pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 221
- 431
Pole na pongezi kwako, naomba nikufikishie hili la TANESCO kuweka umeme kwenye nyumba imekuwa balaa, baada ya kufanya wiring ili kumpata surveyor inabidi usubiri hata miezi sita ila ukitoa chochote wanakuja kwa haraka, wakikuambia kwamba watakuletea umeme bila nguzo gharama yake ni laki tatu, ambapo watakuahidi kuwa watakuja baada ya wiki mbili hapa unaweza kusubiri miezi miwili au mitatu kama hujatoa chochote.
Cha kusikitisha zaidi ni pale eneo lako linapohitaji nguzo moja au zaidi, bei ya nguzo moja ni zaidi ya shilingi laki tano sawa na mshahara wa afisa wa serikali mwenye elimu ya shahada ya kwanza fikiria kama eneo lako linahitaji nguzo tatu mbaya zaidi watakwambia kuwa baada ya kulipa usubiri miezi miwili ila kiukweli hapa utasubiri mpaka miezi sita.
Kama haya yanayotokea ni uzembe, naomba waziri mwenye dhamana na mkurungenzi mtendaji wawajibishwe kwani wanahujumu serikali tunashindwa kufanya biashara ndogo ndogo ambazo zinahitaji umeme, hivyo kuikosesha serikali mapato.
Pia wahusika wawajibishwe kwa kutokuwa waadilifu; yaani kwa sasa mtu Akihitaji kuweka umeme ni mpaka amjue fulani hili shirika sijawahi kulielewa.