Uyu mbulumundu,kumbe kajiunga juzi tuu??
Hivyo ndivyo umenielewa. Wengine wamenielewa tofauti, kwa vyovyote kila mmoja aelewe anavyoweza isipokuwa wote tunakutana katika msamaha.Ndugu kati ya haya iliyoandika, lipo hata moja limesomwa mahakamani? Kama sivyo, wewe ndiye unayejifucha kwenye kivuli cha Magufuli ili umtete huyu swahiba wako Sabaya.
Shutuma za Sabaya mahakamani ziko dhahiri; rushwa ujambazi wa kutumia silaha na matumizi mabaya ya madaraka. Je haya yanakihusuje chama cha mapinduzi? Walimtuma? Je haya yanahusianaje na ubunge wa Hai na Mbowe? Je haya aliyoyafanya ndio yaliyofanikisha ushindi wa ccm Hai? Maswali ni mengi, ila itoshe kusema tuhuma za Sabaya ni personal na usitake kuihusisha na ccm.
Juu ya mwendazake, ni sahihi kuhusishwa naye kwani ukweli uko wazi. Haya mengi sabaya alifanya wakati wa uongozi wa mwendazake na hakukemewa licha ya kuchukuliwa hatua. Kuweri ni ukweli tu, haufichiki.
Sio rahisi kupata maumivu katika maoni rahisi yaliyofunikwa na chuki, ubinafsi, hasira, visasi na ushabiki. Maoni yenye kupingana na msimamo wa maneno ya Mungu hayawezi kuumiza nafsi iliyoshiba msamaha. Ninaendelea kuwasamehe wote wenye kuona tunapaswa kulipa visasi katika maridhiano.Mleta mada, wakati ukisoma michango ya wadau, kaa na vidonge vya kutuliza maumivu jirani.
Hapo sasa....!!!!Ngoja kwanza nicoment kabla ya kusoma: yaan siku mbili izo unaona sabaya ndo binadamu kuliko walionyanyasika wakati woote wa uongozi wake
Kuna tetesi eti bia yetu ilikua id ya meko....😃Hizi ndo zile ID za kazi maalum kama za akina Bia yetu, uchaguzi ulipoisha tu, akasepa jf mazima.
Hapana. Hii ndio rasmi, ni bahati mbaya nilichelewa kujumuika katika jukwaa hili, mimi sio mwenyeweji humu. Matusi, kashfa na maoni yasiyozingatia utu vilinichelewesha lakini hata hivyo muda ulipofika sikua na chaguo. Kwa maneno hayo, hii ndio ID yangu rasmi.Mleta mada JF ID yako rasmi siyo hii: Wakudadavuwa?
View attachment 1808930
Mwaka huu makopo yanawahusu sana.
Nimechagua kupita njia hiyo kwa sababu wenzetu wametangulia. Kama sio kulifanya swala la Sabaya kuwa kisasi cha Ubunge wa Freeman hata mimi (sisi) tungaliacha mambo yaende inavyostahili. Kwa sababu wenzetu wameanza, sisi tumaomba tumalize. #HatutoiPointTatu.Hili jambo tuache Sheria ichukue mkondo wake ili haki itendeke maana hata wewe unakubali ya kuwa kuna makosa amefanya na kama hana makosa haki itendeke. Unachojaribu kukionyesha hapa ni ushabiki wa chama/kisiasa. What if makosa anayotuhumiwa yangekuwa yamefanywa na mtu kutoka upinzani? Sidhani kama ungekuja na haya maelezo yenye mlengo wa kisiasa na kutaka kuonesha huruma.
Hapana. Hii ndio rasmi, ni bahati mbaya nilichelewa kujumuika katika jukwaa hili, mimi sio mwenyeweji humu. Matusi, kashfa na maoni yasiyozingatia utu vilinichelewesha lakini hata hivyo muda ulipofika sikua na chaguo. Kwa maneno hayo, hii ndio ID yangu rasmi.