Failure of the organisation is failure of the management. Failure of a nation is failure of the leadership, and vice versa.
Kama nchi itaendelea kuwepo kwenye mkwamo wa sasa, au ikaenda kwenye hali mbaya zaidi kuliko ilivyo sasa, tutambue kuwa atakayekuwa amesababisha ni Mh. Rais Samia. Lakini pia, kama Taifa hili litabadilika kutoka kwenye hali mbaya ya sasa na kwenda kwenye ustawi wa kweli, atakayekuwa amesababisha ni Mh. Rais Samia. Siyo wasaidizi wake, maana wasaidizi huteuliwa na yeye. Uteuzi wa wasaidizi nayo ni kipimo cha uwezo wa uongozi.
Kiongozi mwenye upeo mkubwa, uelewa na hekima, anajua amteue na na asimteue nani kama anataka kufikia malengo aliyoyapanga.
Wakati wa Mwungano wa Urusi, USSR, watu kwenye mataifa yaliyotengeneza huo mwungano, waliishi kwenye udikteta wa ajabu, watu walifungwa, waliwekwa vizuizini, wenginebwaliuawa kama kuku walipotaka kuuruka ukuta wa Berlin ili kuyatafuta maisha mazuri Ujerumani Magharibi. Hayo yalitokea na kuendelea kwa miaka mingi na kwa vipindi mbalimbali vya viongozi wa Urusi. Hakuna kiongozi aliyejaribu kuibarilisha hali hiyo.
Ni mtu mmoja tu aliyesababisha watu wote kwenye mataifa yaliyokuwa yanaunda mwungano wa USSR kuwa na uhakika wa kuishi, kuwa na uhuru wa kusafiri, kuwa na uhuru wa kumiliki mali, n.k. Mtu huyo ni Rais MIKHAIL GORBACHEV. Huyu aliamua kwenda kinyume na wenzake ndani ya chama cha kikomunisti.
Kule Afrika Kusini, kwa miaka mingi, watu weusi walibaguliwa, wakllifungwa, waliuawa. Lakini hata wazungu walishambuliwa na kuuawa na watu weusi. Kwa ujumla, ni kuwa hakuna aliyekuwa na amani kamili na uhuru kamili. Mtu mmoja tu aliyeitwa FREDERICK DE CLERK, ndiye aliyebadili kila kitu, na kuleta tumaini la maisha ya furaha, amani na upendo nchini Afrika Kusini na mataifa jirani, Tanzania ikiwa mojawapo. Huyu aliamua kwenda kinyume na katakwa ya kundi lake lililoasisi na kuneemeka na siasa za ubaguzi wa rangi
Katika rejea zote mbili, USSR na Afrika Kusini, walioleta mabadiliko ni watawala ambao walitoka kwenye mfumo wa utawala gandamizi, yaani kutoka kwenye kundi la utawala lililokuwa likineemeka kwa gharama ya mateso na upotevu wa maisha ya makundi mengine.
JE, SAMIA ATAKUWA MIKHAIL GORBACHEV NA FREDERICK DE KLERK WA TANZANIA?