Rais Samia Suluhu Sh. Trilioni 2/- za IMF anaweza kuzitumia wapi?

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Bodi ya Shirika la Fedha Duniain (IMF) hapo jana iliidhinisha mkopo wa dola za Kimarekani Bilioni 1.046 ambazo ni sawa na shiliingi Trilini 2.4/- za kitanzania katika kipindi cha miezi 40 ili kusaidia katika kupambana na athari za viizotokana na vita ya Urusi na Ukraine.

Huu mkopo Tanzania tuliuomba Mei mwaka huu, imechukua takribani miezi miwili tu kuupata. Unaweza kudhani ni rahisi au IMF wanapenda kukopesha watu pasi na kujali vigezo na masharti ambayo Taifa lazima livitimize.

Kwanza naipongeza sana serikali ya Rais Samia Suluhu kwa kufanikisha hili, kwani hakuna wakati ambao Tanzania inahitaji mkopo huu kama muda huu ambao serikali inatumia Tsh. Bil. 100 kila mwezi kama ruzuku kudhibiti bei ya mafuta.

Kupewa mkopo na IMF sio jambo rahisi au ambalo kila Taifa linaweza kufanya. Tanzania ina 'Balance of Payment' nzuri, hicho ni moja ya kigezo kikubwa. Balance of Payment kwa ufupi, ni uwezo wa nchi kuweza kuhimili madeni yake, uwezo wa kulipa, kuagiza kutoka nje na kuuza.

Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan biashara zimeimarika zaidi, uwekezaji wa nje na wa ndani umeimarika zaidi, benki za biashara zimeendelea kutoa mitaji zaidi kwa wafanyabishara na faida imekuwa ikitengenezwa kwa kiasi kikubwa tu. Mauzo nje hasa mazao pamoja na madini yameimarika maradufu. Mfumuko wa bei umedhibitiwa (4.4%) na jitihada za dhati zinafanyika kumpunguzia ugumu wa maisha Mtanzania.

Sasa kwanini nimesema Tanzania inauhitaji zaidi huu mkopo?

Kama mjuavyo mafuta ni janga la kidunia, na maadamu Tanzania imo duniani, basi hatuwezi kulikwepa. Serikali ya Rais Samia Suluhu ikaona ibane matumizi ya Serikali na kutoa kiasi Tsh. Bil 100 kila mwezi kama ruzuku katika ili kudhibit bei ya mafuta kupanda zaidi. Lakini Bil. 100 ni nyingi sana, na pengine fedha hii ingetumika kujenga barabara, hospitali, kununua madawa na kusambaza maji vijijini, lakini inawekwa kwenye mafuta.

Kutoa Bil. 100 kila mwezi kunaweza kukausha hazina yetu. Kenya wameshatangaza tayari kwamba hazina yao iko hatarini kutokana na kutumia ruzuku kwa wingi katika mafuta. Ukifubaza hazina serikali itashindwa kabisa kutoa huduma kwa watu.

Mkopo wa IMF utasaidi hapa. Hata kama tutaoa Bil. 100 kila mwezi, bado mkopo utatusaidia kutoa huduma kwa watu wetu. Mkopo utapunguza kasi ya kufubaza hazina yetu, na pia mkopo utatumika kuongeza nguvu katika hifadhi yetu ya fedha za kigeni na pia mkopo huu utasaidia kufufua uchumi katika yale maeneo ambayo yameathiriwa zaidi na janga la UVIKO-19 pamoja na vita ya Ukraine na Urusi.

Rais Samia Suluhu ni hodari wa kusimamia fedha kama hizi, hapa majuzi sote tulisikia kongole zikitoka benki ya Dunia (WB) kumsifu yeye kwa uhodari wake wa kusimamia vyema miradi ya nchi na hukikisha usimamizi mzuri wa fedha. Mkopo huu ni mkombozi kwetu, matumizi yetu ya ndani ni makubwa sana na hajawa bado na uwezo wa kukusanya kingi kwa muda mfupi na kumfikia kila Mtanzania ili apate maji safi na salama, elimu bora na nafuu, umeme bora na nafuu na huduma nyingine, na watu hawawezi kusubiri hadi Serikali ipate, ni lazima tukakope ili kila Mtanzania aishi kwa raha na amani nchini mwake.

Naipongeza kwa mara ya pili tena Serikali yetu chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
 

Attachments

  • XSYBCUM445JCZN4MMCP5J5VK6E.jpg
    XSYBCUM445JCZN4MMCP5J5VK6E.jpg
    566.5 KB · Views: 5
Kwasababu imeshaonekana hizo pesa wanaweza kubadilisha matumizi yake kama walivyofanya kwa zile za Covid 19 kujengea madarasa..

Nashauri azipeleke kwenye kushusha bei ya pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, kama hili likifanyika litasaidia kuongeza uzalishaji wa nafaka ambao utasaidia kushusha bei ya mazao kama mahindi na mpunga zinazozidi kupanda kila siku.
 
Bilioni mia kwa mwezi ndio ikaushe hazina huu ni upuuzi mkubwa, kuna matumizi ha hivyo serikali ikibana hiyo bilioni 100 itapatikana au kukaribia kupatikana

Mfano kwenye level ya maisha ya mtaani(binafsi/mmoja mmoja) Kinachowaponza watu MUFIILISI ni kujaribu kumaintain status, alikuwa wa milioni 30 kwa wiki, sasa kawa qa milioni 10 kwa mwezi ila bado anafosi aishi maisha ya milioni 30 kwa wiki.

Serikali ipunguze bajeti, viongozi kama wao kweli ni watetea wanyonge kama wanavyojinadi, kama kweli ni wazalendo wafanye hivyo

Hawawezi sababu ni wanafiki, ni wabinafsi, ni wachumia tumbo.

Nchi wanaitumbukiza shimoni, kila siku ni afadhali ya jana
 
Kwasababu imeshaonekana hizo pesa wanaweza kubadilisha matumizi yake kama walivyofanya kwa zile za Covid 19 kujengea madarasa..

Nashauri azipeleke kwenye kushusha bei ya pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, kama hili likifanyika litasaidia kuongeza uzalishaji wa nafaka ambao utasaidia kushusha bei ya mazao kama mahindi na mpunga zinazozidi kupanda kila siku.
Mawazo mazuri sana

To ensure food security

Sehemu nyingine ni kuongeza ruzuku ya mafuta na bidhaa muhimu za vyakula mana inaathiri kila mtu

upande mwingine adimu jmn
Package maalum ya Mikopo kwa vijana japo Bn200 kupitia halmashauri zetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom