Rais Samia Suluhu Hassan, ondoa kikwazo hiki na historia itakukumbuka

Dr.Godbless

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
828
1,000
Katika mabadiliko ya nafasi za kisiasa tumekuwa tukishuhudia kila Rais mpya anataka kuteua safu yake ya uongozi kuanzia wa kisiasa na kiutendaji kwa mujibu wa maelekezo ya kikatiba na kisheria.

Sina tatizo na nafasi za kisiasa kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwa nadharia kwamba safu ya utendaji inaweza kudhibiti mabadiliko husika, lakini hili linaweza kuwa practical kama Watendaji wa Serikali watakuwa katika nafasi zao bila kuathiriwa na mabadiliko ya nafasi za kisiasa.

Mathalani kati ya 2015- 2021 kumekuwa na mabadiliko ya nafasi ya KM Wizara ya Afya kwa takribani mara 5.

Nashawishika kuwa mabadiliko ya mara kwa mara katika eneo la utendaji linachangia kupalilia umasikini nchini kwa namna mbalimbali, mfano.

1. Teuzi za watu wapya kwenye mfumo wa ajira zinaambatana ongezeko la ajira mpya zenye malipo makubwa, na hivyo kuongeza matumizi ya fedha za umma.

2. Hata wale wanaoondolewa katika nafasi zao inabidi watafutiwe eneo jingine au walazimike kusubiri nafasi iliyo wazi ili kuijaza. Kwa nyakati zote hizo wanapokea mishahara yao kama kawaida. Mfano ilitokea wakati wa mabadiliko ya DED nchi nzima, wale tu alioondolewa walikosa eneo la kazi na kilichofanyika ni kuwekewa dawati kwenye ofisi ya DED mpya ili amsaidie majukumu.

3. Kwa uchanga wa mifumo yetu,utendaji mzuri wa taasisi zetu hutegemea sana utendaji wa mtu kuliko mfumo uliopo. Kwa kifupi hatuna mifumo ya kiuwajibikaji bila kuwa na Kiongozi mwajibikaji. Hivyo mabadiliko ya mara kwa mara ya kuondoa wa zamani na kuweka wapya bila kuzingatia kigezo cha utendaji kinaacha taasisi katika majeraha makubwa ya kiutendaji.

Kwa muktadha huu, Rais aliyepo madarakani aelekeze mabadiliko ya kisheria ili kuruhusu yafuatayo;
1. Uteuzi wa nafasi za utendaji katika sekta za huduma zinaweza kufanywa kwa kuzingatia uwazi wa vigezo na sababu ya teuzi husika. Mfano kilichotokea katika uteuzi wa Mkurugenzi wa TPDC na baadae kufutwa ni kutokana na ukosefu wa uwazi na sababu zinazopelekea tauzi hizi. Aidha ni muhimu sana nafasi hizi kuthibitishwa na Bunge ili kuweka uwajibikaji kwa umma.

2. Kuweka utaratibu wa kutengua nafasi husika ambapo Rais anaweza kulijulisha Bunge juu ya sababu ya kutengua uteuzi huo. Hii itasaidia kuweka mazingira mazuri ya uwajibikaji. Kwa jinsi ilivyo hakuna anayejua sababu hasa za kuteua huyu na kuondoa yule.

3. Uteuzi wa nafasi za utendaji katika sekta za kibiashara mfano TTCL, TPDC, ATCL, TANAPA, EWURA, TPA na kadhalika unapaswa kuzingatia weledi na uzoefu wakibiashara katika sekta husika. Haitoshi kuchukua Prof fulani kutoka idara ya Petroli Udom ili kuwa Mkurugenzi wa TPDC, Haitoshi kuteua Prof fulani kutoka ndaki ya IT UDSM kuwa Mkurugenzi wa TTCL.

Ambacho kinatakiwa kufanyika ni nafasi hizi kuwekwa wazi ili wenye vigezo na sifa kufanya maombi na kupita katika interviews. Na baada ya watatu kupatikana majina yanaweza kupelekwa kwa Rais ili kuchagua mmoja. Watendaji hawa wanapewa ajira za malengo. Na usipofikia malengo automatically ajira yako inakuwa imekoma. Hili litasaidia kumpa Rais wigo mpana wa kuteua hata wale ambao si makada wa CCM na hawana vyama.

#PublicSectorNeedSustainability
 

Dira Kali

JF-Expert Member
Dec 12, 2020
327
500
Nimekuelewa vema mheshimiwa!

Yes, sheria iwepo tupunguze utashi Wa mtu binafsi katika uteuzi. Teuzi katika mashirika nyeti ya umma zifuate mwongozo makini wa kisheria usiyoyumbayumba!
 

Silly

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
552
250
Big brains at work, mawazo mazuri sana nimeelewa kwenye kuweka misingi ili mfumo ufanye kazi, inawezekana mfumo ukajengwa kuanzia sasa na ndani ya miaka miwili ukawa umekamilika.

Natamani watawala wangekuwa wanapita humu kuona mawazo +ve na kuyaweka kwenye think archive zao.
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
9,731
2,000
Rais abaki kuteua mawaziri, mabalozi, wakuu wa vyombo vya usalama na majaji(waliopendekezwa na TLS pamoja na mahakama)

Nafasi nyingine zote za utumishi wa umma zipitie sekretarieti ya ajira utumishi, zitangazwe watu watume maombi, wafanyiwe usaili wa wazi, watakaopatikana wathibitishwe na waziri wa wizara husika akishirikiana na kamati za bunge husika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom