Maslahi ya wafanyakazi asisahau kabisa kuzungumzia.
  • Mishahara nyongeza
  • Fao la kujitoa
  • Malimbikizo ya likizo,kuhama mahali pa kazi
  • Kuongeza wafanyakazi
  • Stahiki/stahili za waliofukuzwa kwa vyeti feki. (Wapewe mafao yao ambayo MEKO aliwadhulumu maana Mh SSH amesema kwamba hataki fedha za dhuluma)
 
Watanzania leo kuanzia saa kumi jioni wanatarajia kupata hotuba ya kwanza ya serikali ya awamu sita itakayosomwa Bungeni, kupitia hotuba hii watanzania wanataraji kusikia marekebisho mengi ya uzandiki yaliyokuwa yanafanywa na awamu ya tano, baadhi ya uzandiki huo ni juu ya miashahara ya watumishi wa umma, ukandamizaji wa haki za binadamu, kubambikiana kesi zisizo na ukweli, mabadiliko ya sheria kandamizi kama vile sheria ya habari na mawasiliano, utekaji wa watu unaofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama,

Hotuba hii tunataraji pia itafungua milango ya ajira, kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma, hotuba itasema juu makosa ya kubambikiana na kufungiana biashara kwa kuongezeana kodi za uongo, kufungua akaunti za watu zilizofungwa bila ushahidi kwa kifupi wizi wa serikali.

Hii ni serikali tukufu sio kama ile ya awamu ya tano, yakina Sabaya na Sukuma Genge.

Mungu Ibariki Tanzania , Mungu Mbariki Rais wetu Mama Yetu.
 
Je,Leo ndio siku ya maridhiano ya kitaifa yatayofanyika ndani ya bunge letu tukufu ?
Maridhiano ya kitaifa ni uponyaji kwa taifa
Maridhiano ya kitaifa ni baraka kwa taifa
Maridhiano ya kitaifa ni ucha Mungu
Ndugu wakikaa kwa pamoja na umoja Mungu huwabariki
Mara nyingi kinachouwa umoja wa kitaifa ni kauli za wenye mamlaka
Ulimi ni kiungo kidogo lkn hatari katika ustawi na amani katika jamii
Wapenda amani wote
Wapenda haki wote tunasubiri kwa hamu na shauku kubwa hotuba ya mama yetu rais samia suluhu hassani
Tunamuombea kwa Mungu ampe busara na hekima leo atakavyokuwa anazungumza na taifa letu
Mungu ibariki tanzania na watu wake wote
 
Back
Top Bottom