Rais Samia Suluhu Hassan umeingia madarakani kwa nguvu ya Katiba na si nguvu ya wananchii, wewe ndio ungekuwa mstari wa mbele kuitetea Katiba

Chris wood

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,667
5,008
Yaani nashangaa hadi muda huu mama yetu samia suluhu hassan ameshindwa kutoa kauli yoyote kuhusu hawa wabunge 19 wasio na chama, Licha ya kwamba uongozi wa chadema umeshaweka bayana kuwa hauwatambui hao covid 19 kama wanachama wa chadema.

Lakini tunaona wazi wazi katiba inavyo vunjwa bungeni kwa kuwaruhusu hao wabunge wasio na chama kuendelea na vikao huku wakilipwa pesa za wananchi ambazo zingeenda kusaidia hata kujenga vyumba vya madarasa
.
Nakukumbusha tu muheshimiwa wewe sii chaguo la wananchii ni katiba ndio imekufanya umekalia hiko kiti, katiba ingepindishwa kamwe usinge kuwa raisi wa hii nchi.

Ombi langu kwako muheshimiwa raisi msumeno hukata pande zote, kama wewe katiba ilivyokufanyia fair ilinde kwa nguvu zote, Toa kauli kwa spika awatimue hao covid 19 ikiwezekana na pesa zote walizolipwa wazirudishe zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo
 
Nitampa big up sana iwapo tu atafumba macho na kuurejesha kibabe ule mchakato wa katiba mpya katika bunge jipya la katiba, lenye wataalamu wengi na wanasiasa wachache wenye akili timamu.
 
Katiba inamtaka asiingilie mihimili mingine!
Na ataendeleza precedent mbaya akifanya.
 
Katiba inamtaka asiingilie mihimili mingine!
Na ataendeleza precedent mbaya akifanya.
Nikweli hiyo mihimili inajitegemea lakini serikali kuu itabaki kuwa na nguvu. Hata mahakama ikiharibu mahala fulani anaetupiwa mawe ni president.
 
Back
Top Bottom