Rais Samia Suluhu kuzuru Uganda Kesho Aprili 11 kwa mwaliko maalumu wa Rais Museveni

Rais kufanya Ziara ya siku moja nchini Uganda anatarajia kuonana na Mwenyeji wake Yoweri kaguta Museveni. More to follow

C3E52372-5BD3-4588-B891-1D38659D576B.jpeg
 
Awe mwangalifu, asije akasainishwa mkataba uliofanyiwa maboresho, tofauti na ule uliokwishakubaliwa wakati wa Magufuli.

Asikubali marekebisho kiurahisi.

Hapo hapo, ni wakati mwafaka sasa kwa Tanzania kujihusisha zaidi kibiashara na Uganda. Nguvu nyingi sana zimeelekezwa kwenye biashara na Kenya, kiasi kwamba majirani zetu wengine ni kama hawapo!
Tazama kwa mfano njia kuu za kuingia Kenya: Sirari, Namanga, Holili, na Horohoro, na bado kuna vichochoro vingi sana vya kuvusha mali kwa njia zisizo halali.

Uganda na Tanzania, njia kuu ni moja tu, kama ilivyo kwa Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Mozambique.

DRC yenyewe, hata hakuna njia kabisa inayoeleweka. Hawa tungekuwa nao mwingiliano mkubwa zaidi kuliko nchi zote majirani, kwa sababu tunao mpaka mrefu zaidi nao. Hata kama walikuwa na matatizo yao, hayo matatizo hayatakuwepo siku zote. Ni wakati mwafaka sasa kuongeza biashara nao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom