Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 121,947
- 95,237
Mbona wewe uliajiliwa kwa kazi ya kukuna nazi hapo lumumba lkn sasa unajifanya mpiga zumari wa chakubanga?Kila mmoja atakula kwa jasho lake majungu si mtaji!
Mbona wewe uliajiliwa kwa kazi ya kukuna nazi hapo lumumba lkn sasa unajifanya mpiga zumari wa chakubanga?Kila mmoja atakula kwa jasho lake majungu si mtaji!
Chini ya ccm ujinga wote unawezekanaNa wewe unaamini huu upuuzi.Tanzania kuna watu wajinga sana
Hapana!
Tatizo letu watanzania kila mtu ni mjuziFedha za kugharamia Kurugenzi hii zielekezwe kwenye matumizi mengine. Nawasilisha!
Soma uzi kwa utulivu hutoumia ubongo. Nani kakukatalia hao uliowataja hawapo? Ikulu ni nyumbani kwangu!Tatizo letu watanzania kila mtu ni mjuzi
Hujawahi hata kufika geti la ikulu lakini unashauri kitengo kivunjwe.
Rais anatakiwa awe na mwandishi wake wa habari popote alipo hata kama ni msibani
Rais anatakiwa awe na wapiga picha wake,haiwezekani kuwa na mmoja,lazima wawe wawili na kuendelea kwa ajili ya shift na kupokezana kazi
Kunatakiwa kuwe na mtu wa mitandao ya jamii n.k
Kitengo cha habari ikulu kinatakiwa kutoa habari zote za Rais na ikulu kwa ujumla,msidhani watu wanakula raha kule
umetaka kitengo kisambaratishwe,kazi utafanya wewe?Soma uzi kwa utulivu hutoumia ubongo. Nani kakukatalia hao uliowataja hawapo? Ikulu ni nyumbani kwangu!
Ngoja nisubiri wengine waseme, mie nitakuwa wa mwisho.Posho day mil 15....huo ni mshahara wangu wa miaka 5
Salva hajawahi kumiliki gazeti. Mtanzania, Rai, Dimba na The African chini ya New Habari Cooperation ni Mali ya Rostam Aziz. Huko nyuma kampuni ikiitwa Habari Cooperation ilimilikiwa na Jenerali Ulimwengu kabla ya kuuza kampuni hiyo na kuanzisha Raia Mwema. Salva alikuwa Mhariri na Mchambuzi.Gazeti la Mtanzania?
Soma uzi uelewe au unatumia kiungo gani kuelewa?umetaka kitengo kisambaratishwe,kazi utafanya wewe?
National cake.Kwa siku posho $6700 = TShs 15,443,500/=
Kuna baadhi ya watu wanaifaidi hii nnchi aisee
Huo ni wivu na majungu. Mkurugenzi hiyo ina majukumu mazito ndomaana kikaanzishwa na tunaona uwajibikaji katika utoaji habari, uendeshaji hafla na shughuli zingine za ikulu.
Tumeona juzi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiteua wasaidizi kadhaa ktk masuala mbalimbali. Ikulu ni taasisi hivyo inapaswa kuwa na Mkurugenzi.
Yawezekana nawe ni miongoni mwa waliopunguzwa Ktk Jiko LA Ikulu hivyo unaoenda mkose wote.
Kwamba Msigwa kajaza washkaji wake, sio jambo LA kweli, Ikulu hawawezi kuwa kama N. G.O, kutoa ajira kiholera namna hiyo.
Acha Msigwa apige kazi, kijana hodari sana na mchapa kazi. Kazi Iendeleee.
Naunga mkono hoja. Mama apewe muda na sapoti ajipange. Mpaka sasa anakwenda vizuriMimi Wala Sina Shida ni nani awepo wapi wakati huu ila ili Mama afanye kazi yake vizuri tumpe muda ajipange..
Hii kazi na style aliyochukua nchi ni tofauti sana..Akianza kufukuza wote mara moja wakati ndio anajipanga anaweza kuharibu zaidi...
Kazi ya Urais ni ngumu sana ...sio rahisi sana kama mnavyowaza..Mpeni Muda ajitulize kwenye kiti kile.
Hii kurugenzi iendelee hata kama ilianzishwa kimagumashi kumpa ulaji salva
Shida yako ulitaka kusema kuhusu corona au ghalama za hiyo kurugenzi?Wanabodi Shaloom!
Ninakuomba kama itakupendeza futilia mbali Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili fedha za umma zinazoteketea kuligharamia zitumike kwingine. Ni kitengo cha upigaji.
Nikukumbushe: mwaka 2005 baada ya Jakaya kuingia madarakani ndipo kitengo hiki kiliundwa mahsusi kumpa Salvatory Rweyemamu ulaji kwa kazi kubwa aliyoifanya kumpamba Jakaya na kuwachafua wapinzani wake kupitia gazeti la RAI Nguvu ya Hoja.
Nafasi za Ubunge, Uwaziri, U-DC au RC hazikuonekana "kumtosha" Salva ndipo alipopendekeza kuwepo na Kurugenzi hiyo ili asafiri na Rais popote duniani na posho ya dola 6700 kwa siku kwa kila safari nje ya nchi.
Rais Magufuli alipoingia naye akaridhi kitengo hiki cha upigaji hela za umma akimweka Gerson Msigwa ambaye naye akawaalika "washikaji" wake kujazana hapo bila kazi maalum zaidi ya kupiga hela. Ofisi ina watu 13 lakini uliza kazi ya kila mmoja ni nini?
Magufuli alisambaratisha kitengo cha Jikoni-Ikulu iliyokuwa na watu zaidi ya 100 akisema, "nitapikiwa na mke wangu". Kilikuwa cha upigaji sawa na hii Kurugenzi.
Unajiuliza Rais anaye Katibu wake, Mwandishi wake wa Habari, Mpigapicha, nini kazi ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu? Hivi kuandika barua za teuzi na tenguzi ni za kuajiri Mkurugenzi na Idara hewa chini yake? Nini kazi ya Msemaji Mkuu wa Serikali?
Sasa tunaona Msigwa ndiye Msemaji wa Serikali na wakati huo ndiye Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu (Serikali). Huku ni kuchanganya Mawasiliano ndio maana tulishuhudia JPM akikana uwepo wa Covid-19 na Dk. Abbas akikiri kuwepo Corona. Ikulu vs Idara ya Habari MAELEZO.
Fedha za kugharamia Kurugenzi hii zielekezwe kwenye matumizi mengine. Nawasilisha!
#FreedomIsBack
Vipi umekopeshwa bundle!Mbona wewe uliajiliwa kwa kazi ya kukuna nazi hapo lumumba lkn sasa unajifanya mpiga zumari wa chakubanga?