Rais Samia Suluhu kama kweli umedhamiria kuboresha mazingira ya biashara nchini futa utaratibu wa framework contracts kupitia GPSA

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,873
4,276
Kumekuwa na utaratibu wa GPSA kutangaza framework contracts za kusupply bidhaa na huduma mbalimbali kwenye taasisi za umma kila mwaka.

Kusema ukweli utaratibu huu hauna tija. Unaongeza ugumu na gharama katika kufanya biashara na serikali.

Sisi wafanyabiashara tunapo fungua kampuni, tunaruhusiwa kufanya biashara sehemu yoyote ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatuna mpaka wa kufanya biashara. Ingawa leseni za baadhi ya biashara tunakata katika halmashauri iliyopo ofisi, ila haituzuii kufanya biashara sehemu nyingine.

Sasa huu utaratibu wa kuomba tender ki mkoa unatoka wapi? Yaani inabidi ninunue na kuomba tender 26 za ku supply kwa mfano stationery tu. Hii ni kazi kubwa na yenye gharama isiyo ya lazima.

Lakini hata hivyo framework work contract za kila mwaka sijui lengo lake hasa nini. Maana pamoja na kupata framework contract bado unaweza usipate kazi yoyote mwaka mzima.

Sijui lengo la GPSA nini. Kama lengo ni kufanya due diligence, mbona kuna vyombo vingine kama TRA na brela ambapo kila mwaka tunapata clearance certificates?. Au kama ni due diligence basi ifanyike kila baada ya miaka mitatu, siyo kila mwaka.

Kama lengo ni kupanga bei elekezi, GPSA wanaweza wakawa wanafanya utafiti na ku publish bei elejezi za bidhaa mbalimbali kila mwaka au pale inapobidi..ili kuwa guide wanunuzi kwamba wasinunue zaidi ya bei iliyopendekezwa. Wanaweza wakatoa bei elekezi bila kulazimisha suppliers wanunue na kuomba tender.

Mchakato wa manunuzi ufanywe moja kwa moja na taasisi husika kama zamani.

PPRA na CAG wanafanya ukaguzi kila mwaka ili kudhibiti manunuzi yasiyo fuata utaratibu.

Hebu tuangalieni hili swala kwa jicho la tatu hivi Framework contract na GPSA wana add value gani kwenye mchakato wa manunuzi?

Mh. Rais tuondolee huyu mdudu anaitwa framework contract inaongeza vyanzo vya rushwa na gharama zisizo za msingi.
 
Yaani task force TRA ilipora billions zaidi 900 za wafanyabiashara ....wamekwala mihela yao yote wakaweka miradi elephants....ya jiwe noma sanaaaa
 
Hao wafanyabiashara walikwepa kodi mno hawakuonewa.....
serekali ikichukua tu walichokwepa
 
Naunga mkono hoja. Huu utaratibu ni kuongeza urasimu na gharama za kufanya biashara na serikali, taasisi zake na mashirika ya umma

Hata hivyo ushauri huu unaweza kufanyiwa kazi na waziri mwenye dhamana. Mheshimiwa Rais itachukua muda kufikia na kushughulikia kila changamoto iliyopo kwenye taasisi za umma
 
Baadhi ya watu hawapendi serikali ijihusishe na biashara ya aina yoyote, lakini wanapenda sana kufanya biashara na serikali!

Kwa wasiojua mavitu kama "due diligence; GPSA; PPRA, framework contracts, n.k.,, kama mkuu
Msaada kwa tusiojua hiki ni nini
Sijui wao wataanzia wapi kupata upigaji unaopatikana huko serikalini?
 
Baadhi ya watu hawapendi serikali ijihusishe na biashara ya aina yoyote, lakini wanapenda sana kufanya biashara na serikali!

Kwa wasiojua mavitu kama "due diligence; GPSA; PPRA, framework contracts, n.k.,, kama mkuu

Sijui wao wataanzia wapi kupata upigaji unaopatikana huko serikalini?
Siongelei upigaji. Naongelea biashara halali. Hao unao waongelea nao wana sehemu zao za kupatia riziki. Hatuwezi kufanya kitu kimoja wote. Lakini pia hawajazuiwa. Na kupitia hii thread wale wale waliokuwa hawajui na wana interest watajifunza na ndo itakuwa mwanzo wa kujua.
 
Kuna taasisi za serikali zimeanzishwa na haziwezi kujiendesha ndio hizo zinazounda tozo za kinyonyaji ili wapate pesa za kujiendesha na kujilipa.

Kuna taasisi hazina tija, zinaweza kupelekwa zikawe department kwenye taasisi kubwa huko, mizigo kwa mfanya biashara ni mingi sana utadhani tunatengeneza faida mara 5 ya tunachouza.
 
Kumekuwa na utaratibu wa GPSA kutangaza framework contracts za kusupply bidhaa na huduma mbalimbali kwenye taasisi za umma kila mwaka.

Kusema ukweli utaratibu huu hauna tija. Unaongeza ugumu na gharama katika kufanya biashara na serikali.

Sisi wafanyabiashara tunapo fungua kampuni, tunaruhusiwa kufanya biashara sehemu yoyote ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatuna mpaka wa kufanya biashara. Ingawa leseni za baadhi ya biashara tunakata katika halmashauri iliyopo ofisi, ila haituzuii kufanya biashara sehemu nyingine.

Sasa huu utaratibu wa kuomba tender ki mkoa unatoka wapi? Yaani inabidi ninunue na kuomba tender 26 za ku supply kwa mfano stationery tu. Hii ni kazi kubwa na yenye gharama isiyo ya lazima.

Lakini hata hivyo framework work contract za kila mwaka sijui lengo lake hasa nini. Maana pamoja na kupata framework contract bado unaweza usipate kazi yoyote mwaka mzima.

Sijui lengo la GPSA nini. Kama lengo ni kufanya due diligence, mbona kuna vyombo vingine kama TRA na brela ambapo kila mwaka tunapata clearance certificates?. Au kama ni due diligence basi ifanyike kila baada ya miaka mitatu, siyo kila mwaka.

Kama lengo ni kupanga bei elekezi, GPSA wanaweza wakawa wanafanya utafiti na ku publish bei elejezi za bidhaa mbalimbali kila mwaka au pale inapobidi..ili kuwa guide wanunuzi kwamba wasinunue zaidi ya bei iliyopendekezwa. Wanaweza wakatoa bei elekezi bila kulazimisha suppliers wanunue na kuomba tender.

Mchakato wa manunuzi ufanywe moja kwa moja na taasisi husika kama zamani.

PPRA na CAG wanafanya ukaguzi kila mwaka ili kudhibiti manunuzi yasiyo fuata utaratibu.

Hebu tuangalieni hili swala kwa jicho la tatu hivi Framework contract na GPSA wana add value gani kwenye mchakato wa manunuzi?

Mh. Rais tuondolee huyu mdudu anaitwa framework contract inaongeza vyanzo vya rushwa na gharama zisizo za msingi.
GPSA ni mojawapo ya mashirika ya umma yasiyo na pesa. Kama unavyojua mishahara ya mashirika ya umma hupangwa na bodi na hivyo kuyafanya wawe wanalipana pesa kubwa.

Wanachofanya GPSA ni harakati za kutafuta mapato kwa nguvu zote ili na wao walipane vinono kama mashirika mengine ya umma.
 
Siongelei upigaji. Naongelea biashara halali. Hao unao waongelea nao wana sehemu zao za kupatia riziki. Hatuwezi kufanya kitu kimoja wote. Lakini pia hawajazuiwa. Na kupitia hii thread wale wale waliokuwa hawajui na wana interest watajifunza na ndo itakuwa mwanzo wa kujua.
Andiko langu halikukulenga wewe na mada yako, lakini ni mfano mzuri unaoweza kutumiwa kueleza matatizo yanayoendelea kwenye hizo shughuli zenu na serikali.
 
Back
Top Bottom