Rais Samia Suluhu, matatizo waliyonayo Watanzania ni ajira kwanza na siyo nyongeza kwa watumishi wa umma ambao ni 0.6% ya Watanzania

Mkuu punguza roho mbaya hacha watu wapate stahiki zao, lazima kuajili huku ukiboresha maslai ya wale ulionao,
Sijasema wasipate maslahi, Ila kwa namna inavyozungumziwa ni Kama watanzania wote ni watumishi wa umma.
Kelele nyingi huku hawafiki hata 1% ya watanzania wote.
 
Acha uchawi wewe mleta mada!

Vyote vinahitajika, Yaani Ajira na Masilahi bora ya wafanyakazi, na ndiyo maana Rais anafanyia kazi vyote!
Hilo la maslahi ya wafanyakazi kwa makusudi linafanywa Kama ajenda ya watanzania wote huku uhalisia ni kuwa watumishi wa umma ni 0.6% ya watanzania wote.
Sisemi asiwaongezee mishahara Ila tatizo kelele. Nyingi huku wanaotegemea kilimo ambao ni zaidi ya 65% ya watanzania wakiwa wanaonekana hawana maana.
Mama anatakiwa ku-deal na hili kundi kubwa
 
Nyongeza ndio ajira yenyewe hio.Ukiongeza uwezo wa mtumishi kununua mahitaji yake mfano nguo, chakula,usafiri,ujenzi,nk mfanyabiashara atauza atapata faida.
Kumbuka enzi ya JK nyumba za nyasi nchini zilitoweka kwa speed ya uyoga sababu ya mzunguko mzuri,zilisimama ilipoingia awamu ya kuwasomesha namba watu,awamu ya propaganda za kuhadaa wanyonge.
 
Sio kweli, impact ipo lakini ndogo Sana.
Wafanyakazi wa umma 0.6% haiwezi kuleta unafuu kwa watanzania 99.4%.
Mama Samia anatakiwa ku-deal zaidi na kundi kubwa ambalo wanaotegemea kilimo ambao ni 65%
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom