Rais Samia Suluhu ukiongeza mshahara na Madaraja Mei Mosi 2021 watumishi wataandika jina lako kwa Mhuri wa moto kwenye mioyo yao

Acheni kimsumbua mama. Mwacheni kabisa atulie kwanza.

Mbona Magufuli mlikuwa hammdai hizo nyongeza? Si mlikubali kwamba tujenge Sgr na bwawa la Nyerere kwanza? Imekuwaje sasa muanze kumsumbua mama... Serikali ni ileile...tulieni.
 
Hakika kama kuna kundi ambalo lipo dersparate ktk jamii basi ni watumishi wa umma, wamedhalalika sana!! wanakopa hao mpaka wanajificha!!
wapeni Haki zao, acheni kukalia haki za watumishi.
 
"YEHODAYA, post: 387260
mmmmmm mnataka muendelee na ukare wenu .Mwanaume anaacha kuandika mnke wa ndoa na watoto wake anaenda muweka hawara yake na watotoi wa hawara yake ambao hata hakuzaa naye.Hili malipinga kwa nguvu zote.i

Kwani wewe una ubia pale NHIF?au mmiliki wa NHIF ni babu yako nini?
Hili linchi Lina watu wa HOVYOHOVYO KICHWANI.[/QUOTE]
 
Hivi kwanini JPM alikuwa haongezi mshahara? Na akisikia manunguniko anadai hata yeye hajaongezwa. Hivi ilikuwa sahihi CEO kujifananisha na messenger na wengine?
 
Hakika kama kuna kundi ambalo lipo dersparate ktk jamii basi ni watumishi wa umma, wamedhalalika sana!! wanakopa hao mpaka wanajificha!!
wapeni Haki zao, acheni kukalia haki za watumishi.
Hatukopi Tu Bali tumekuwa ombaomba.
 
Wewe ni mwongo! Usilinganishe kwa tarakimu. Wakati wa Nyerere sh ilikuwa ina nguvu. 1985 fresh engineering graduate alikuwa analipwa sh 2750, bei ya tray ya mayai Kibaha ilikuwa sh 15!
Mkuu sina sababu yeyote ya kudanganya.Ili iweje hasa?If money had value nobody would complain. Money had value before the Uganda war,but after the Uganda war everything went wild.Mishahara haikuongezwa kwa kuwa nchi haikuwa na fedha na vitu vikapanda bei kwa kuwa vingi havikuwepo madukani,they were sold in the black market.I remember the only thing that you could get in shops was Marie biscuits and Siftings tea!The shops had virtually nothing.

Mkuu hivi unajua at one point we ran out of money and Norway had to come to our rescue by even paying salaries of civil servants!Wewe you are refering to an ideal economic situation,Tanzania after the war,that is 1978 onwards, hali ilikuwa tete sana.Everything went out of control.

Tuliambiwa tufunge mikanda for a year hali itakuwa nzuri ,it never improved mpaka Mchonga akaamua kung'atuka.Tulifulia majani ya mpapai na kutengeneza mafuta ya kula wenyewe kwa kutumia matunda ya miwese kwa kuwa hapakuwa na mafuta ya kula madukani!Hatukuvaa makata mbuga kwa kupenda mkuu,tulivaa kwa kuwa there were no shoes in shops.Tulifika mahali ukimuona mtu kabeba rambo,ujue katoka Ulaya.Hata dawa ya mswaki ilikuwa haipatikani.Mkuu unanikumbusha machungu ya Mchonga,tuache tu.
 
lkn cha kushangaza kuna baadhi ya watumishi wa umma wanalipwa mshahara mpaka Milioni 15, mil.10 kwa mwezi,.

Serikali inapaswa iangalie watumishi wa chini...sio wale wanao pokea mishahara kuanzia milioni 4 mpaka 10 kwa mwezi.

Serikali iwaangalie watumishi wanao lipwa mishahara kuanzia Milioni 2 kushuka chini
 
Kwenye uhamisho hapana mkuu kila mtu atataka akafanye Kazi mjini au sehemu aitakayo uko vijijini au Kuna sehemu watakosa walimu alafu itakua Haina maana swala unapodai maslahi ya watumishi hasa walimu na idara ya afya ambao Mara nyingi huduma wanazotoa zinahitajika Sana vijijini basi iendane na ikama (idadi tarajiwa) sehemu husika ili kuleta matokeo chanya kwenye utendaji .Tunaitaka Tanzania iliyoendelea
 
Naomba nikusaidie, umeingia matopeni huwezi kuvuka. Ukweli uko hivi:

1. Si kweli kwamba watumishi wa umma hawajaongezwa mshahara, kila mtu ana mkataba wake anapanda ngazi moja kila miaka kadhaa. Na kuna wengine wamepata promotions si kweli kwamba hawajapanda mshahara.

2. Magu alipandisha kima cha chini kwa kuongeza threshold ya PAYE. Huu ni mshahara wa pili almost, hasa kwa walio chini.

3. Kila mtumushi wa umma ana watoto, wengine hadi watoto 7 au 10. Nusu yao ni umri wa kwenda shule, sasa wanasoma bure. Kabla ya Magu, watoto milioni 2 walikuwa nyumbani tu wakichunga ng'ombe au kupiga miayo kwa sababu wazazi hawana hela ya ada ya shule. Sasa wote wanasoma, huu ni mshahara mkubwa sana.

4. Swali kikokotoo huna ujuzi nalo umeparamia tu. Hii ni sheria ya uchumi utaikuta duniani kote. Sina haja ya kukuelimisha ukitaka kujua nilipe au nenda Chuoni ukasome ulipe.

5. Mkopo wa Loans Board ni haki ya Watanzania wote. Kama wewe unataka usilipe riba au kuurudisha ilina wengibe waoate, jitoe. Kuna wengi saba watalipa riba na kurudisha deni kwa furaha kwa hiari.

Kwa ujumla haya ni malalamiko yako tu umeazima kutoka kwa tundulissu alisema hivohivo na matusi sawia. Ndiyo alibwagwa chini puuu!
Nafikiri hukutakiwa kucomment chochote aisee....Ni aibu
 
Badala ya kuomba kupandishiwa mishahara ni kwanini msiombe bei za bidhaa zishuke? Mnataka muongezewe mishahara kwani mmeongezewa kazi?
Hela wanayo omba waongezwe itatokana na ongezeko la kodi kwa wafanya biashara, wakulima na wenye viwanda. Wafanyakazi halitawahusu kwani hata PAYE hayati aliwapunguzia. Kodi iliopo bado inapigiwa kelele kuwa ni kubwa, ongezeko lolote la kodi litaongeza mfumuko wa bei ambao utameza walicho ongezwa kwenye mshahara na wataanza upya kudai kuongezwa mshahara. Ni tabu tupu.
 
lkn cha kushangaza kuna baadhi ya watumishi wa umma wanalipwa mshahara mpaka Milioni 15, mil.10 kwa mwezi,.

Serikali inapaswa iangalie watumishi wa chini...sio wale wanao pokea mishahara kuanzia milioni 4 mpaka 10 kwa mwezi.

Serikali iwaangalie watumishi wanao lipwa mishahara kuanzia Milioni 2 kushuka chini
Hapo nakuunga mkono. Tatizo lipo kwenye mlinganisho wa mishahara na kipato Tanzania. Kundi dogo la wafanyakazi na wanasiasa wanalipwa mapato makubwa sana, na ndilo lenye uwezo kupanga kujiongezea mapato zaidi kupitia safari za kikazi, semina na mengineyo. Huku kundi kubwa la watumishi na wasio katika ajira rasmi wakilipwa au kupata kisicho weza kidhi mahitaji yao.
 
Hela wanayo omba waongezwe itatokana na ongezeko la kodi kwa wafanya biashara, wakulima na wenye viwanda. Wafanyakazi halitawahusu kwani hata PAYE hayati aliwapunguzia. Kodi iliopo bado inapigiwa kelele kuwa ni kubwa, ongezeko lolote la kodi litaongeza mfumuko wa bei ambao utameza walicho ongezwa kwenye mshahara na wataanza upya kudai kuongezwa mshahara. Ni tabu tupu.
Ndio maana sioni sababu ya kudai nyongeza ya mishahara, maana hiyo nyongeza itamezwa na mfumuko wa bei, uko sahihi 100%, wadai serikali iwezeshe uzalishaji mali na huduma wenye tija ili bei za bidhaa na huduma zishuke, kiasi hata hicho kidogo wanacholipwa kitoshe
 
mmmmmm mnataka muendelee na ukare wenu .Mwanaume anaacha kuandika mnke wa ndoa na watoto wake anaenda muweka hawara yake na watotoi wa hawara yake ambao hata hakuzaa naye.Hili malipinga kwa nguvu zote.ibakie kama ilivyo
naamini hii sababu umejitungia tu,ila kama ni kweli ndiyo sababu iliyotumika kufanya maamzi yale,na hao waliyoyafanya wanajiita wataalam,basi mimi sitaki kuwa mtaalam
 
Ukitaka kujua unyonge wa watumishi wa umma kuendelea au kukoma ni tamko rasmi la mama, rais Samia Suluhu kutangaza ongezeko la mishahara miez ijayo na sio kuboresha masilahi yao katika kipindi chake cha awamu ya Sita bila kutaja muda rasmi.
 
Back
Top Bottom