Rais Samia Suluhu Hassan, mteue Zitto Zuberi Kabwe awe Mbunge akaongeze chachu ya hoja Bungeni

Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,561
2,000
Bunge letu linahitaji kuongezewa chachu ya aina fulani ili liweze kuichambua kikamilifu Miswada ya Serikali.

Vile vile Bunge letu linahitaji Sauti ya Upinzani yenye kukubalika mbele ya jamii yetu ya Kitanzania.

Kwa kuwa Kada wawili wa CCM wamekuwa Wabunge wa Kuteuliwa, Humphrey Polepole na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, basi ikimpendeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, itapendeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe wa ACT-Wazalendo, akateuliwa kuwa Mbunge, katika zile nafasi za Rais.

Hali hii itaimarisha Muungano wetu kwa kuwa ACT-Wazalendo imekubali kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

CCM, kwa upande wa Tanzania Bara, itakuwa imeungana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuonesha dhamira njema ya kushirikiana na makundi yote ndani ya Nchi yetu, katika kuijenga Nchi yetu.
Zitto alipigwa jimboni sasa anaombewa ubunge wa hisani
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,102
2,000
Hahaaaa mwami kama mwami sasa anaombewa Ubunge kwa Mama , hatari sana yaani mambo yanakwwenda kasi sana jamani
 
Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,748
2,000
Sina hakika kama WanaKigoma wote watakubaliana na wewe.
Jamii zetu Tanzania zina kundi dogo la Wafiachama, ambalo kwalo Nchi inakuja baada ya Chama.
Kundi hilo dogo linafurahia Wabunge wote watoke CCM, Madiwani wote watoke CCM.
Kwa wale wengi wanaoipenda Nchi yao kuliko Vyama vyao, wanaamini kuwa SAUTI MBADALA Bungeni inaimarisha AFYA ya Taifa.
Sauti ya Zitto Bungeni ni Sauti Mbadala.
Wanakigoma mpaka sasa wanashangilia kugaragazwa kwa huyo jamaaa yenuuu. Kama zito anafaa siuombe aje awe mbunge wa jumbo lenu hapo ufipani??
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,555
2,000
Kila nikiliangalia Bunge letu la miaka hii minne iliyobaki, na kauli ya Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kueleza bayana kuwa Serikali yake iko tayari kukosolewa, Mbunge aina ya Zitto Zuberi Kamwe, mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja, ni faida sana kuwa nawe Bungeni.
kazi za mbunge ni.kujenga hoja kwa ajili ya watu wa jimboni.kwake bungeni .Zitto hoja zipi nzito alizowahi jenga kwa ajili ya jimbo lake? Lisu pia hoja zipi alizowahi jenga kwa ajili ya watu wa jimbo lake? tuanzie hapo
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,811
2,000
Katika miaka yake 15 bungeni ambayo alikuwa anafanya ukosoaji nini kimebadilika??
Kukosoa kwa staha, kwa lugha ya Kibunge, na hoja ikafanyanyiwa kazi na Serikali, kwa mujibu wa Katiba yetu, inabidi awe Bungeni.
Ndiyo, ni vizuri kukosoa ukiwa Bungeni.
 
gasper jj

Member
Nov 13, 2012
18
45
Bunge letu linahitaji kuongezewa chachu ya aina fulani ili liweze kuichambua kikamilifu Miswada ya Serikali.

Vile vile Bunge letu linahitaji Sauti ya Upinzani yenye kukubalika mbele ya jamii yetu ya Kitanzania.

Kwa kuwa Kada wawili wa CCM wamekuwa Wabunge wa Kuteuliwa, Humphrey Polepole na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, basi ikimpendeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, itapendeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe wa ACT-Wazalendo, akateuliwa kuwa Mbunge, katika zile nafasi za Rais.

Hali hii itaimarisha Muungano wetu kwa kuwa ACT-Wazalendo imekubali kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

CCM, kwa upande wa Tanzania Bara, itakuwa imeungana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuonesha dhamira njema ya kushirikiana na makundi yote ndani ya Nchi yetu, katika kuijenga Nchi yetu.
TANZANIA INA WATU WENGI WENYE UWEZO SAWA NA ZITTO NA WAPO WALIOMZIDI, SEMA HAWAJAPATA FURSA ALIZOWAHI PATA ZITTO. NAFIKIRI ILI UPINZANI UJIIMARISHE NI VYEMA WASIWE WANAPEWA VYEO VYA HISANI KWANI VINALETA UKAKASI HUKO MBELENI JARIBU KUMUWAZA A.E. MREMA, NA MBATIA JE VYEO WALIVYPEWAGA VILISAIDIA JAMII YAO AU WATZ ZAIDIZAIDI VILIWASAIDIA WAO KWA MUDA FULANI MWISHOWE VIKATUONDOLEA IMANI KWAMBA WALE NI WAPINZANI HALISI, SISHAURI ZITTO AINGIE KWENYE MTENGO HUO KWANI BADO ANANAFASI YAKUFANYA HAYO UNAYOSEMA NA ZAIDI AKIWA NJE YA BUNGE CHA KUSHAURI NI PAWEPO NA TAASISI IMARA NA MADHUBUTI YENYE KUHESHIMU SHERIA NA HAKI YA RAIA WAKE, UHURU WA MAWAZO KINZANI HATA KAMA MUNATOKA CHAMA KIMOJA PASIWE NA WEWE NI MWENZETU USITUKOSOE. HATA NDANI YA CCM WAKIACHA U CCM WAKAJIPAMBANUA KUIJENGA TANZANIA KULIKO KUWAZA CHAMA WANAWEZA TUSAIDIA SANA.(REJEA BASHE KABLA YA KUPEWA UNAIBU WAZIRI PIA REJEA NAPE BAADA YAKUTUMBULIWA UWAZIRI WA HABARI) ALAFU HEBU TUWATIZAME KAMA JENERAL ULIMWENGU, ISSA SHIVYA , TUNDU LISU N.K WASIKUTANENA VIZUIZIVYOVYOTE PALE WANAPOTOA MAWAZO HURU NACHNYA AMBAYO NI MWARUBAINI WA SEREKALI
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,811
2,000
Ubunge wa viti maalum na kuteuliwa ufutwe.
Ni ufujaji tu wa pesa za walipa kodi wavuja jasho.
Unapendekeza nani aende huko badala ya Zitto?
Huko nyuma, Rais Kikwete aliwahi kumteua Mhe. Mbatia kuwa Mbunge.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom