Rais Samia Suluhu, suala la Bandari ya Dar na umuhimu wa Deusdedit Kakoko umeonekana dhahiri

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Madudu yameanza bandarini ndani ya muda mfupi sana baada ya DG engineer Kakoko kuondolewa bandarini.

Ifahamike hapo nyuma matatizo haya yalikuwepo mpaka Magufuli aliingilia kati akiamini ndio roho ya nchi kiuchumi, hatimaye bandarini palisafishwa na ufanisi kurejea ukiambatana na ongezeko la mapato ya bandari, mizigo kuondoka kwa haraka sana na malalamiko kwa wateja kama hayakwisha basi yamepungua kwa kiasi kikubwa sana, kazi hii ilifanywa vyema na engineer Kakoko.

Cha kushangaza CAG katika report yake akataja bandarini kuna matumuzi mabaya ya fedha za umma na kugharimu nafasi ya DG wa bandari, Mr Kakoko, siamini kama Kakoko alikuwa na hatia bali ni mpango uliosukwa kwa ustadi barabara na wafanyabiashara baadhi wasio waaminifu wakwepa kodi ambao hawakupenda kazi nzuri ya Kakoko kwani aliwadhibiti barabara.

Kwa kuthibisha hilo, Rais Samia ulielekeza Takukuru kufanya uchunguzi bandarini hapo na kutengua nafasi ya Kakoko kabla ya uchunguzi kukamilika. Ni sawa lakini ilifaa asimamishwe mpaka uchunguzi ukamilike, cha kushangaza, haraka tu Rais Samia ukapeleka mtendaji mkuu mwingine, ni kama ilikua njia ya kumtoa

Takukuru walifanya uchunguzi wao na walipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu uchunguzi ulipofikia, walidai wanaendelea na uchunguzi na itachukua muda mrefu kwa Kakoko kupelekwa mahakamani.

Kwangu mimi walikosa ushahidi wa kumtia hatiani na kwa kuwa Rais Samia alikwisha tengua wakaona isiwe tabu. Kinachoendelea kwa sasa bandarini ni rushwa kubwa na magendo ya wafanyabiashara baadhi wasio waaminifu,kutaka kupitisha mizigo yao kwanza, hatimaye wanasababisha inconveniences isiyo ya lazima kwa watumiaji wengine.

Nimkumbushe Rais Samia aspokuwa makini ataangushwa sana tu,ni kama alivyotaka kumtengua Mataragio wa TPDC na kumrudisha ndani ya saa 24 ,hapa inaonekana kuna watu wanapanga safu zao bila yeye kujua, na umakini ni sifuri ,asposhtuka atakwama .
Hali hii ya kuumiza watendaji makini wasio penda rushwa ilifanyika sana awamu ya nne ,majungu kupakaziana ndio ulikuwa mtaji , naona hali hiyo inataka kujirudia.

Mwisho ufanisi wa bandari zote nchini utapimwa kwa namna unavyofanya kazi kwa mafanikio na mapato kwa serikali yakiongezeka ,

Hivyo maamuzi ya rais Samia kama yanatija kwa bandari, yatapimwa kwa graph, kipindi cha Kakoko na huyu ulie mteua ,muda ni mwalimu.
 
E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
Hata hivyo huyo aliyekuwepo alijenga mfumo wake na sio wa taasisi, ili kupata mafanikio endelevu inahitajika watu watakaojenga mifumo ambayo kila atayekuja haitampa nafasi ya kufanya anavyotaka. ni wakati sasa Raisi aajiri wafanyakazi kutoka nje ili walete utaalamu na uzoefu ili kuondokana na hili tatizo.
 
Hapa kuna mawili (1) Huenda kweli Kakoko alikuwa mtendaji mzuri asie endekeza rushwa sababu iliyofanya watu wamtengenezee majungu, fitna na chuki isiyokuwa na msingi (2) Huenda Kakoko ametengeneza vijana wake waliobakia hapo ili waweze kumfanyia hujuma DG mpya ili baada ya muda mfupi aonekane hajui kazi nk. So let's wait to see what's gonna happen.
 
Back
Top Bottom