Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara ya siku 3 Nchini Misri

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 10 Novemba, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Cairo nchini Misri kwa Ziara ya Kiserikali ya siku tatu.

Ziara hiyo ya Kiserikali ya siku tatu inafuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Samia pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii

Mhe. Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja (]) na hati saba (7) za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.

CA3E7C61-39E8-4AB9-B209-98C9F5752AAD.jpeg


9A454D4E-447A-4876-928C-9E2B92FC3A66.jpeg
 
Hivi anafahamu kweli kuhusu huu mfumuko wa ghafla wa bei wa bidhaa mbalimbali na hasa zile muhimu? Au ndiyo ameamua tu kuwaachia wafanyabiashara wasio waaminifu kujiamulia vile wapendavyo!

Anashindwa hata kumwagiza Waziri mkuu/Waziri mwenye dhamana kufanya uchunguzi juu ya jambo hili! Au anafahamu kinacho endelea na hivyo ameona ni wakati wake kupuyanga kwa watu, huku wananchi wakiendelea kuumia?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 10 Novemba, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Cairo nchini Misri kwa Zara ya Kiserikali ya siku tatu.

Ziara hiyo ya Kiserikali ya siku tatu inafuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Samia pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za
diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii

Mhe. Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja (]) na hati saba (7) za makubaliano kati va Tanzania na Misri.

View attachment 2004534

View attachment 2004542
Tunaanza kulaumu saa ngapi jamani?
 
Hivi Kwa ziara ya kualikwa Kama hii je huo mkataba na hizo hati zinazosainiwa zinakuwa zimeandaliwa na nchi gani?
Wataalamu wa wizara kisekta pande zote na ofisi ya wataalam wa ofisi ya mwanasheria mkuu.
 
Back
Top Bottom