa Tanzania tu,hata kwa wazungu ajira serikalini ni tatizo, labda iimarishe sekta binafsi ili ziajiri zaidi
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
14,486
2,000
Asante sana Kwa ushauri mzuri. Nadhani hata yeye amejifunza makosa aliyofanya mteule wake.
 
Jan 28, 2020
86
125
  • Mlishauri serikali inunue ndege leo mnaiponda serikali hiyo hiyo kwa kununua ndege
  • Mlishauri serikali iwanyime motisha ya msamaha wa kodi wawekezaji sasa nyiye ndiyo mnailaumu serikali kwa uwekezejai kudorora
  • mliishauri CCM imuache Lowassa kuwa ni nani sijui nyinyi mkampa ugombea urais
  • tuliposema tutaishida corona kwa kumtegemea Mungu + tiba asilia + tiba za kisasa isipokuwa lockdown nyie mlisema Mungu si kitu barakoa inatosha na ikwekwa lockdown tumepona
nk n k
Mama Samia wasikie tu usiwasikilize
Mkuu nafikiri ungejikita katika hints tajwa hapo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom