Rais Samia Suluhu Hassan; Muda si Rafiki kwako, unahujumiwa na hao hao unaowalea na kuwaonea aibu

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,581
Kwako Rais,

Najua itakufikia hii makala, ila sijui kama utaifanyia kazi.

Kumbuka, sisi wana JamiiForums (Mnaotuita Viherehere Wa Mitandaoni) kuanzia mwanzo wa safari yako ya Urais, speech zako za awali zilitupa moyo sana na kutufuta machungu ya awamu iliopita (Miaka 5 iliopita). Tulipata amani na kushusha pumzi nzito kuona hatimae mwokozi wa taifa amepatikana. Tukajikuta tunakuunga mkono na kukupa support licha ya itikadi zetu za kichama.

Safari ilipo anza tuliona mwangaza ukilimulika taifa, hakika tulipata ari ya kuungana wananchi na kuwa wamoja. Tulikua wamoja na maono ya pamoja.

Ila usafiri wetu kama taifa, ulianza kutoka nje ya njia pale ulipo tangaza baraza la mawaziri, tupo tulioshangaa na kusikitika sana, tulikuonya na kukusihi kwamba baraza lako la mawaziri lina kasoro na hitilafu za kiufundi ambayo itazua ajali huko mbeleni. Mabadiliko yalihitajika haraka sana kabla ya kuendelea na safari.

Miongoni mwa hitilafu za ufundi ni kuna Mawaziri uliowateua siku ile tuliwakubali, na kuna Mawaziri tulikupigia kelele hawakufai na watakurudisha nyuma sambamba na kukuhujumu. Uliziba masikio na haukutusikiliza. Pengine kiti ulikua hujakizoea vizuri bado. Tukapiga moyo konde kwa kusubiri uzoee kiti na pia kusubiri kujionea yajayo.

Sasa tumefika tulipokua tukipasubiri, umefika ulipokua ulipokua unapafumbia masikio na macho, sio kwa nia mbaya, ila kwa kukataa kutusikiliza wananchi wako wenye nia njema kwako.

Hujuma zimeanza, fitina zimeshika kasi, kashikashi zimewasili, na uzalendo umebakia kwa kuvaa tai zenye rangi ya bendera ya tanzania.

Uliowa amini katika baraza lako la mawaziri, ambao sisi tulikupa onyo, wameanza ya kuanza (Kukusaliti na kuandaa njia ya kukaa katika kiti ulicho kalia).

Bila kupepesa macho, nao ni kijana wa Iramba Singida & Co Ltd.

Simple logical theory wanayotumia Kijana Wa Iramba Singida & Co Ltd;

SSH unatakiwa utingishwe kisawasawa na kukoseshwa imani kwetu wananchi na ndani ya chama, haya naweza kusema yameshatimia kwa asilimia 80%. Bado asilimia 20% tu.

Nayo kwa ufupi ni kwa;

1) Ufitinishwe na wananchi kwa kupandisha kodi/tozo kwa wanyonge (Miamala Ya Simu, Wakulima, Wavuvi), kuua mzunguko wa hela ndani ya nchi kwa kisingizio cha kuongeza mapato na makusanyo ya fedha. Hapa ametumika Kijana Wa Iramba Singida.

2)
Ufitinishwe na vyombo vya Usalama kwa kukuonesha umekurupuka kwenye maamuzi yako ya Chanjo za Covid 19, na kwamba unataka kuviweka hatarini vyombo vya usalama.

Sambamba na kuzua taharuki kwa wananchi na vyombo vya usalama vya taifa letu. Taharuki imeanza kuzuka na malumbano hatimaye yameanza kufukuta chini kwa chini. Hapa ametumika Askofu Gwajima.

3)
Ufitinishwe na dunia nzima kwa kuwapa viongozi wa upinzani kesi za Ugaidi na kuzuia waumini wa dini kuwaombea viongozi wao. Kuwakamata viongozi wa kiroho na kuwaweka mahabusu. Hapa vimetumika vyombo vya Police.

4)
Ukose kuungwa mkono na CCM wenyewe ndani kwa ndani kwa kuona huna msimamo thabit na ni dhaifu. Hapa itatumika CCM yenyewe kwenye vikao vya NEC taifa.

5)
Upinzani wapambishe moto kudai Katiba Mpya. Hapa walianzisha Upinzani na Viongozi Wa Kiroho.

6) Kijana Wa Iramba Singida aanze mapema ya kutafuta point/hamasa kwa wananchi kwa kufanya ziara yenye msafara kama wa JPM. Aonekane yeye ndio anajali wananchi kuliko Rais na Makamu wake.

Atembee na kusimama ziarani kusikiliza kero za wananchi ili wakuone Rais SSH wala Makamu Dk Mpango hamna time na wananchi wako pia upo bussy kwenda ziara nje ya nchi kama Burundi. Kijana Wa "Iramba Singida" kaishaanza hizi ziara hatari.

7)
Mapigo yaanzie "Kaskazini - Magharibi" (Mwanza) kwa upinzani kudai Katiba Mpya kwa nguvu zote, na ya Kijana Wa Iramba Singida yaanzie "kusikini" (Mtara - Tunduma) kujifanya anasikiliza kero za wananchi.

Wakati huo huo Jeshi La Polisi likicheza na "Magharibi" (Dar Es Salaam) kwa kumshikilia Freeman Mbowe na viongozi wengine wa upinzani kwenye kesi ya Ugaidi. Formation Three In One.

Pia walio shitakiwa kwa kumteka Mo Dewj waachiliwe. Siku ya leo Twalib (Dereva Tax) ameachiliwa huru kwa kigezo Jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi hio.

8) Utoe matamko yatakayoonesha hauna msimamo madhubuti kukufanya uonekane wewe ni kigeugeu ndani ya chama, ndani ya nchi na nje ya nchi.

Mama cha ajabu bado hujaisoma katika radar zako hii vita, vita si ndogo na pengine wanaokushauri wanakupa moyo na kukudanganya.

Kama ukiendelea kuwalea hao viumbe unao waamini, huchomoki kwenye mabano ya CCM wenzako wenye uchu wa madaraka. Nikukumbushe, ndio kwanza 2021 mpaka 2025 ni mwendo wa masafa marefu na ujiandae kwa kuvaa viatu vizuri tu Mama (Safety Boots).

Wamejipanga na wakapangika, mahesabu ni makali sana dhidi yako. La mwisho kukusihi ni Kijana Wa Iramba na Askofu Gwajima hawakufai hawakufai hawakufai katika chama na serikali yako.

Ukisikiliza ni sawa, na usiposikiliza ni sawa. Sisi kama viherehere mnavotuita, hatutakua na muda wa kukukumbusha tena hilo. Kazi yetu itakua ni kukukosoa na kukuzodoa kwa kutokutusikiliza.

NOTE THAT: Upinzani sio maadui wa taifa wala sio magaidi, maadui wa taifa na magaidi ni hao hao unao walea na kuwadekeza.

Wako mtiifu,
Adui wa CCM, Raia Mwema Mwenye Upendo Kwa Taifa.

Alexander The Great

Rais%20SSH.jpg
 
Power struggle. Ila wameanza mapema
Huo ndio ujinga wao kwenye mahesabu, Character assasination wamefanya mapema sana mtu hajamaliza hata mwaka mmoja madarakani, njaa ikizidi akili huwa zinaruka pyuuuuuuuh, ilipaswa mikakati hii kuwa 2024 huko au 2025 mwanzoni.

Pia wrong timing, kwasababu upinzani ulishawahi kuanzisha amsha amsha za Katiba Mpya. Wao walipaswa wawe wamoja ili kumeza mikiki-mikiki ya upinzani kudai katiba badala ya kufarakana kichama.

Maybe, just maybe, chama tawala wanataka kumtoa madarakani kwa kupitia kura ya kutokua na imani nae katika vikao vya chama kitaifa. Kama walivyomfanyia Rais Mzee Mwinyi katika uongozi wake.
 
Kwani hiyo ndiyo political strategy ya kijana wa iramba singida? Je yule kijana wa bumbuli tanga yeye ndio basi tena amekata tamaa? Mambo mengine ni insidently tu hayakupangwa
 
Yule amepata akili sasa, ameanza kujua jinsi ya kucheza vigodoro/amaboko na wakubwa zake. Siku ya leo katoa tamko la kulaani baadhi ya viongozi wa chama kutoa kauli kwa wananchi wao za kugeuka/kupinga matamko ya mwenyekiti wa chama tawala.

Kijana wa Bumbuli amem target Gwajima ili kujivuta kwa SSH, pengine ameona akifanya hivo mama na yale macho yake ya mlegezo atamuweka kwenye PDF za Gerson Msigwa za usiku wa manane.
 
Huo ndio ujinga wao kwenye mahesabu, Character assasination wamefanya mapema sana mtu hajamaliza hata mwaka mmoja madarakani, njaa ikizidi akili huwa zinaruka pyuuuuuuuh, ilipaswa mikakati hii kuwa 2024 huko au 2025 mwanzoni.

Pia wrong timing, kwasababu upinzani ulishawahi kuanzisha amsha amsha za Katiba Mpya. Wao walipaswa wawe wamoja ili kumeza mikiki-mikiki ya upinzani kudai katiba badala ya kufarakana kichama.

Maybe, just maybe, chama tawala wanataka kumtoa madarakani kwa kupitia kura ya kutokua na imani nae katika vikao vya chama kitaifa. Kama walivyomfanyia Rais Mzee Mwinyi katika uongozi wake.
HAKUBALIKI
 
Nyie watu wa chadema ni wapumbavu sana ukiwemo wewe mtoa post
Hivi mnamchukulia poa Sana Samia? Kwamba yeye ni mjinga sana hadi sijui afitinishwe? Eti Kuna watu kwenye serikali yako wanakufitinisha,nyie ndio mnaojua hao watu kuliko yeye ambaye ni boss wao?
Wapumbavu wakubwa nyie

Umetumia risasi kuua mbu aliyepo kwenye “balls “

Sijui kama utapona!
 
Ndio kusema kwamba wewe unajua sana nchi kuliko hata anayeiongoza?.mama anawashauri mbona wengi.wewe ndio unawivu na watu.Fanya yako sio kila siku mnataka watu wafukuzwe kazi.fukuza wakwako hata mkeo fukuza.unachokiona kibaya kwako cc wengine twakiona chema.hyo mihemko yako pelekea mkeo
 
Kwani hiyo ndiyo political strategy ya kijana wa iramba singida? Je yule kijana wa bumbuli tanga yeye ndio basi tena amekata tamaa? Mambo mengine ni insidently tu hayakupangwa
 
Mama ameshikilia msimamo kwamba kodi/tozi hazifutwi. Sasa wananchi tunaafiki maamuzi gani?
Si kwenye mada yako unasema ana haribiwa na kundi flani la kina Mwigulu?

Sasa mwenyewe kasema waliweka na yeye akiwemo!

Tatizo la bavicha ni ujinga na si kingine
 
Kwako Rais,

Najua itakufikia hii makala, ila sijui kama utaifanyia kazi.

Kumbuka, sisi wana JamiiForums (Mnaotuita Viherehere Wa Mitandaoni) kuanzia mwanzo wa safari yako ya Urais, speech zako za awali zilitupa moyo sana na kutufuta machungu ya awamu iliopita (Miaka 5 iliopita). Tulipata amani na kushusha pumzi nzito kuona hatimae mwokozi wa taifa amepatikana. Tukajikuta tunakuunga mkono na kukupa support licha ya itikadi zetu za kichama.

Safari ilipo anza tuliona mwangaza ukilimulika taifa, hakika tulipata ari ya kuungana wananchi na kuwa wamoja. Tulikua wamoja na maono ya pamoja.

Ila usafiri wetu kama taifa, ulianza kutoka nje ya njia pale ulipo tangaza baraza la mawaziri, tupo tulioshangaa na kusikitika sana, tulikuonya na kukusihi kwamba baraza lako la mawaziri lina kasoro na hitilafu za kiufundi ambayo itazua ajali huko mbeleni. Mabadiliko yalihitajika haraka sana kabla ya kuendelea na safari.

Miongoni mwa hitilafu za ufundi ni kuna Mawaziri uliowateua siku ile tuliwakubali, na kuna Mawaziri tulikupigia kelele hawakufai na watakurudisha nyuma sambamba na kukuhujumu. Uliziba masikio na haukutusikiliza. Pengine kiti ulikua hujakizoea vizuri bado. Tukapiga moyo konde kwa kusubiri uzoee kiti na pia kusubiri kujionea yajayo.

Sasa tumefika tulipokua tukipasubiri, umefika ulipokua ulipokua unapafumbia masikio na macho, sio kwa nia mbaya, ila kwa kukataa kutusikiliza wananchi wako wenye nia njema kwako.

Hujuma zimeanza, fitina zimeshika kasi, kashikashi zimewasili, na uzalendo umebakia kwa kuvaa tai zenye rangi ya bendera ya tanzania.

Uliowa amini katika baraza lako la mawaziri, ambao sisi tulikupa onyo, wameanza ya kuanza (Kukusaliti na kuandaa njia ya kukaa katika kiti ulicho kalia).

Bila kupepesa macho, nao ni kijana wa Iramba Singida & Co Ltd.

Simple logical theory wanayotumia Kijana Wa Iramba Singida & Co Ltd;

SSH unatakiwa utingishwe kisawasawa na kukoseshwa imani kwetu wananchi na ndani ya chama, haya naweza kusema yameshatimia kwa asilimia 80%. Bado asilimia 20% tu.

Nayo kwa ufupi ni kwa;

1) Ufitinishwe na wananchi kwa kupandisha kodi/tozo kwa wanyonge (Miamala Ya Simu, Wakulima, Wavuvi), kuua mzunguko wa hela ndani ya nchi kwa kisingizio cha kuongeza mapato na makusanyo ya fedha. Hapa ametumika Kijana Wa Iramba Singida.

2)
Ufitinishwe na vyombo vya Usalama kwa kukuonesha umekurupuka kwenye maamuzi yako ya Chanjo za Covid 19, na kwamba unataka kuviweka hatarini vyombo vya usalama.

Sambamba na kuzua taharuki kwa wananchi na vyombo vya usalama vya taifa letu. Taharuki imeanza kuzuka na malumbano hatimaye yameanza kufukuta chini kwa chini. Hapa ametumika Askofu Gwajima.

3)
Ufitinishwe na dunia nzima kwa kuwapa viongozi wa upinzani kesi za Ugaidi na kuzuia waumini wa dini kuwaombea viongozi wao. Kuwakamata viongozi wa kiroho na kuwaweka mahabusu. Hapa vimetumika vyombo vya Police.

4)
Ukose kuungwa mkono na CCM wenyewe ndani kwa ndani kwa kuona huna msimamo thabit na ni dhaifu. Hapa itatumika CCM yenyewe kwenye vikao vya NEC taifa.

5)
Upinzani wapambishe moto kudai Katiba Mpya. Hapa walianzisha Upinzani na Viongozi Wa Kiroho.

6)
Kijana Wa Iramba Singida aanze mapema ya kutafuta point/hamasa kwa wananchi kwa kufanya ziara yenye msafara kama wa JPM. Aonekane yeye ndio anajali wananchi kuliko Rais na Makamu wake.

Atembee na kusimama ziarani kusikiliza kero za wananchi ili wakuone Rais SSH wala Makamu Dk Mpango hamna time na wananchi wako pia upo bussy kwenda ziara nje ya nchi kama Burundi. Kijana Wa "Iramba Singida" kaishaanza hizi ziara hatari.

7)
Mapigo yaanzie "Kaskazini - Magharibi" (Mwanza) kwa upinzani kudai Katiba Mpya kwa nguvu zote, na ya Kijana Wa Iramba Singida yaanzie "kusikini" (Mtara - Tunduma) kujifanya anasikiliza kero za wananchi.

Wakati huo huo Jeshi La Polisi likicheza na "Magharibi" (Dar Es Salaam) kwa kumshikilia Freeman Mbowe na viongozi wengine wa upinzani kwenye kesi ya Ugaidi. Formation Three In One.

Pia walio shitakiwa kwa kumteka Mo Dewj waachiliwe. Siku ya leo Twalib (Dereva Tax) ameachiliwa huru kwa kigezo Jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi hio.

8) Utoe matamko yatakayoonesha hauna msimamo madhubuti kukufanya uonekane wewe ni kigeugeu ndani ya chama, ndani ya nchi na nje ya nchi.

Mama cha ajabu bado hujaisoma katika radar zako hii vita, vita si ndogo na pengine wanaokushauri wanakupa moyo na kukudanganya.

Kama ukiendelea kuwalea hao viumbe unao waamini, huchomoki kwenye mabano ya CCM wenzako wenye uchu wa madaraka. Nikukumbushe, ndio kwanza 2021 mpaka 2025 ni mwendo wa masafa marefu na ujiandae kwa kuvaa viatu vizuri tu Mama (Safety Boots).

Wamejipanga na wakapangika, mahesabu ni makali sana dhidi yako. La mwisho kukusihi ni Kijana Wa Iramba na Askofu Gwajima hawakufai hawakufai hawakufai katika chama na serikali yako.

Ukisikiliza ni sawa, na usiposikiliza ni sawa. Sisi kama viherehere mnavotuita, hatutakua na muda wa kukukumbusha tena hilo. Kazi yetu itakua ni kukukosoa na kukuzodoa kwa kutokutusikiliza.

NOTE THAT: Upinzani sio maadui wa taifa wala sio magaidi, maadui wa taifa na magaidi ni hao hao unao walea na kuwadekeza.

Wako mtiifu,
Adui wa CCM, Raia Mwema Mwenye Upendo Kwa Taifa.

Alexander The Great

Mwandishi nimekuelewa
 
Back
Top Bottom