Rais Samia Suluhu tumia Teknolojia kuiokoa Tanzania

MzeeWaTeknolojia

New Member
Apr 11, 2021
4
4
Kwako Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,

Hoja yangu kwa sentensi moja: napendekeza serikali iwekeze kwenye matumizi ya teknolojia (haswa simu, mitandao ya mawasiliano, na apps) ili kuboresha utumishi wa umma na utawala bora.

Hoja yangu kwa kirefu kidogo: napendekeza uanzishe Shindano La Ubunifu Kwenye Utumishi Wa Umma (Public Service Innovation Challenge) ambalo litahamasisha (motivate), litatambua (recognize) na kutoa zawadi (reward) kwa Mtanzania yeyote atakaebuni na kuonyesha mfumo unaotumia teknolojia kutatua matatizo mbali mbali kwenye utumishi wa umma, haswa kwenye swala la matumizi mabovu ya pesa kama yalivyoanikwa kwenye ripoti ya CAG siku chache zilizopita.

Hoja yangu kwa urefu wake kamili:
Mhe Rais, kampuni ya Facebook ina wafanyakazi takriban elfu 58 tu lakini wanahudumia wateja bilioni 2.6 kila mwezi. Yani ni kama kila mfanyakazi mmoja anahudumia watu elfu 44! Inawezekanaje?!

Mhe Rais, kampuni ya Walmart kule Marekani yenyewe inawafanyakazi takriban milioni 2.3. Hiyo ni idadi ya wafanyakazi tu, sio wateja. Inawezekanaje kampuni moja ikaajiri na kusimamia watu wengi namna hiyo?!

Mhe Rais, bila shaka umeshawahi kumsikia Jeff Bezos. Huyu ndio tajiri namba moja duniani kwa sasa, na utajiri wake (net worth) ni sawa na dola za kimarekani bilioni 196. Inawezekanaje binadamu mmoja akawa na utajiri ambao ni mara tatu ya pato la taifa letu lenye watu milioni 58?!

Mhe Rais, jibu la maswali hayo na mengine mengi ya mfumo huo ni lile lile: nguvu ya teknolojia zinazojumuisha simu (smartphones), mitandao (internet) na apps mbali mbali.

Mhe Rais, siku chache za nyuma wakati unaapisha makatibu, uliwasistiza waende kuwa wabunifu. Tatizo la kuwa mbunifu kwenye sekta ya umma ni kwamba hamna faida yeyote kwako binafsi. Huku kwenye sekta binfasi hamna kikomo kwenye kipato chako - ukiwa mbunifu unaweza kunufaika kwa mabilioni ya pesa. Huko serikalini kupata mabilioni inabidi uyaibe na ndio kinachofanyika miaka nenda rudi.

Kutatua tatizo hilo, tenga bilioni moja ya kutoa kama tuzo kisha anzisha Shindano La Ubunifu Kwenye Utumishi Wa Umma (Public Service Innovation Challenge). Acha wananchi wabuni mifumo na walete proposal pamoja na mifano (yani demo) mbele yako. Toeni kati ya milioni 50 hadi milioni 200 kwa proposal zenye mvuto ili kuwezesha utelekezaji (full implementation) wa proposal husika. Utakuta proposal nyingi zinaishia njiani ila kati ya kumi utapata moja ambayo itabadilisha hili taifa kwa kipindi cha miaka hata 100 ijayo.

Mhe Rais, umepata fursa ya kipekee ya kuwa mwanamke wa kwanza kukaa kwenye kiti cha Rais kwenye taifa letu. Ukiwekeza kwenye matumizi ya teknolojia katika serikali yako unaweza kuwa Rais wa kwanza Tanzania, kama sio barani Africa au duniani kwote, mwenye uwezo wa kuamka asubuhi na kuona (kwenye simu yako) matumizi yote ya pesa yanayofanyika kwenye kila wizara/taasisi pamoja na orodha nzima ya watu wote walioidhinisha matumizi hayo mpaka ngazi ya kule chini kwenye serikali za mitaa.

Kwa wanabodi wenzangu, nimekua nikisoma post za JF kwa muda mrefu na kunufaika kwa mawazo yenu. Asanteni sana! Huu ndio uzi wangu wa kwanza hivyo naomba mchangie mawazo yenu (mfano mbinu mbali mbali za kuendesha shindano lililopendekezwa hapo juu na namna ya kudhibiti wezi watakaopinga mawazo kama haya kwasababu yatazuia ulaji wao) ili kama nchi, tupige hatua na sote tuwe na maisha yanayoheshimika (dignified life) na yanayotokana na jasho halali.

Nawashukuru,
Mzee Wa Teknolojia.
 
Kwanza kabisa Tanzania turushe satellite yetu wenyewe ili isaidie kupunguza gharama za internet....

Halafu mengine ndo yafuate
 
Swali langu lipo nje mkuu watu 2.6m kama warlmart wanafanya nini zaidi? Naona wengi sana pia facebook hao wote elfu 58 inakuaje wakati app zipo chache na makao makuu sehemu moja USA najua wewe mzee wa technology utalijibu kiteknology
 
Umeanza vizuri
Joined today na thread Kongole.
Nashukuru sana! 🙏

Endapo wazo hili litamfikia Mhe Rais, naomba aangalie mfano wa bilionea Mo Ibrahim (alieanzisha kampuni ya Celtel ambayo leo tunaijua kama Airtel). Yeye kupitia foundation yake alianzisha Ibrahim Prize inayotoa $5mln USD (sawa na TSH bilioni 11.5) kwa viongozi bora wa Afrika watakapotoka madarakani.

Mfumo kama huu ukiwepo kwa watumishi wote wa umma wa ngazi zote, naamini watumishi watakua na moyo mkubwa zaidi wa kulitumikia taifa vizuri kwasababu mwisho wa siku mwenye nyumba akija kudai chake, vitu kama "uzalendo" na "moyo wa kujitolea" havimuhusu: yeye anataka pesa taslimu tu 😅
 
Kwanza kabisa Tanzania turushe satellite yetu wenyewe ili isaidie kupunguza gharama za internet....
Chochote tunachoweza kufanya kupunguza gharama za teknolojia, ikiwemo internet uliyotaja lakini pia vitu kama simu na computer, kitatusaidia kupiga hatua.

Tanzania tumejitahidi sana kwenye maswala ya internet/mawasiliano (mfano angalia mkonga wa taifa) na watu wengi wako active sana kwenye mitandao.

Tukikaza huku zaidi tukaanza kuitumia mitandao vizuri kwenye ufatiliaji wa mambo mbali mbali (kama matumizi ya pesa za umma) hakika tutafika mbali. Ni viongozi tu kuamua, uwezo upo na watendaji tupo wengi tu 💪
 
Swali langu lipo nje mkuu watu 2.6m kama warlmart wanafanya nini zaidi? Naona wengi sana pia facebook hao wote elfu 58 inakuaje wakati app zipo chache na makao makuu sehemu moja USA najua wewe mzee wa technology utalijibu kiteknology
Hao Walmart ni supermarket kubwa hatari, ina matawi zaidi ya 4,700 kwahiyo wafanyakazi wengi watakua wafanya shuguli za kuendesha matawi hayo na kuhakikisha bidhaa zinawafikia wateja.

Kwa upande wa Facebook, hakika wafanyakazi elfu 58 ni wengi, ila kumbuka Facebook ndio inamiliki Instagram na Whatsapp, huduma ambazo zote zinawateja zaidi ya bilioni moja. Asilimia kubwa ya wafanyakazi wengi wa Facebook naamini wapo kwenye kazi ya moderation (kuzuia urushaji wa mambo ya ajabu ajabu kwenye mtandao huo), nishasoma sehemu kuna watu elfu 10 waliajiriwa kwa kazi hiyo miaka ya nyuma.

Kingine cha kuelewa upande wa kampuni kama Facebook na Google, ni kwamba mitambo yao (yani computer kubwa ambazo kitaalam tunaita servers) ni mikubwa vibaya mno na inahitaji watu wengi kuisimamia. Angalia video hii kuona mfano:

 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom